Elections 2010 Kwa nini Watanzania wanaoishi nje ya nchi hawapigi kura?

Nameless-

Member
May 21, 2009
47
1
Hivi ni kwa nini Watanzania wanaoishi nje ya nchi hawapati haki yao ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu kama huu uliopita kama zinavyofanya nchi nyingine?
 
Serekali haina hela bado inandaa utaratibu..labda tukisha kufa itaruhusu tupige kura..kwani watakuwa na hela
 
Mimi ninaishi nje ya nchi lakini nilipiga kura mwaka huu. Hata hivyo, nililazimika kwenda kujiandikisha na kuhakiki jina langu kwenye daftari la wapiga kura, halafu nikaenda kupiga kura. It was an expensive venture. Serikali yetu haina utaratibu wa kutuletea vifaa vya kupigia kura huku huku tuliko au kuturuhusu kupiga kura kwa njia ya posta kama wafanyavyo wenzetu. Inawezekana ni kutokana na uwezekano wa kuongezeka kwa uchakachuaji.
 
Hawawezi kupiga kura due to remoteness. Mfumo wa manu ukibadilishwa na kuwa wa digital, wote waliko nje pia watapiga kura zao.
 
sababu kubwa ni katiba ya ccm iliyopitwa na wakati ambayo ina viraka vingi ndani yake mpaka mtu ukiisoma unashindwa kujua original version ni ipi na kipi ni kilaka.

Shime wananchi kusimame tujadili mstakabali wa kubadili katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania
 
Simulipiga hapa jamii forum na mkashinda kwa kishindo. sasa mnataka nini tena? au hamjaridhika?
 
Back
Top Bottom