Kwa nini waziri aliyepoteza sifa za uwaziri asipoteze ubunge pia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini waziri aliyepoteza sifa za uwaziri asipoteze ubunge pia?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sn2139, May 5, 2012.

 1. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa vile Katiba ya JMT inamtaka Rais kuchagua mawaziri kutokana na kundi la wabunge wa JMT ambao ni wabunge wa kuchaguliwa, kuteuliwa na waliopita bila kupingwa (nadhani viti maalum hawahusiki?). Naamini kuwa watu hao walipata sifa ya kuchaguliwa ama kuteuliwa kuwa wabunge wa JMT kwa sifa za uaminifu. Je mbunge akipewa uwaziri kwa sababu ya sifa za ubunge na kisha kuharibu uaminifu wake katika ofisi ya waziri, kwa nini anaendelea kubaki mbunge?

  Ofisi ya waziri na ofisi ya bunge zote zinatumikia wananchi na uaminifu ni sharti halali kila upande. Mimi nilikuwa ninadhani wakiondolewa uwaziri na ubunge wapewe naqfasi ya kwenda mahakamani kujisafisha badala ya serikali kuwashitaki. Naomba nipewe shule hapo, mimi sheria niliiogopa huko shuleni. Natanguliza bahasha ya shukrani zangu.
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Bado haijathibitishwa Mahakamani kwamba kweli wamekosa huo "uaminifu!"
   
 3. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  great thinking!
   
 4. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,257
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  ...kwa hilo nadhani waliowatuma wana jukumu la kuwaondoa. Aliewapa uwaziri kawatoa, kadhalika waliowapa ubunge wafanye hivyo ili kila mtu afanye kazi yake.
  Sidhani kama ni busara kwa rais kuwanyang'anya wananchi mwakilishi wao.
   
 5. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Babkey

  Rais aliyewapa uwaziri ni mtumishi wa watu walewale waliowapa wabunge ubunge. Hivyo Rais aakikosa imani na wabunge hao, amefanya hivyo kwa niaba ya watu wa JMT. Hivyo inabidi wapokonywe uwaziri na ubunge kama uthibitisho wa kupungukiwa na sifa ya uaminifu ya kutumikia watu.

  Kama hawataridhika na hatua hiyo waende mahakamani, lakini kama wasipokwenda mahakamani watakuwa wamethibitisha uovu wao na serikali itakuwa imeokoa pesa ya kuwafungulia mashtaka.


  Kama Rais atawaacha wabaki bungeni, je bunge halihitaji watunga sheria wenye sifa ya uaminifu? Wajumbe wa kamati za bunge waaminifu? Wabunge ambao azma yao ni kutumikia watu na kuharakisha maendeleo ya watu?


  Mawazo ya layman... lakini ni mawazo.
   
 6. Sn2139

  Sn2139 JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 827
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Buchanan, mnaendeleaje huko ???

  Kama bado hawajathibitishwa kutokuwa waaminifu, kwa nini amewaondoa na kuwahukumu mbele ya raia wote wa JMT? Je, wanaweza kumshitaki Rais wa JMT kwa kuwadhalilisha?
   
 7. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Just a matter of time. Uwaziri alipewa na rais na rais kampora. Ubunge alipewa na wananchi na wananchi watampora
   
Loading...