Amesikika Zungu akiongelea masuala ya Internet:
Zungu hana ufahamu wowote wa kuhusu Internet zaidi ya kuwa yeye ni mtumiaji kama mtu mwingine tu.
Cha kushangaza ni kuwa ameachwa kuendelea na upotoshaji wake tena kwa raha zake.
Wataalam, TCRA, wasomi, vyuo nk wapo ila wote kimya! Utadhani wamemwagiwa maji. Hii ndiyo Tanzania sasa, nani mwenye kumfunga pale kengele?
"Kabla ya kuandika uzi huu ilibidi kujridhisha kwa kupata maoni ya wadau mbali mbali wakiwamo wabobezi kweli kweli."
Hapa chini ndiyo ulio ukweli:
1. Internet ni mtandao uliokua kimataifa kufika sehemu mbali mbali kwa wahitaji kujiunganisha kutokea katika sehemu ya karibu ulipo (point of presence).
2. Gateways ni points za kuingilia kuliko na internet kunapokuwepo pia vifaa husika vya kuwezesha kujiunganisha kwenye hizo points of presence. Vifaa hivyo vya kujiunganisha hapo navyo huitwa jina hilo "gateways." Kwa maana yake gateway ni kifaa au mahali.
3. Gateways (vifaa) zaidi vinaweza kutumika mahali pengine kwa wateja kwa ajili ya usalama wa watumiaji kwenye eneo fulani.
4. Kuweza kuwa mtoa huduma (ISP) yahitaji uwekezaji mkubwa wenye kuhusisha minara ya simu, masafa, nyaya, majenereta nk. Huo ni nje (outdoor) bado wa ndani (indoor) wenye kuhitaji servers, viyoyozi, na vifaa bwerere.
Zungu anapokomaa na kwamba gateway iko nje anajua anachokiongea au hata kuwa ana lenga nini?
U ISP upi anaowaongelea vijana na internet cafe zipi kwenye zama hizi ambazo internet Iko kwenye simu kiganjani?
Watu wa aina ya kina Zungu wanaochomoza kuudanganya umma ni muhimu wakaaswa kuachana na wasiyoyajua.
Ni muhimu wakaelekezwa kujikita kwenye tuliyowategemea kuyafanya. Yaani kuwatetea na kuwawakilisha wananchi dhidi ya serikali.
Kwani kodi zote stahiki, Zungu analipa? Kwani malipo yake yana nasibu uhalisia gani ikilinganishwa na tunayolipwa waajiriwa wengine?
Mnaowakamua tozo na kodi ni wazazi wao hawa:
Kulikoni kutudhania hamnazo?