Kwanini Wizara ya Michezo isiweke idadi ya wanasoka wa kigeni? Maelfu ya vijana wa Kitanzania wanakosa nafasi

Mars 12

JF-Expert Member
Feb 25, 2021
221
349
Nimeamua kuandika habari za mpira wa miguu kwa sababu nyingi lakini za msingi ni kuwa soka ni ajira,biashara,n.k lakini pia ina mipaka yake.mpira wa miguu (Football or soccer) ni biashara kubwa sana sio Kwetu bali duniani kote. Sasa timu zetu kubwa ni mbili tu yaani Yanga na Simba. Hakuna nchini wapenzi wa timu zingine.

Cha ajabu ikiwa mpira wa miguu ni ajira kwa nini wizara husika isiweke kikomo kwa wachezaji ws kigeni hasa kwa timu hizi kubwa ili vijana wetu wapate nafasi na ajira? Leo timu hizi mbili zimejaza wachezaji,makocha kibao wa kigeni tena wanalipwa kwa dola za kimarekani.Hatufaidiki kwa mambo makuu mawili.

La kwanza hawa wachezaji wa kigeni (sijui kama wanalipishwa kodi)wanatuma pesa zao makwao hivyo nchi zao ndizo zinazofaidika.

Pili vijana wetu hawapewi nafasi hivyo wanakosa ajira.Jamani tusijidanganye nchi yetu bado masikini,hawa vijana kupitia wizara husika wangeweza na wanaweza kushika nafasi za wageni na kujipatia rizki. Mpira wa miguu ni biashara kubwa sana ndio maana wajinga ndio waliwao.

Chama cha soka nchini TFF kinaingia mkataba wa kurusha matangazo mubashara kwa miaka 10 na kampuni moja tu eti kwa bilioni 22na ushee kwa mwaka tu, wakati zipo TV nyingi zingeshindanishwa na kila mmoja akapata mgawo wa kurusha mechi mubashara nina uhakika ,wangekusanya mpaka bilioni 600 au 700kwa mkataba wa miaka 3 tu.

Hakuna chama cha soka cha nchi yoyote duniani kinaingia mkataba wa miaka 10 na TV moja tu! Vijana wetu wanaachwa solemba na wizara inaangalia tu.

Tumekuwa mbumbumbu kweli,tunakazania mabeberu tu kumbe wapo miongoni mwetu.Napendekeza mambo mawili la kwanza kila timu ya ligi kuu zikiwemo Yanga na Simba ziwe na wachezaji 3 tu wa kigeni, 2 waruhusiwe kucheza waliobaki watanzania.

Pili mkataba na TV moja kwa miaka 10 uvunjwe na tenda mpya itangazwe na Tv hata 3 zipewe ruhusa kwa makubaliano kurusha matangazo,ukijumlisha unapata bilioni 600 na zaidi ila kwa miaka 3 tu.Tusijaribu bali tutende na nina uhakika wa asilimia mia moja litafanikiwa.

TUAMKE HII AWAMU YA SITA.
 
Azam Tv ndiye kaibuka kidedea kwenye tenda na ndiye aliyeipa hadhi ligi yetu ya ndani.
 
Kweny mkataba wa tv kurusha.. Mbashara hapo nakuunga mkono zingepewa hata tv 3 tofaut mfano azamTv, dstv na startimes nazani hao watu nilio taja wanahitaji kwa sana hio fursa ni ubabaishaji wa tff tu, sjui walihogwa??!!
 
Dah aisee kuna watu mnapenda kulalamika na kutupia lawama wengine maisha yanapowashinda.

Unajukumu na maisha yako sio serikali, baba, mama, mjomba, mkenya, mgeni, jirani au mtu mwingine yeyote.

Jiaminishe kupata ni jitihada na mbinu; kama binadamu mmoja kafanikiwa basi na kwa mwengine inawezekana.

That’s all there’s to life attitude.

Hizi fikra za kulaumu wengine zinawalemaza sana kwenye kukabiliana na uhalisia wa maisha; it’s not easy kwa kila mtu some of us weren’t born with a silver spoon but anything is doable.
 
Back
Top Bottom