Kwa nini wateule wa DED watolewe sekta binafsi, wakati kuna watumishi wa umma wengi wazuri?

MIGNON

JF-Expert Member
Nov 23, 2009
4,104
5,102
Niliahidi ya kuwa nakaa pembeni katika kuchangia mada mbalimbali hasa zinazohusu mambo ya siasa.Hii ni kutokana na kuwa mengi yanayoendelea sikubaliani nayo na nilihisi ya kuwa ni bora kupima upepo ukiwa pembeni kuliko kukabiliana nao.
Leo nadiriki kujaribu kuandika kidogo kwani nahisi nimeumia moyo.Nimeumia moyo na teuzi zilizofanyika karibuni hasa ma DC na DED.
Kuna watu ambao wametumia muda wao mwingi katika utumishi kwa uadilifu mkubwa lakini teuzi hizi hawakufikiriwa hata kidogo.
Nashindwa kuelewa inakuwaje mtu atolewe sekta binafsi akabidhiwe majukumu na yule ambaye amekuwa katika utumishi kwa muda mrefu akiachwa.
Hili limeniuma na limenivunja moyo na najua nitajibiwa kwa kejeli lakini waadilifu ndani ya serikali hawakutendewa haki.
 
Back
Top Bottom