Kwa nini wanawake husalitiwa na mashoga zao kirahisi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini wanawake husalitiwa na mashoga zao kirahisi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Nov 15, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa nikijiuliza ni kwa nini wanawake husalitiwa zaidi na mashoga zao kwenye uhusiano kuliko ilivyo kwa wanaume? Naamini kila mmoja ni shahidi kwa kutendwa, kusikia au kuona wanawake walionyangÂ’anywa waume au wapenzi na mashoga zao. Je tatizo ni nini? Je ni tamaa za wanaume au wanawake hao walikuwa na kasoro ambazo zilikuwa hazirekebishiki na wanaume hao walikuwa wanasubiri tu atokee mwenye sifa wazitakazo waoe?
   
 2. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Tatizo huanzia kwa wanawake wenyewe. Mwanamke akiwa na mpenzi wake hupenda sana kuanika kwa mashoga zake sifa za zote huyo mwandani wake kama vile mapigo yake kwenye 6x6, huduma anazompa bibie na misifa kedekede. Shoga mara nyingi huvutiwa na hizi sifa na huduma na kutamani naye azipate. Hivyo kinachofuata ni shoga kufanya kila jitihada ili ajilengeshe aweze kumpata huyu mpenzi wa shoga yake. Bahati mbaya wanaume ni wadhaifu sana, wakichokozwa kidogo tu wanaitikia. Ushauri wa bure kwa wanawake; jaribu kuwa msiri sana kuhusiana na mambo yako ya kimapenzi vinginevyo utalizwa na mashoga zako tu.
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Mimi sijawahi kushuhudia hilo bado
   
 4. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mashoga wengine roho zao hazija kinai, wengine hata kama hujawaelezea raha unazo pewa akimuona mumeo mnaelewana mnapenda baada ya kukuliza siri ya maelewano yenu nini anataka achukue yeye akijua atakua na raha kama ulizo nazo wewe wakati hajui bwana yule mmeanzia wapi,
  wengine wanavutiwa na unavyomuelezea kama mume wangu ananipa hiki au kaninunulia kile anaona akijilengeshe yeye ndio atakutoa wewe,kwa ufupi ni ufisadi na choyo.......
   
 5. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  nadhani kuna sababu nyingi, baadhi ni:-
  1. tamaa shoga, haswa pale anaposimuliwa mambo ya yule mwanaume lets say unamwambia shoga yako "bwana wangu mjuzi ananipeleka ananifanya hivi au vile" au pale shosti anapoona bwana wa mwenzie anamjali anampa hiki au kile simu mara kwa mara; anadhani akiingia na yeye atapata, au kama mwanaume ana fedha shosti anaweza kumtokea akijua atapata fedha nk

  2. tabia mbaya ya mwanaume; kuna mijanaume mizinzi inatongoza hadi ndugu zako wa damu sembuse rafiki. na ukikuta na shosti ana tabia mbaya ndo inakua balaa

  3. baadhi ya mashosti wanafanya hivyo kukomoa "tuone anachoringia kwa huyo mwanaume wake" au " naweza kumchukua huyo mwanaume wakati wowote"

  4. wengine labda wana matatizo kisaikolojia jamani, kuna mdada yeye ni kujirahisi kwa waume wa wenzie, akimpata anafanya kama competition fulani, akiweza kupata attention ya mume wa mwenzie ndo anapata faraja. Sijui huu ni ugonjwa au vipi, ilifikia kipindi wanawake walipomshtukia wakawa wanamkwepa

  wanawake wanatakiwa kuwa makini sana na hawa mashosti, usiache rafiki kumzoea mumeo/boyfriend. lazima kuwe na limit ya uhusianao kati ya rafiki na mume/boyfriend. haiwezekani kila rafiki akawa na namba ya simu ya mumeo, na ampigie anavyojisikia. akitaka kitu kwako badala ya kukupigia wewe yeye anampigia mumeo. Hili pia linaenda hata kwa wanaume, asimzoee sana shemeji yake.

  pia mwanaume makini aliyependa kwa dhati, anayemuheshimu mwenza wake hawezi kutembea na shosti wa bibi yake, kama kutoka atacheza mbali
   
 6. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,674
  Trophy Points: 280
  Kwa uzoefu nilioupata kwa walioolewa na kuoa,hilo jambo limegawanyika kwenye makundi mawili,mosi,Kuna wakati wanaume wanaongozwa na tamaa,hawa haijalishi mke anamjali ama la yeye tamaa ni big deal.Pili,Wapo ambao tatizo ni wanawake,hawajali,wachafu n.k,hayo na mengineyo humkimbiza mume,tena atakapo mwona rafiki yake mkewe anafit!!
   
 7. WALIMWEUSI

  WALIMWEUSI JF-Expert Member

  #7
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 2,058
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  1. Tamaa na wivu kwa mwanamke mwenziwe na hii sio kutokana na kuanika mambo yake kwa shoga, sometimes unaweza kusiwe unamsiimulia au kumpa habari za kwako ila yeye kwa kuona tu akatamani yeye awe na mumeo.
  2. Kukosa maadili ni sababu kubwa sana, kama una maadili wewe shoga utamuheshimu mume wa refiki yako coz ni shemeji yako huyo!All ni all, mwaname mwenye hofu ya Mungu kamwe hawezi kumsaliti rafiki yake kwa mumewe bali na yeye atatafuta mume wake ambae ataapewa na Mungu. Ukiona shoga kamchukua Mume wa rafiki yake basi ujue huyo ni gumegume aliyekubuhu na hana hata mshipa wa aibu!
   
 8. feis buku

  feis buku JF-Expert Member

  #8
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 29, 2011
  Messages: 2,371
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake!! Tusipende kuwaamini marafiki zetu especialy hawa mashoga !!
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Na wanaume nao kwa nini wanaangukia kwenye mitego ya shoga wa wake zao. Hapo naona wote wana matatizo, wanawake na wanaume pia.
   
 10. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #10
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  hivi hii dunia ya leo bado kuna watu bado wanaendekeza mambo ya ushoga...................
   
 11. s

  sawabho JF-Expert Member

  #11
  Nov 15, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Tabia ya wanawake kumwamini shoga yake mapema na kumsimulia mambo yake ya ndani yawe ya furaha au raha ambapo shoga yake huamua kufanya majaribio ili aone kama ni kweli. Wakati mwingine Mwanamke anaposimulia shoga yake kuhusu shida anazopata ndani ya familia yake, huyo shoaga yake anaweza hiyo nafasi ataipataje.
   
 12. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #12
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  umeona eeh! Hii inahusu pande zote mbili.
   
 13. M

  MyTz JF-Expert Member

  #13
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sidhani kama kuna ubaya ukiwa na shoga...
  nafikiri cha kufanya ni kuweka ukuta unaotenganisha ndoa na ushoga...
   
 14. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #14
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,672
  Likes Received: 941
  Trophy Points: 280
  Nashukuru Mungu sijawahi kutendwa wala sitegemei. Hii ni kwa sababu sijawahi kuwa na shoga zaidi ya marafiki, na ukweli ni kwamba sijawahi kuwapa access ya kujua undani wa mahusiano yangu na mume wangu au hata boyfriend wangu enzi hizo. Mimi mahusiano yangu na mpenzi wangu ni personal hata akiniudhi siwezi kumwambia friend zaidi ya Mungu wangu...
   
 15. Chauro

  Chauro JF-Expert Member

  #15
  Nov 15, 2011
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 2,969
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mimi hiyo biashara sina nilishaifutia mbali siku nyingi maana unaweza hesabu hasara kuliko faida.

   
 16. M

  MyTz JF-Expert Member

  #16
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 334
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  yashawahi kukuta nini?
   
 17. Cantalisia

  Cantalisia JF-Expert Member

  #17
  Nov 15, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 5,229
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Haijalishi nimemsimulia huyo shoga habari zangu au au ni umalaya wake tu unamsumbua au tamaa zake za kijinga,huyo mwanaume akitegwa na kutoka na huyo shoga au ndugu yangu naye hafai ni malaya tu.
  Mwanaume yoyote mwenye busara kwanza hatotoa mwanya wa kuzoewa hovyo na mwanamke yoyote asiye ndugu yake yeye,na kamwe huwa hategeki na mwanamke yoyote isipokuwa mkewe/gf wake.
  Binafsi hapa mwenye tatizo ni huyo mwanaume,kwann ategwe na kukubali kutegeka?
   
 18. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #18
  Nov 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,103
  Likes Received: 6,567
  Trophy Points: 280
  Mkuu umeamkaje na maumivu ya mkono leo.

  hata wanaume husalitiwa na marafiki zao, na usaliti wao ndio mbaya zaidi ya ule wa wanawake,
  ni kuwa mara zote inakuwa ni siri zaidi kuliko upande wa wanawake,
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Nov 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Niko hapa Regancy Hospital, nasubiri kumuona Doctor, kwa ajili ya matibabu......................Lakini naendelea vizuri.
   
 20. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #20
  Nov 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  Mhhhhhhhhhhh!
   
Loading...