Kwa nini watu hawajiandikishi kupiga kura | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini watu hawajiandikishi kupiga kura

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kaa la Moto, Oct 29, 2009.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Wakuu, moja ya matatizo makubwa ninayoyaona katika nchi hii ni jinsi ambavyo linapofika suala la kutumia haki zetu kidemokrasia kwa kupiga kura watu hawajiandikishi. Hii imebainika hata sasa kwenye uchaguzi uliopita wa serikali za mitaa. Serikali imekili kwamba watu wengi hawakujiandikisha.

  Maswali yangu kadhaa ni je watu hawajui haki zao katika kupiga kura?

  Je kama watu hawawezi kutilia umuhimu wa chaaguzi kama za serikali za mtaa, je watapata maendeleo waliyokusudia?

  Je ni Tamisemi ambao hawakufanya mipango na kuhamasisha watu mapema ili wajue umuhimu wa kufanya uchaguzi?

  Je kwa hali hii viongozi tulionao ndio kweli wanakubalika kwa wananchi hata uko mitaani au wamechaguliwa na kundi dogo la marafiki na wana familia?

  Hili jambo bado laumiza kichwa changu na najiuliza hivi kweli tutafikia maendeleo ya kweli kama kweli tunadharau mambo ambayo yangechochea maendelo yetu?

  NAPATA MASHAKA NA KIGUGUMIZI KWA HALI HII
   
 2. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Mchukia fisadi hii hali mi mwenyewe inanichisha akili sana. Sababu ninazozifikiria ni:Ujinga (kutofahamu) wa watanzania walio wengi. Watanzania hawana kabisa muda wa kufuatilia siasa na matendo ya wanasiasa wetu. Tunaofuatilia ni wachache sana, wengi walishaaminishwa siasa ni mchezo mchafu unaopaswa kuachwa kwa wanasiasa peke yao waucheze wanavyotaka.Kutoweka kwa uzalendo miongoni mwa watanzania walio wengi. Wengi wetu hawaoni umuhifu wa hata kufahamu mambo yanayotokea katika nchi yao. Matokeo yake ni kutoshoriki katika shughuri za kijumuia tunazopaswa kuzifanya kwa pamoja.Nyama za chama cha mapinduzi kuhakikisha wanaojiandikisha na kupiga kura ni wachache. Sioni kwa nini swala la kujiandikisha ili kupiga kura lifanywe kuwa la misimu karibu na uchaguzi. Na mbaya zaidi taratibu za watu kumchagua kiongozi wanayemtaka hata kama hana chama cha siasa ni mbaya na haziwapi watu uhuru wa kuchagua. Ushahidi wa hili ni uchaguzi wa serikali za mitaa. Watu hawajajitokeza kwa sababu wagombea waliokua wengi ni wa CCM walotangazwa wameshind bila hata kupigiwa kura za ndio au hapana.Pia uzembe wa viongozi wa vyama vya upinzani wa kutohakikisha wanaweka mizizi ya vyama vyao katika ngazi ya kaya. Wana sura nzuri sana ya kitaifa lakini kimtaa wanaudhaifu mkubwa sana. KIPUTIPUTI AONDOLEWE CBE DODOMA KWA MASLAHI YA UMMA.
   
 3. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Mchukia fisadi hii hali mi mwenyewe inanichosha akili sana. Sababu ninazozifikiria ni:Ujinga (kutofahamu) wa watanzania walio wengi. Watanzania hawana kabisa muda wa kufuatilia siasa na matendo ya wanasiasa wetu. Tunaofuatilia ni wachache sana, wengi walishaaminishwa siasa ni mchezo mchafu unaopaswa kuachwa kwa wanasiasa peke yao waucheze wanavyotaka.Kutoweka kwa uzalendo miongoni mwa watanzania walio wengi. Wengi wetu hawaoni umuhifu wa hata kufahamu mambo yanayotokea katika nchi yao. Matokeo yake ni kutoshoriki katika shughuri za kijumuia tunazopaswa kuzifanya kwa pamoja.Nyama za chama cha mapinduzi kuhakikisha wanaojiandikisha na kupiga kura ni wachache. Sioni kwa nini swala la kujiandikisha ili kupiga kura lifanywe kuwa la misimu karibu na uchaguzi. Na mbaya zaidi taratibu za watu kumchagua kiongozi wanayemtaka hata kama hana chama cha siasa ni mbaya na haziwapi watu uhuru wa kuchagua. Ushahidi wa hili ni uchaguzi wa serikali za mitaa. Watu hawajajitokeza kwa sababu wagombea waliokua wengi ni wa CCM walotangazwa wameshind bila hata kupigiwa kura za ndio au hapana.Pia uzembe wa viongozi wa vyama vya upinzani wa kutohakikisha wanaweka mizizi ya vyama vyao katika ngazi ya kaya. Wana sura nzuri sana ya kitaifa lakini kimtaa wanaudhaifu mkubwa sana. KIPUTIPUTI AONDOLEWE CBE DODOMA KWA MASLAHI YA UMMA.
   
 4. K

  Koba JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 494
  Trophy Points: 180
  ...kujiandikisha tuu haitaondoa ubazazi na wizi wa kura unaofanywa na taleban wa CCM
   
 5. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Watu wengi hawakujiandikisha kupiga kura wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa sio kwasababu hawajaelimishwa au hawajui hapana, kwani wengi ninaowafahamu mimi ambao hawakujiandikisha ni watu wasomi na wenye uelewa wa mambo. Sababu kubwa iliyowafanya watu wasijiandikishe ni unafiki wa serikali kutokuwapa wananchi haki yao ya kuchagua watu wanaowataka ; hili linajionesha wazi kwa mizengwe inayofanywa na serikali kupinga kuwepo na independent candidates; hii inadhihilisha wazi jinsi CCM inavyotumia mbinu chafu kutaka kutawala milelel!! CCm ikumbuke tu kuwa inaweza kushinda chaguzi kwa mizengwe lakini utawala wake hautakuwa "LEGITEMATE" na hilo lina athari zake; amani haiwezi kupatikana!!
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  CCM ofcourse wanafikiri wata tawala milele lakini ni ujinga tu one day they will fall and forever.
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Of course sababu ni kuwa wananchi wamekata tamaa ya maisha na wanaona hawana mkombozi tena, maana safu za uongozi zimekuwa ni mtandao wa kujinufaisha na kuwahilikisha wanyonge kwa kuwatia umaskini kwa kila wanachojaribu kukifanya kujikwamua. Fikra za kutokuona mwangaza mwisho wa tunnel hata mimi ninayo, na bahati mbaya wananchi wengi wanayo. Kwa muelekeo wa sasa ni poverty cycle, kuwa umaskini unaleta kukata tamaa, wajanja na wafidhuli wanazidi kuinyonya nchi, rasilimali zinazidi kutoroshwa nje, zile chache zinazobakia zinazidi kuwa centralized mikononi mwa kundi la mafioso na asilimia zilizobaki ndio twagombea sisi akina yakhe.
   
 8. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Elimu ya uraia na umuhimu wa kuchagua viongozi ni muhimu sana kwa jamii.

  nafikiri serikali iimarishe nguvu zake huko ili kufika kwenye demokrasia ya kweli
   
Loading...