Kwa nini Watu (Watz)Wanaamini sana BBC?

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,397
8,880
Nimekuwa nikijiuliza sana ni kwanini Watz wanakiamini sana hiki chombo cha Habari cha Nchi ya Uingereza BBC?
Yaani utakuta mtu anabishania kitu ukimuuliza atakwamba BBC wamesema, hata humu JF ukitaka hoja yako iaminiwe na kukubalika basi sema imetoka BBC unganisha na website ya BBC hapo utaaminika!

Lakini kama habari imetoka ITV, TBC au hata Star TV inayohusu nchi yetu hata tusema kuhusu tu Mitaa ya Manzese haitaaminika na utaambiwa ulete ushahidi ukileta wa BBC basi umeaminika, sasa ni kwa nini?

W
akati Dunia nzima inatambua ya kwamba BBC ni chombo cha Propaganda cha Serikali ya Uingereza hata Waingereza wenyewe ambao ndio walipa kodi hawakiamini sasa ni kwa nini sisi tunafikiri kila wanachosema kuhusu sisi ni sawa? kuna sababu yoyoyte ya Msingi?
 
Hiyo ni dalili ya kukosa uzalendo. Ila tabia hiyo imechangiwa na vyombo vyetu vya habari kuandika habari za kupotosha mambo yaliyo wazi. Wenzetu wangalau wanasema ukweli japo wanatangaza habari zetu zile mrengo hasi kama vita na magonjwa, bila kusahau wizi wa kura. Ninaposema uzalendo ninamaanisha hebu angalia TBC wanatangaza habari za chama tawala na wakitangaza habari za upinzani ni propaganda za kuwaharibia wapinzani. Katika mazingira hayo ni bora usikilze bbc ambao watatangaza ukweli hata kama ni habari mbaya kwa taifa letu. Ukitaka tusisikilize habari za nje/bbc tbc itangaze taarifa bila upendeleo kwani inachukua kodi zetu wote na sio za watawala tu. Kwa kumalizia idumu bbc tbc zii.
 
Naamini we mwenyewe mleta Uzi huiamini TBC ndio ujiulize kwa nn hivyo jibu utakuanalo
 
Nimekuwa nikijiuliza sana ni kwanini Watz wanakiamini sana hiki chombo cha Habari cha Nchi ya Uingereza BBC?
Yaani utakuta mtu anabishania kitu ukimuuliza atakwamba BBC wamesema, hata humu JF ukitaka hoja yako iaminiwe na kukubalika basi sema imetoka BBC unganisha na website ya BBC hapo utaaminika!

Lakini kama habari imetoka ITV, TBC au hata Star TV inayohusu nchi yetu hata tusema kuhusu tu Mitaa ya Manzese haitaaminika na utaambiwa ulete ushahidi ukileta wa BBC basi umeaminika, sasa ni kwa nini?

W
akati Dunia nzima inatambua ya kwamba BBC ni chombo cha Propaganda cha Serikali ya Uingereza hata Waingereza wenyewe ambao ndio walipa kodi hawakiamini sasa ni kwa nini sisi tunafikiri kila wanachosema kuhusu sisi ni sawa? kuna sababu yoyoyte ya Msingi?

Wananchi walitakiwa waiamini sana TBC kwa kuwa inalishwa na KODI zao na ilitakiwa iwapatie chakula sahihi lakini kwa hakika Tanzania hatuna Chombo kikachoitwa cha Umma, iwe TBC, RADIO TZ (TBC zote), ni uozo, uozo na ni uozo kweli kweli! Siku ya kwanza nchi itakapopata UHURU na kukamatwa na Wazalendo, jambo la kwanza ni kuifagia TBC na vyombo vyake vyote vinavyotetea wezi, ufidhuli na kuangamiza fikra za watanzania wakati inalishwa na kujishibisha kwa KODI ZA UMMA! Watawala wote na Viongozi wa TBC ni sehemu ya Tatizo l;inalotakiwa kuondolewa ili Watanzania wapate UHURU sahihi.

Kwa sasa wananchi kwa vyombo vya ndani wanaiamini sana ITV na kidogo Mlimani lakini sio wachumia tumbo waTBC...! kWA VYOMBO vya nje, sana sana BBC, VOA na DW kidogo...NA SASA RADIO FRANCE INTER'L ya DSM/FRANCE!
 
Jibu ni simpo. ITV,TBC,Star TV huwa wana copy na kuonesha habari za BBC. Sasa niambie,lini BBC imecopy na kuonesha habari za ITV,TBC au Star TV?
 
Hiyo ni dalili ya kukosa uzalendo. Ila tabia hiyo imechangiwa na vyombo vyetu vya habari kuandika habari za kupotosha mambo yaliyo wazi. Wenzetu wangalau wanasema ukweli japo wanatangaza habari zetu zile mrengo hasi kama vita na magonjwa, bila kusahau wizi wa kura. Ninaposema uzalendo ninamaanisha hebu angalia TBC wanatangaza habari za chama tawala na wakitangaza habari za upinzani ni propaganda za kuwaharibia wapinzani. Katika mazingira hayo ni bora usikilze bbc ambao watatangaza ukweli hata kama ni habari mbaya kwa taifa letu. Ukitaka tusisikilize habari za nje/bbc tbc itangaze taarifa bila upendeleo kwani inachukua kodi zetu wote na sio za watawala tu. Kwa kumalizia idumu bbc tbc zii.

Ni nini kinakufanya uone ya kwamba BBC ndio wanaosema Ukweli, tuseme kuliko labda Star TV ama ITV au TBC?
 
Wananchi walitakiwa waiamini sana TBC kwa kuwa inalishwa na KODI zao na ilitakiwa iwapatie chakula sahihi lakini kwa hakika Tanzania hatuna Chombo kikachoitwa cha Umma, iwe TBC, RADIO TZ (TBC zote), ni uozo, uozo na ni uozo kweli kweli! Siku ya kwanza nchi itakapopata UHURU na kukamatwa na Wazalendo, jambo la kwanza ni kuifagia TBC na vyombo vyake vyote vinavyotetea wezi, ufidhuli na kuangamiza fikra za watanzania wakati inalishwa na kujishibisha kwa KODI ZA UMMA! Watawala wote na Viongozi wa TBC ni sehemu ya Tatizo l;inalotakiwa kuondolewa ili Watanzania wapate UHURU sahihi.

Kwa sasa wananchi kwa vyombo vya ndani wanaiamini sana ITV na kidogo Mlimani lakini sio wachumia tumbo waTBC...! kWA VYOMBO vya nje, sana sana BBC, VOA na DW kidogo...NA SASA RADIO FRANCE INTER'L ya DSM/FRANCE!

Swali langu ndio liko hapo, Je hao unaowaita Wananchi wana uhakika gani kama hawa BBC, radio Ufaransa &Co. ndio wanaosema UKWELI? Yaani kuna nini hapo kinachosema kwamba TBC ni waongo ila BBC ndio wakeli? ndio swali langu hasa!
 
Jibu ni simpo. ITV,TBC,Star TV huwa wana copy na kuonesha habari za BBC. Sasa niambie,lini BBC imecopy na kuonesha habari za ITV,TBC au Star TV?

Kwa hiyo ndio kinachokufanya uone ya kwamba BBC wanasema UKWELI?
 
BBC ilianzishwa kutetea matakwa ya uingereza na kueneza propaganda zao ukiwa unaangalia karibu wanakupitia tena ukichanganya na kuwepo watanzania ambao wanatangazia chombo hicho ndiyo kabisa mimi BBC huangalia kama ninavyoangalia igizo la mzee majuto tu.
 
Swali langu ndio liko hapo, Je hao unaowaita Wananchi wana uhakika gani kama hawa BBC, radio Ufaransa &Co. ndio wanaosema UKWELI? Yaani kuna nini hapo kinachosema kwamba TBC ni waongo ila BBC ndio wakeli? ndio swali langu hasa!

hawa watu huwa hawatangazi hovyo kama vyombo vyetu,wanahakiki mambo,mpaka waandike kitu wamehakikisha,mfano angalia gazeti la uhuru leo imesema ccm imetisha kama tsunami ukawa waangukia pua halafu wameandika front page,hapo hata hajapata matokeo ya nchi nzima halafu uniambie niwaamini kwa pumba zao.
 
uzalendo unatakiwa ila kwa chombo kinachosema na kutangaza ukweli na uhalusia si udhanaishi wa vyombo vya ndani kama TBC na vingine
 
Ni nini kinakufanya uone ya kwamba BBC ndio wanaosema Ukweli, tuseme kuliko labda Star TV ama ITV au TBC?

Sijaitaja Star TV au ITV maana ni vituo huru vinaendeshwa kibiashara, acha kupotezea, nimeitaja tbc kwa kuwa inaendeshwa kwa kodi zetu. Tuna mamlaka na tbc kwani inatumia kodi zetu. Startv na itv zife zisife hatuna cha kupoteza kwani wenye hasara ni wamiliki wake. Ni lini tbc imejiunga hata siku moja kutangaza habari za watanzania wote na kama sio kuegemea zaidi yale yanayowafurahisha watawala? Kama chombo cha umma kilitakiwa kitoe elimu ya kutosha kuhusu maswala nyeti ya nchi yetu, lakini tbc imegeuka ni chombo cha propaganda ya ccm na watawala. Ni bora Hao bbc ambao wanatangaza ukweli hata kama ni aibu kwa nchi yetu. Na kama una uchungu kweli waambie tbc wafanye kazi ya taifa na sio kutangaza kwa upendeleo wakati kodi ni zetu wote. Narudia tena hongereni bbc kwa taarifa za ukweli hata kama mnatuaibisha kama taifa na tbc zii kabisa japo wanatumia kodi zetu na kutoa matangazo kwa upendeleo na propaganda za kizee.
 
Hakuna kama AL JAZEERA na TV/RADIO IMAAAN Yakheee..Chukulia EVERYBODY IS WITH HIS/HER OWN CREDIBLE SOURCE OF INFO.Teh
 
Swali langu ndio liko hapo, Je hao unaowaita Wananchi wana uhakika gani kama hawa BBC, radio Ufaransa &Co. ndio wanaosema UKWELI? Yaani kuna nini hapo kinachosema kwamba TBC ni waongo ila BBC ndio wakeli? ndio swali langu hasa!

Samahani kama nitakosea,nisahihishwe. Unapozungumzia ulinganisho wa vyombo vya habari kuaminika au kutoaminika,ni lazima ujikite kwenye HABARI yenyewe kuambatanisha na facts (zenye kuthibitisha). Mfano : Wakati sakata la Tembo likiripotiwa na BBC,walitoa taarifa yenye vithibitisho vya kimaelezo. Ili chombo cha ndani kukanusha (TBC,IKULU) inapaswa waje the facts against siyo porojo. Ni katika mazingira hayo ndipo media kama BCC zinaaminika sana.

Generaly,vyombo vya umma kama TBC vimekua vya upande mmoja. Inatumika kutetea utawala na kusahau mantiki ya chombo cha umma. Uwepo wa private media umesaidia sana sana.
 
Na BBC ya akina Regina Mziwanda ni ya hovyo huwezi kuilinganisha na ile ya akina Mhando enzi hizo!
 
Back
Top Bottom