Wale wenzangu na mimi tunaopenda kufanya tafiti nyepesi nyepesi za maisha mtaani utajagundua wasichana wa siku hizi wanapenda zaidi kuwa na wanaume za watu kuliko vijana wenzao ambao ni single. Hii pia nimedhibitishiwa na akina dada kibao ambao kila mmoja alikuwa na sababu zake lakini nyingi ya sababu hizo zilikuwa
- Kwanza Mume wa mtu si msumbufu kama vijana "shalobaro" wengi walioko mtaani ambao hupenda kukuganda sana hata kama huna future naye
- Ni wepesi kuelewa hata kama utamwambia kuwa mimi ninamtu wangu waume hao hawana shida yeyote.
- Pili hawadanganyi. Hii ina maana kuwa anachotaka ni penzi na wewe unachotaka kwake atakupa bila maneno mengi ya uongo
- Wana uzoefu wa kujali (care) hivyo unajisikia huru zaidi. Pia si wapenda malumbano kwani wanajua fika kuwa wana wake zao hivyo wasingependa kujitafutia matatizo.