Kwa nini watanizia wamesahaulika kwenye msiba wa mandela?

gnsulwa

Senior Member
May 4, 2012
110
195
1.kw.kwa nini melody ya wimbo wa taifa inafanana na melody ya wimbo wa afrika kusini?
2.kwa nini bendera ya taifa ya taifa inafanana na bendera ya afrika kusini?
3.mandela alitokea tanzania mazimbu morogoro baada ya kukutana na nyerere kuweka mikakati ya kupigania haki za waafrika kusini dhidi ya serikali ya ubaguzi wa rangi,na punde aliporejea afrika kusini alikamatwa na kufungwa miaka 27,kwa nini tanzania imesahauliwa kiasi cha kutopewa nafasi ya kutambuliwa kwenye mazishi ya mandela licha ya mandela kusisitiza kuwa "msisahau tanu na ccm" wakati akiwa hai?
 
Azipa

JF-Expert Member
Mar 19, 2012
1,071
1,225
I've been asking myself the same question. The mainstream media in SA only talk about Kenyatta even aired his message of condolences

Mandela came to Tanzania just before he went to jail and also soon after he was released
 
gnsulwa

Senior Member
May 4, 2012
110
195
I've been asking myself the same question. The mainstream media in SA only talk about Kenyatta even aired his message of condolences

Mandela came to Tanzania just before he went to jail and also soon after he was released
can you ask your fellow friends if in S.A as to why Tanzania is totally neglected regardless of her big role that was recognizined even by the late Madiba(the s.a father of nation)himself.
 
msafwa93

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
4,644
2,000
NYMBO ZA TAIFA KUFANANA..

Huenda ukawa umejiuliza swali hili kwa kipindi kirefu lakini hujawahi kupata jibu. Kwanini Tanzania, Afrika Kusini na Zambia zinatumia wimbo wa taifa wenye melody inayofanana?

Melody za wimbo huo ambao kwa Tanzania unaitwa‘Mungu Ibariki Afrika, zimetoka kwenye wimbo uitwao “Nkosi Sikelel’ iAfrika”, neno la lugha ya Xhosa lenye maana hiyo hiyo pia). Wimbo huo ulitungwa mwaka 1897 na Enoch Sontonga, aliyekuwa mwalimu kwenye shule ya misheni ya jijini Johannesburg.

Wimbo huo ulianza kutumika kama wimbo maalum wa hekaheka za ukombozi wa Afrika na baadaye kuanza kutumiwa kama nyimbo za taifa za nchi tano barani Afrika, zikiwemo Zambia, Tanzania, Namibia na Zimbabwe baada ya kupata uhuru.

Zimbabwe na Namibia zimepata nyimbo zingine za taifa. Wimbo huo kwa sasa unatumika Tanzania, Zambia na tangu mwaka 1994 kama sehemu ya wimbo wa taifa wa Afrika Kusini.

Hata hivyo ikumbukwe kuwa Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza kuanza kuutumia wimbo huo kama wimbo wa taifa 1961 pale ilipokuwa Tanganyika na kuendelea nao baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Tafsiri ya mashairi ya awali yaliyokuwa kwa lugha Xhosa kwenda Kiswahili ilifanya na kundi la watu.

Wimbo unaotumiwa na Afrika Kusini hata hivyo ni mchanganyiko wa “Nkosi Sikelel iAfrika” na “The Call of South Africa” (unaojulikana kwa lugha ya Afrikaan kama “Die Stem van Suid Afrika”).

20 April, 1994 ndipo ilipotangazwa kwamba
zote Nkosi Sikelel’ iAfrika na Die Stem ziwe
nyimbo za taifa za Afrika Kusini. Wimbo
uliounganishwa ulianza kufanya kazi October,
1997, baada ya maneno ya Kiingereza yalipoongezwa na wimbo kupangwa upya na Jeanne Rudolph.
 
afwe

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
4,085
2,000
Kumbe ni kweli kuwa tenda wema uende zako usingoje shukurani!
 
Pastor Achachanda

JF-Expert Member
May 4, 2012
3,023
2,000
Ni kwa sababu TANZANIA inaongoza kwa UFISADI na RUSHWA kuliko yoyote duniani. Na pale ni patakatifu hawakanyagi wala rushwa. Akisimama kiongozi wetu lazima ingeanza minong'ono kwamba hii ndo nchi masikini duniani ila ina magari ya kifahari ambayo hata raisi yeyote hatembelei.
 
cha'

JF-Expert Member
Jun 22, 2013
466
195
Mkuu, umenena!
Ni kwa sababu TANZANIA inaongoza kwa UFISADI na RUSHWA kuliko yoyote duniani. Na pale ni patakatifu hawakanyagi wala rushwa. Akisimama kiongozi wetu lazima ingeanza minong'ono kwamba hii ndo nchi masikini duniani ila ina magari ya kifahari ambayo hata raisi yeyote hatembelei.
 
gnsulwa

Senior Member
May 4, 2012
110
195
NYMBO ZA TAIFA KUFANANA..

Huenda ukawa umejiuliza swali hili kwa kipindi kirefu lakini hujawahi kupata jibu. Kwanini Tanzania, Afrika Kusini na Zambia zinatumia wimbo wa taifa wenye melody inayofanana?

Melody za wimbo huo ambao kwa Tanzania unaitwa‘Mungu Ibariki Afrika, zimetoka kwenye wimbo uitwao "Nkosi Sikelel' iAfrika", neno la lugha ya Xhosa lenye maana hiyo hiyo pia). Wimbo huo ulitungwa mwaka 1897 na Enoch Sontonga, aliyekuwa mwalimu kwenye shule ya misheni ya jijini Johannesburg.

Wimbo huo ulianza kutumika kama wimbo maalum wa hekaheka za ukombozi wa Afrika na baadaye kuanza kutumiwa kama nyimbo za taifa za nchi tano barani Afrika, zikiwemo Zambia, Tanzania, Namibia na Zimbabwe baada ya kupata uhuru.

Zimbabwe na Namibia zimepata nyimbo zingine za taifa. Wimbo huo kwa sasa unatumika Tanzania, Zambia na tangu mwaka 1994 kama sehemu ya wimbo wa taifa wa Afrika Kusini.

Hata hivyo ikumbukwe kuwa Tanzania ndio ilikuwa nchi ya kwanza kuanza kuutumia wimbo huo kama wimbo wa taifa 1961 pale ilipokuwa Tanganyika na kuendelea nao baada ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.

Tafsiri ya mashairi ya awali yaliyokuwa kwa lugha Xhosa kwenda Kiswahili ilifanya na kundi la watu.

Wimbo unaotumiwa na Afrika Kusini hata hivyo ni mchanganyiko wa "Nkosi Sikelel iAfrika" na "The Call of South Africa" (unaojulikana kwa lugha ya Afrikaan kama "Die Stem van Suid Afrika").

20 April, 1994 ndipo ilipotangazwa kwamba
zote Nkosi Sikelel' iAfrika na Die Stem ziwe
nyimbo za taifa za Afrika Kusini. Wimbo
uliounganishwa ulianza kufanya kazi October,
1997, baada ya maneno ya Kiingereza yalipoongezwa na wimbo kupangwa upya na Jeanne Rudolph.
asante sana kwa kunielewesha kuhusu wimbo,je kuhusu bendera na stahiki ya tanzania kutambuliwa katika ,mchango wake kusaidia harakati za mandela kupambana na utawala wa kibaguzi
 
Jino Kwajino

Senior Member
Dec 22, 2012
191
0
Kwa sababu Tanzania ya leo haina taswira ya ukombozi wa Afrika wala mwafrika, haifananii na ile iliyokomboa Kusini mwa Afrika. Nashukuru kutotambuliwa kwani imepoteza heshima yake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom