Kwa nini watoto wa wazazi ndugu huwa na kasoro za maumbile? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini watoto wa wazazi ndugu huwa na kasoro za maumbile?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JAYJAY, Dec 14, 2011.

 1. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #1
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,495
  Likes Received: 824
  Trophy Points: 280
  ndugu wadau wa JF, nimejiuliza swali hili kutokana na taarifa nilizowahi kuzisikia zamani na taarifa ambazo ni za hivi karibuni. mwaka 2007 nadhani, kuna yule mzee wa Austria ambaye alihukumiwa jela maisha kwa kumbaka binti yake na kumzalisha watoto kadhaa, baadhi ya watoto walikuwa na aina fulani ya ulemavu na mmoja alifariki. jumapili ya desemba 4, 2011, kulikuwa na habari kwenye moja ya gazeti la kiswahili kuhusu mzee wa ujerumani ambaye naye anashitakiwa kwa makosa ya aina hiyo pia, baadhi ya watoto aliomzalisha binti yake wana matatizo ya ulemavu. naomba kuuliza wadau ni kwa nini hii hali inatokea sana kwa wazazi ndugu (baba na binti, kaka na dada,...) kuzaa watoto wenye ulemavu wa viungo au akili?
   
 2. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #2
  Dec 14, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Inbreeding huzidisha uwezekano wa kuongezeka kwa vile vilivyo vibaya katika kizazi husika .

  Genetics hiyo.Ngoja madaktari waje kukuhabarisha zaidi.
   
 3. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #3
  Dec 14, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Mi kuna wa hapa bongo alizaaga na mwanae, dogo akaziliwa bila mdomo, ikabidi madakitari wapasuwe kute'ngeza mdomo wa kufoji.
   
 4. g

  gidytitus JF-Expert Member

  #4
  Dec 14, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  LAANA! Wala hapa 2sijadili.
   
 5. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #5
  Dec 14, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Mkuu hii inatokana kwa vile binadamu tunakuwa tuna chukua genes (alelle) moja moja kutoka kwa wazazi wetu (yani moja kutoka kwa baba na moja kwa mama) kukamilisha aina ya muonekano flani mwilini.

  Sasa kwa mfano ugonjwa wa ngozi wa albino unatokana na alelle aa (yani a moja itoke kwa baba na moja kwa mama). Sasa kupata hizo a sio lazima wazazi wawe albino. Wazazi wanakuwa na Aa ambayo inamaanisha ana ngozi ya kawaida lakini kwa vile ana a ndogo pia anabeba alelle moja ya albino lakini haonekani alibino kwa vile a ndogo aina nguvu zidi ya A kubwa. A kubwa inakuwa inaonekana amabayo ndio ngozi ya kawaida.

  Nii iweke vizuri zaidi kama inachanganya hapo juu:

  aa = albino, Aa= ngozi ya kawaida, AA = ngozi ya kawaida.

  Baba = Aa (ngozi ya kawaida), Mama =Aa ( Ngozi ya kawaida).

  Sasa hapo kwa vile tunachukua herufi moja kwa kila mzazi uwezekano unakuwepo mtoto wa huyo baba na mama kuchukua a ndogo moja kutoka kwa baba na a ndogo moja kutoka kwa mama ambayo inatupa aa= albino. Kwahio mtoto anakuwa mlemavu wa ngozi. Na ndio utakuta watoto wengine wa wazazi hawa hawa wanaweza kuwa sio walemavu wa ngozi kwani wanaweza kuchukua Aa au AA kutoka kwa wazazi hawa hawa.

  Sasa tukirudi kwenye swali lako, kama baba tayari ana Aa na mtoto wake wa kike ana Aa (moja kutoka kw ababa na moja kwa mama) wanapata mtoto, uwezekano unakuwepo wa mtoto huyo kuwa mlemavu wa ngozi kwa vile anaweza kuchukua (a) kutoka kwa mama ( mtoto wa huyo mzee ) na (a) kutoka kwa baba ambaye ni babau yake.

  Hio trend inatumika kwenye aina ya ulemavu na magonjwa kama sickle cell anemia na pia hali ya kawaida.

  Kwahio kama ndugu wawili wanapta mtoto pamoja mara nyingi ni rahisi ulemavu kutokea kwa vile utakuta familia hio ina aina ya ulemavu kwenye genes zao lakini hainokekani kwa vile wamebeba alelle moja yenye nguvu kuliko hile moja ambayo ukiwa nazo mbili inaonesha ulemavu.

  Na sio ndugu tu, bali pia inatokea kwa familia tofauti pia kama wazazi wawili wana beba hizo genes, sema kiwango kikubwa kwa ndugu kwa vile wana genes sawa kutoka kwa wazazi wao.


  I hope nimekusaidia mkuu na kama mtu mwingine ana maelezo mazuri zaidi atakuja. Pole kwa kutofupisha nilitaka uelewe zaidi.
   
Loading...