Kwa nini wasichana hubabaikia wenye magari na fedha? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini wasichana hubabaikia wenye magari na fedha?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jan 2, 2010.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jan 2, 2010
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Inasemekana wasichana wa mijini wanadanganyika zaidi kwa magari. Msichana anakubali kuwa na uhusianao na mwanaume kwa sababu amegundua kwamba ana gari, hata kama anajua kwamba hilo gari sio la huyo mwanaume, lakini hujikuta akikubali kuwa na uhusiano na mwanaume huyo kwa sababu ya gari tu.

  Ndio maana madereva wengi hasa wale wa teksi wanajisifu kwamba wanawake wanawapapatikia sana.

  Je hili lina ukweli kiasi gani?

  Lakini je ni wasichana wote ambao wanawapapatikia madereve au watu wenye magari?
  Nadhani hili ndilo swali gumu sana kwenye suala hili
  Kila kitu kinachohusu uhusianao wa kimapenzi, tunajifunza kutoka kwa wazazi au walezi wetu, labda asilimia 10 tu ndio tunayojifunza nje ya nyumbani.

  Siyo suala la gari peke yake, bali ni suala la karibu kila kitu. Je watoto wetu tunawajengea dhana gani kuhusu kila kitu kwenye maisha?
  Halafu tunawaambia kitu gani kuhusu kupenda?
  Siku zote na tulio wengi tunawaambia watoto wetu uongo mwingi sana, na uongo huo unatokana na sababu nyingi.
  Kwanza nasi tulidanganywa na wazazi wetu. Pili hatujiamini. Tatu hatuna uhakika sisi ni akina nani, na nne tunadhani uongo huo utawasaidia watoto wetu.
  Hebu chunguza kwa makini utagundua kwamba, wasichana wanaobabaikia magari ni wale ambao wamelelewa kwenye malezi ya uongo mtupu.

  Unaweza kudhani wale waliotoka kwenye familia masikini ndiyo ambao wanababaikia magari, hapana.
  Msichana anaweza kutoka kwenye familia masikini na asibabaikie utajiri wala magari, wako wengi wa aina hiyo.
  Kama nyumbani wazazi wanawasifu wenye magari, wanaonesha kwamba ukiwa na gari ndio unakuwa na maana, kwamba ndio kiwango cha juu cha mafanikio, unatarajia kitu gani kutoka kwa watoto?
  Kuna wakati wazazi wanasema , “ameshafika mbali sio mwenzio, yule ana akili sana. Ana magari mawili na nyumba tatu.

  Wakati mwingine inatosha mara moja tu, jambo kusemwa na mzazi, na mtoto kuamini kwamba mwenye gari au magari na nyumba ndiye aliyekamilika, ndiye mwenye akili..

  Kumbuka mtoto anaingiza maarifa akilini mwake kutoka kwa watu anaowaamini anaokutana nao maishani. Kwenye suala la uhusianao wazazi ndio wanaoaminika zaidi.

  Kwa sababu ya umasikini wetu, tulio wengi na uhaba wa malengo makubwa kuliko sisi wenyewe, gari na nyumba ndio malengo ya juu kabisa ya binadamu kuyapata.

  Mtoto anakuwa na akili ya aina hiyo, kigezo chake kuhusiana na mtu kitakuwa ni gari, nyumba au mali kwa ujumla.
  Kwake binadamu mwenye maana na anayefaa ni yule anayemudu kumiliki vitu hivyo.

  Hii sio kwa wasichana peke yake bali hata wanaume. Kama mtoto wa kiume alioneshwa kuwa thamani ya mtu inatoka kwenye gari, nyumba na mali, basi naye atakuwa anababaikia vitu hivyo.

  Linapokuja swala la uhusianao, atajitahidi kumuonesha msichana kwamba anavyo vitu hivyo au anao uwezo wa kuvimiliki. Anafanya hivyo kwa sababu aliambiwa thamani yake inakuwepo pale anapokuwa na vitu hivyo.

  Wazazi wengi wameegemeza thamani zao kwenye vitu badala ya wao wenyewe. Bila ya hiyari yao wanawafundisha watoto wao kujali na kuthamini vitu badala ya utu wao.
  Kwa kadiri mfumo wa maisha wa mitaji ulivyokuwa ukiendelea, binadamu alijitoa thamani na kuiweka kwenye vitu, hasa mali.

  Kwa bahati mbaya wale watoto wa wazazi ambao wana maisha ya kati ndio ambao wanasumbuliwa na mali.

  Kwa nini?

  Kwa sababu wazazi wao hawajui kama wako juu au chini kimapato.

  Katika kujitafuta hutoa kauli zenye kuonesha kwamba maisha ni mali, basi.

  Wazazi walio na kipato cha chini nao wanaweza kuwaathiri vibaya watoto wao, kwa kuzungumza na kutenda katika njia ambayo watoto wataamini kwamba umasikini huondoa kabisa thamani ya mtu.Wale walio juu kabisa wanaweza wasifikirie kwamba gari au nyumba ni mambo ya maana sana, hata kama wamefundishwa kuhusu mali. Wao watafikiria mali kwa mkabala mkubwa zaidi.

  Labda watafikiria kuhusu ndege au kutembelea boti ya kifahari na mengine, lakini wote watakuwa na udhaifu ule ule wa kuamini kwamba mali ni kubwa kuliko thamani ya binadamu.
  Mali ambayo unaitengeneza na kuitafuta mwenyewe halafu iwe kubwa kuliko wewe! Hii ni ajabu kabisa.

  Wazazi ambao wanachukulia mali kama kitu cha kawaida sana, ambacho uwe nacho au usiwe nacho, maana ya maisha haibadiliki, na thamani yako haiondoki kamwe, hawa ndio watoto wao watakuwa na maisha bora.
   
 2. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2010
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280

  Mkuu, hili swala limeenda mbali zaidi mpaka kwa wanafunzi.
  Utakuta mwanafunzi yuko kituoni saa 3 ya usiku, ukadhani makonda walikua wanamkatalia kupanda daladala, kumbe sio mkuu.
  Huwa wanasubiri daladala maalumu ambazo zina maboy-friend zao mkuu, na hupanda free of charge.

  Daladala inaweza ikawa haina abiria kabisa, lakini binti hapandi na pengine keshapewa signal/amebipiwa na konda amsubiri.

  Hawa mabinti wamejirahisisha sana kwa makonda, na kwa taarifa yako mkuu, MAKONDA NDO WANAOONGOZA KWA KUTOA BIKIRA ZA MABINTI ZETU.Bado naendelea na utafiti mkuu.
   
 3. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  kwani ulikua hujui hilo mkuu
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Jan 2, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,606
  Likes Received: 3,904
  Trophy Points: 280
  mzee naona unataka kugombana na asili!
   
 5. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Kama unamtaka demu wewe azima tu gari ya mshkaji weka wese mtokee demu au km anafanya kazi mpitie asubuhi daily, yaani utakula mzigo kiulainiiii. Kuna kisa kimetokea job dada mmoja hajaolewa yupo kwenye late thirties ana gari, kampata jamaa mmoja pale kazini bd bachelor, yule dada anamwachia yule jamaa gari, kilichoendelea ni kwamba jamaa sasa kwa kutumia hiyo gari anawamega akina dada pale job si mchezo takriban sita, huyo wa mwisho ndo alizua balaa alizoea kupewa lifti daily na jamaa akadanganya ni gari yake. Siku ya siku mwenye gari wako na huyo jamaa wanatoka job yule dada aliyekuwa akimegwa bila kujua kuwa jamaa gari si lake alipowaona si akamind akajitia kushoboka, mwenye gari nusura amkate mtu makonde, watu wakasuruhisha lkn jamaa tayari keshatia damage
   
 6. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280

  Story tamu kweli Chimu! LOL
   
 7. M

  Mende dume Member

  #7
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 73
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanajamii, hili si suala la asili. fedha na vitu vimebadili sura ya jamii. Japo mtoa hoja anawaona watoto kike kuwa ni wanaendekeza, nadhani huu ni mtazamo wa kijuujuu zaidi. Hali ni mbaya zaidi kwa watoto wa kiume. Mtoto wa kike atamkimbilia mwenye gari ili nature iiendelee, sasa wa kiume atatoa nini? anageuzwa! siku hizi sikiliza hata nyimbo zetu za ubongo wa flava vijana wanlenga zali la mentali, mara mtoto wa kigogo, mara mtoto wa bosi, geti kali mkopo wa nguvu!

  hadithi zetu za zamani, zenye last part, --- lived happy there after! zilikuwa na mlengo wa mtu kafanya kazi kwa bidiii mpaka akafanikiwa, au binti alikuw na tabia njema akachaguliwa na mtoto wa mfalme akawa ndo malkia etc etc, siku hizi no such a thing, utasikia alikuwa changu akachukuliwa na mzungu ndo kamjengea, mara Mc Lymb alimpenda akampa rav 4 nyekundu, mtoto wa kiume akachukuliwa na mwarabu ndo kamfungulia show room. what is this?

  tunapiga vita ufisadi in public, huku unaangalia kama mtoto wa karamagi, lowasa, au nani kama yupo reachable hata leoleo upo tayari kumvisha pete- kisa zari la mentari. what is this?

  ni jamii nzima tumeoza, hatutaki kazi ila maramoja unataka nyumba masaki, na rav 4, how come?

  Can u imagine, baada ya uchambuzi dhidi ya mafisadi sisi wenyewe tutatoka na kumpigia kura muungwana arudi atutese tena kwa miaka 5! kisa katakrima kidogo tu ahadi kuwa utafikiriwa!
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  mende dume umesema vema sana hapo na nimekugongea senks!!!

  jamani binafsi naona suala zima la kumpapatikia mwanaume kisa gari ni wazi kuwa you are in love with his car/ house/ biashara and the list goes on!!!!

  mapenzi yanakuwa driven ma material things si mapenzi ya dhati na mara nyingi hayadumu!! upendo wa kweli hutoka ndani ya moyo wa mtu haya mengine yanakuja tu!!!

  sasa na weew unapoazima gari ili ukatongozeee unategemea nini kama si kupendwa kwa kudanganywa!!! after all we pia ni muongo!!! so endeleeni kudanganyana.
   
 9. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tufanye kazi, waswahili wanasema "mtegemea cha ndugu hufa masikini". Tumeacha itikadi ya ujamaa na kujitegemea na tumeanza mambo ya kujipendekeza kwa matajiri na kuwaabudu mafisadi, kumbe sasa ufisadi ni zaidi ya utamaduni na kila mtu ana sehemu yake katika ufisadi huu. Mkuu hapo juu amesema jamaa kaazima gari ya demu kaenda kutongozea huo nao ni ufisadi, tena mbaya zaidi huu ni ufisadi wa ki maadili ambao ni mbaya kuliko wa ki uchumi.

  Tujiangalie sana kama wana jamii wapi tuendako?
   
 10. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2010
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  .........Hivi kuna mtu anapenda umasikini?
  BTW siyo kila msichana anababaikia magari na fedha, na wale wasichana ambao wana magari na fedha zao tayari utawaweka kundi gani?Naona hapa umegeneralize wasichana wote kumbe kuna wengine wala hawababaishwi na magari wala fedha toka kwa mwanaume.
   
 11. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wale wana tusenti tu na vijigari vya bei poa wakimuona mtu mwenye senti zake halafu anasukuma kitu kizito kama Mercedez Benz 420 Mettallic in color basi huwa wanaweweseka.
   
 12. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2010
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  naona ujengele amesema yote...wasichana wenye magari ndo wanaweweseka zaidi wakimuona mwenye gari kali kuliko lake....kama ana Vitz/nissan march/starlet/tcossa/corolla ltd na zifananazo na hizo basi akimuona mwenye kuanzia rav4 baaasi anachizika.....na kama alinunuliwa hicho kibeetle basi atafanya bidii ampate wa kumnunulia gari kali.....ndo maana ck hizi wanawake wanasukuma magari makubwa utadhani ni madereva wa SU fulani....binti yuko single na anasukuma L/cruiser V8 mjini jamani!!! mwanamke akiwa mbunge anaridhika kama mumewe ni waziri, kama yeye ni waziri anataka angekuwa firstlady....ukiona yuko na mtu wa chini yake ujue hana amani au hajaridhika bado...most of them jamani sio woote...nashawishika kuamini wanawake wanawafanya wanaume zao/marafiki zao wa kiume wawe mafis Adi.
  atil kabati ya mbekho??n.k
   
 13. Sugar wa Ukweli

  Sugar wa Ukweli JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 373
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani wewe acha tu!!!,umasikini huu utatumaliza!!!,tujitahidini tubadilike tukubaliane na hali tulizonazo tusitamani vitu ambavyo viko nje ya uwezo wetu!!!
   
 14. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Nimependa sana mchango wako. Natamani wangekuwepo wengi wenye msimamo kama wako.
   
 15. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,721
  Likes Received: 242
  Trophy Points: 160
  nimeipenda hii topic mkuu...thanks

  kwa uzito na upana wa mjadala nadhani heading imeegemea zaidi kwa wanawake ingawaje muelekeo ni kukosoa tabia yetu ya kuwathamini watu kwa kuangalia wanachomiliki katika mali.

  pengine kichwa cha mada kingekuwa kwa nini kizazi cha leo kinathamini zaidi pesa na mali tusingeonekana tumewadhalilisha wanawake. lakini hata hivyo nikupongeze mkuu, heading uliyotumia inavuta zadi hadhira kuliko pendekezo langu.
   
 16. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  wanawake wanafikiria kitu kimoja tu wakati wanamkubalia mtu amvue chupi...!WANAFIKIRIA SECURITY!..akijihakikishia kwamba akiwa na wewe atakuwa secured basi mzee unabeba kifaa huyoooooo!

  ...kuna kitu kimoja tu wao huwa hawaangalii!....HAWATAKI KUDADISI SAAANA

  (natania tu jamani/.....:D
   
 17. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  utani wa ngumi huu......
   
 18. bht

  bht JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  utani gani huu sasa na we mpwa wa ukweli!!
   
 19. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  This should be the hi! time for Change
   
 20. carmel

  carmel JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 2,841
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Jamani mbona mara nyingi hapa habari ni wanawake hili wanawake lile, why? I think we are being unfair to women! what about men? wangapi ambao wako tayari kuwekwa kinyumba na wamama wenye pesa ambao wanawazidi umri mara tano kwa ajili ya pesa, magari nk? si kweli kwamba wanawake wote wanapenda wanaume wenye magari, eti hicho ndo kigezo, inategemea akili ya mtu na malezi paamoja na defition yake ya mapenzi. Halafu si kweli kwamba mdada wa kawaida lets say graduate tu mwenye kazi ya kawaida ya laki sita hadi saba kwa mwezi anashindwa kununua gari ya kawaida ya million sita, kama ishu ni usafiri. Lakini inapokuja ni model gani ya gari, how expensive it is na mengine kama hayo, tutakuwa tunaongelea zaidi personal traits za tamaa ambayo ndo hupelekea kutaka vitu vya juu zaidi bila kuangalia uwezo. Lazima tukubali kuwa wanawake wengi wamebadilika na wanafight kivyao kupata magari mazuri na nyumba nzuri kwa pesa zao wenyewe, after all, wanaume wenyewe wa kuhonga wako wako wapi kama si mafisadi?
   
Loading...