Kwa nini watoto wa kiume huwaonea wivu mama zao kuliko baba zao?

Kashaijabutege

JF-Expert Member
Oct 20, 2010
2,696
740
Wana jamvi,

Hivi ni kweli watoto wa kiume huona wivu sana wanapowakuta mama zao na wanaume wasio baba zao, kuliko wanavyowakuta baba zao wakiwa na wanawake wasio mama zao? Kama ni kweli, kwa nini?

Je hali ni kinyume kwa watoto wa kike?

Nijuze.
 
Duh, JF kuna mambo aisee! Ila umesema kweli kabisa. Watoto wa kiume huwa wana wivu tena wivu mbaya sana dhidi ya mama zao. Hawapendi mama zao waguswe na wanaume wa nje: inaumiza na kuudhi. Sababu ni kuwa watoto wa kiume kama alivyo baba yao wana hulka ya kumiliki. Kumbe wangependa kuona mama yao anamilkiwa na baba yao tu, na si zaidi.
 
Mkuu hata watoto wa kike ni the same hawapendi kuona mamazao wanamegwa hovyo.
 
Issue nyingine ni mfumo Dume, mtoto wa kiume ana express fillings hata kwa kufanya violence, but mtoto wa kike anaogopa kichapo kutoka kwa mama yake au kwa hiyo njemba inayommega mamaye
 
mie najua mwanaume mmoja since baba yake alivyokuwa na nyumba ndogo,akamchukia kweli baba yake...akawa protective wa mama yake....inategemea mtoto amelipokeaje ,ndoa ya wazazi wake kuvunjika.:teeth:
 
Mahali ulipotoka (tumboni kwa mama) ungependa pawe patakatifu - sio panaingiliwa hovyo hovyo.
 
ni kweli kabisa. watoto wa kiume huanza kuonyesha wivu mkali kwa mama zao tokea wakiwa na umri mdogo sana kabla hawajaanza kuongea. na wakianza kuongea na kujua maneno makali wanaweza mtukana mnyemeleaji na akabaki anajishauwa shauwa. nakumbuka tukiwa wadogo wa umri wa miaka 7 mwenzetu alikuwa anatuhamasisha kumzomea njemba moja ambaye alikuwa mtumishi wa Mungu tumuite shetani. unajua kina mama hawajui umri gani mtoto anaweza elewa wasemayo - tuliweza waelewa wakiteta kuwa yule tuliyekuwa tunamzomea alikuwa na tabia ya kufika pale nyumbani kwa rafiki yetu wakati baba ya rafiki yetu kasafiri. inawezekana hawaoni wivu kwa niaba ya baba zao bali wanachukia ku share penzi la mama na mtu ambaye si mtu waliyemzoea na ambaye wanamkubali ambaye anatokea baba mzazi au wa kambo.
 
Both ways is applicable- hata mtoto wa kike pia hapendi baba yake amwache mamake it is natural? Hizi ni instinct ambazo Mungu kaziweka na zinakubalika. Haiji kuona mama anachukuliwa na jamaa wakati baba hayupo au kinyume chake pia watoto hawapendi.
 
inategemeana na culture...kama culture unayoishi mwanaume anaweza kuoa mke wa pilihuwezi kumchukia baba yako akitoka nje,utachukia kama na pesa za matunzo zimepunguatu nyumbani,basi....kwa culture za kizungu,hata baba akitoka nje anaweza kuchukiwa n watotowachina wana msemo,msichana analelewa na baba,halafu anatunzwa na mumewe,halafu mumewe akifaau akiachwa anakuja kulelewa na kaka,na mwisho atalelewa na mwane wa kiume.....na tusisahau kuwa mwanaume na mwanamke sio sawa,ingawa panatakiwa kuwa na usawa....i personally believe in women's rights kuliko gender equality....je mwanamke anaweza kuolewa na waume wawili??????????is it normal?????????
 
Wivu ni wivu tu nadhani kwangu mimi napata shida mpaka namwonea mtoto wangu mchanga wivu anaponyona na kushika ziwa la mama yake kwa mbwembwe naona kama dogo ana matani yasiyo na mipaka
 
i could be wrong but watoto wa kike hufichiana siri na mama zao......
 
Mkuu hata watoto wa kike ni the same hawapendi kuona mamazao wanamegwa hovyo.

Lakini nasikia wakati mwingine watoto wa kike huficha siri za mama zao. Nahisi wivu wa wavulana unazidi wa wasichana.
 
inategemeana na culture...kama culture unayoishi mwanaume anaweza kuoa mke wa pilihuwezi kumchukia baba yako akitoka nje,utachukia kama na pesa za matunzo zimepunguatu nyumbani,basi....kwa culture za kizungu,hata baba akitoka nje anaweza kuchukiwa n watotowachina wana msemo,msichana analelewa na baba,halafu anatunzwa na mumewe,halafu mumewe akifaau akiachwa anakuja kulelewa na kaka,na mwisho atalelewa na mwane wa kiume.....na tusisahau kuwa mwanaume na mwanamke sio sawa,ingawa panatakiwa kuwa na usawa....i personally believe in women's rights kuliko gender equality....je mwanamke anaweza kuolewa na waume wawili??????????is it normal?????????

Nakubaliana nawe 100% isipokuwa kwenye msisitizo mwekundu. Hapo tunaweza kujadili zaidi.
 
Back
Top Bottom