Kwanini Watanzania hamjiungi na ALIBABA small business website

Sorry, how does this work... can you pls PM me in detail wana Great Thinkers

Inafanya kazi hivi unaweza kutangaza bidhaa yako kule na ukapata wanunuzi na pia unaweza ona bidhaa unayotaka ukaipata kwa kuweka order hasa kama inatoka nje ya nchi pia kupata contact mbali mbali za wafanya biashara world wide
 
nilikuwa nanunua mashine ya photocopy, na nilipa kupitia huko ktk escrow, kilichofanyika Jamaa walileta simu Fake ya kupapasa Iphone, nilisubiri sana nikajua labda hii simu ni zawadi kwa Mteja huku mzigo hukija.... pamoja na kwamba subira yavuta kheri lakini sasa ni mwaka wa pili nasubiria tu kwa kifupi nimetapeliwa.

hiyo despute nilifungua na wao wakaniambia nitume picha ya mzigo uliowasilishwa....... nilifanya hivyo lakini tangia nimewatumia picha hakuna lolote linalo endelea.

ufuatiliaji kaka, ufuatiliaji! uliowatumia picha ni alibaba au waliokuuzia? you can surely reopen the case, ngoja niangalie terms zao, nipm tukomae nao. hapa navoandika nimepotezewa package na kampuni moja ya hapa tanzania inayowakilisha kampuni moja kubwa sana ya courier ya kimataifa, kulikuwa na package zangu mbili zilitakiwa kufikishwa mikoa miwili tofauti, moja imefika, nyingine nayo inaonesha imefika, imepokelewa na imesainiwa na mtu mwenye jina langu wakati mimi hata sikuwa kule hiyo siku, nimewapigia wamekubali kuna upotevu umetokea wanafanya utaratibu wa kunirefund, najua itachukua muda na mizunguko mingi, kwa vile kilichopotea siyo cha bei ghali mimi niko patient kama vulture na ninakomaa nao mpaka warejeshe senti yote, najua wanamfahamu aliyeiba nimeomba jina lake naona wanalindana lakini najua ntampata.
 
alibaba ni wezi tu, ebay ndio ya ukweli

mtoa mda umetumwa na mwizi wa alibaba?
 
www.Alibaba .com .kwenye search engine type biashara yoyote unavyotaka Kama " women clothes or containers or mobile houses .Wafanya biashara kibao watajitikeza hapo register na Anza kuwasiliana .I feel safe and secure sasa Hivi Yaani mpaka kiwandani unaenda unaona bidhaa na kununua Kama ni china India USA .nimeamua kuwashtua mliolala usingizi .

Natalia are u sure? coz nina kamtaji kangu ka 6million nilikuwa nawaza kufuata simu nje nije niuze,nisije nikatapeliwa!
 
vp km ukimuambia akutumie sampo???
Sample siyo guarantee, kwani unaweza pokea sample iko safi ila mzigo wenyewe ukawa na matatizo.Cha muhimu ni lazima uwe na mtu wa kukuchekia bidhaa zako kabla hazijasafirishwa kuja TZ.
 
Kuna njia kubwa mbili tu za kuepuka na matatizo ambayo yanaweza jitokeza pindi unachukua mzigo kutoka China au nchi nyingine yoyote.Ya kwanza safiri wewe mweyenye na ukafunge mzigo we mwenyewe.Njia nyingine, kama huwezi kusafiri,tumia sourcing agent ambae unaweza kumuamini kwa asilimia 100%.

Traders Easy Way-We Supply According to your Budget - Don't buy from Reselling Company, get factory price via Traders Easy Way

Sisi tunalijua ilo tatizo, na kampuni yetu imeanzishwa ili kusaidia watanzania ambao wangependelea kuwa wanachukua mzigo kutoka uchina.

Kama utakuwa interested, wasiliana nasi tutakutumia company profile! Tunasehemu maalum ya kupokelea mizigo ya wateja at Lumumba udoe street, gharama za kutuma kutoka china to dar na ushuru wa TRA unaweza lipia dar siku ya kupokea mzigo wako.China unatuma pesa za manunuzi na service charges zetu.Kama ni order kubwa tunatoa information za kiwanda pia kama mteja atahitaji.

Wasiliana nami! Komba, komba@traderseasyway.com whatsup:+8615996481355
 
Unajua wenzako wanafanyaje sasa hivi, wananunua alibaba wanauza ebay na amazon, akili mukichwa!
ebay yenyewe kuna seller wa kichina kibao lakini wanaogopa kuibia watu sababu ya paypal,

lakini bado haibadili kuwa alibaba ni wezi tu, jamaa wa alibaba angetaka iwini site yake angelazimisha paypal kwa sellers wote!
 
ebay yenyewe kuna seller wa kichina kibao lakini wanaogopa kuibia watu sababu ya paypal,

lakini bado haibadili kuwa alibaba ni wezi tu, jamaa wa alibaba angetaka iwini site yake angelazimisha paypal kwa sellers wote!

Iwini mara ngapi? pesa inayozunguka alibaba ni zaidi ya ebay na amazon, zote kwa pamoja! wewe ulishaibiwa mara ngapi na uliibiwa katika mazingira gani?
 
Na mimi nasubiri paypal waiwezeshe Tanzania kupokea pesa kwa account yao, nataka nianze na hii kitu

utangoja sana baba, sjui kwa nini wameamua kutuchinjia baharini, huenda ni ujinga wa mabenki yetu tu!
 
ebay yenyewe kuna seller wa kichina kibao lakini wanaogopa kuibia watu sababu ya paypal,

lakini bado haibadili kuwa alibaba ni wezi tu, jamaa wa alibaba angetaka iwini site yake angelazimisha paypal kwa sellers wote!

Si kweli mdau...tumefanya business za kufa mtu Alibaba na Ali express....acha woga na kutisha watu...

Escrow ni muuch better kuliko hata PAYPAL...alibaba na Ali express pesa hapewi seller mpaka mzigo ufike na wewe u confirm kuwa ni wenyewe na similar specifications kama ulivyoagiza....

la muhimu uwe makini na modes za payments hasa ali baba na Ali express ukinunua Escrow ndio iwe broker wa payment na si Western union...na ratings za seller unaenunua kwake ana feedback kiasi gani....

WAACHIE WATU FURSA ......................
 
halafu unakuta hajawahi kununua hata mswaki!!

ndugu huwa unajifanya unajua sana na kumbe hujui chochote, na una maneno ya dharau!

kama niliwahi ibiwa alibaba.com ulitaka nikae kimya??

mawazo yangu ya kutoiamini alibaba.com ni lazima uyabebe kama wewe umeamua kuiamini??

huu ni uzi wa pili kuhusu alibaba na nimeona wadau kadhaa kama watano nao wakisema walishawahi ibiwa ndani ya alibaba, hivyo wote ni waongo? hao wote hawajahi nunua hata mswaki ndani ya alibaba??

au umetumwa na mmliki wa ailbaba???
 
utangoja sana baba, sjui kwa nini wameamua kutuchinjia baharini, huenda ni ujinga wa mabenki yetu tu!

Shida ipo na BoT. Kuna siku nilikuwa nawasiliana nao wakasema financial regulations zetu zipo tight kinoma na mbaya zaidi haziendani na za nchi nyingine ndo maana transactions zitakuwa ngumu kufanyika kati ya sisi na nchi nyingine
 
ndugu huwa unajifanya unajua sana na kumbe hujui chochote, na una maneno ya dharau!

kama niliwahi ibiwa alibaba.com ulitaka nikae kimya??

mawazo yangu ya kutoiamini alibaba.com ni lazima uyabebe kama wewe umeamua kuiamini??

huu ni uzi wa pili kuhusu alibaba na nimeona wadau kadhaa kama watano nao wakisema walishawahi ibiwa ndani ya alibaba, hivyo wote ni waongo? hao wote hawajahi nunua hata mswaki ndani ya alibaba??

au umetumwa na mmliki wa ailbaba???

Hata ebay ukiingia hovyo wanakula kichwa. Kila siku nanunua Alibaba na aliexpress na sijawah kuibiwa hata.
 
Back
Top Bottom