Kwa nini?

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
Wakati akiwahutubia wananchi kupitia salamu zake za mwisho wa mwaka, rais Kikwete alitoa hotuba iliyoonyesha kuwa hali mambo si mbaya sana nchini. Hotuba yake ilionyesha ingawa kuna matatizo ya hapa na pale, hali inatia matumaini na tunasonga mbele kama tulivyopanga.

Lakini nilipoiona hotuba aliyoitoa leo katika sherry party kwa mabalozi, nimepatwa na mshituko kwani anaonyesha kabisa kuwa mambo si mazuri nchini.

Hivi, waungwana mna habari kuwa serikali yetu inaandaaa bajeti ndogo ili kukabiliana na matatizo ya kuuchumi ambayo yemejitokeza? basi amewaeleza mabalozi leo kuwa ili kupaya Sh6.7 bilioni ili kutengeneza miundombinu iliyoharibiwa na mvua, serikali itachota fedha hizo kutoka katika wizara na idara zake katika mafungu ya bajeti ya mwaka huu.

Amesema wazi kwahiyo inamaanisha kuwa serikali italazimika kuachana na baadhi ya mipango yake kwa mwaka huu. Amewaeleza pia kuwa baadhi ya mipango na programu zitapunguziwa fedha.

Hii ndio hali halisi ya uchumi wetu, aliwaeleza mabalozi.

Kinachonishangaza ni kwa nini alipotuhutubia watu wake juzi juzi tu hapa hakutueleza haya? Anatupaka mafua kwa mgongo wa chupa?
 
Kama hili ndilo tatizo:
- kutengeneza miundombinu hiyo inagharimu bilioni 6.7

Suluhisho haliwezi kutoka hapa:
- Kuandaa programu ya kusupport soka la Tanzania bilioni 7
- Nyumba ya Magavana Bilioni 2.6
-
 
Back
Top Bottom