Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 6,398
- 8,885
- Thread starter
- #21
Samahani kama nitakosea,nisahihishwe. Unapozungumzia ulinganisho wa vyombo vya habari kuaminika au kutoaminika,ni lazima ujikite kwenye HABARI yenyewe kuambatanisha na facts (zenye kuthibitisha). Mfano : Wakati sakata la Tembo likiripotiwa na BBC,walitoa taarifa yenye vithibitisho vya kimaelezo. Ili chombo cha ndani kukanusha (TBC,IKULU) inapaswa waje the facts against siyo porojo. Ni katika mazingira hayo ndipo media kama BCC zinaaminika sana.
Generaly,vyombo vya umma kama TBC vimekua vya upande mmoja. Inatumika kutetea utawala na kusahau mantiki ya chombo cha umma. Uwepo wa private media umesaidia sana sana.
Kwa hiyo kwa taarifa hiyo ya BBC ndio umeamini kwa 100% kwamba walichokisema ni sahihi?
Yaani umeamini ya kwamba ni kweli Raisi/kiongozi wa Uchina alipakia Meno ya tembo kwenye ndege yake? Ni nini kimekufanya uamini hilo?
Ninaweza pia nikakupa mfano ni BBC hao hao waliotumiwa na Serikali ya Uingereza kusema ya kwamba Sadamu Huseni alikuwa Silaha za Nyuklia ili hali walijua ni Uongo na mpaka UN sasa wamethibitisha haikuwa kweli, sasa uaminifu wao unatoka wapi? kumbuka pia walionyesha vielelezo vyote kwamba Sadamu wana Silaha za Nyuklia!