Kwa nini wanaume wengi hudanganya kwenye hili………………! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini wanaume wengi hudanganya kwenye hili………………!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, May 10, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Ni mara ngapi umeshawahi kusikia malalamiko au hata kuvunjika kwa ndoa kutokana na ugunduzi wa wanawake kwamba waume zao walishazaa nje bila kuwajulisha wakati wakioana? Jibu bila shaka litakuwa ni mara nyingi.

  Ni mara nyingi kwa sababu kwa kiasi kikubwa wanaume huwa hawapendi kuwa wakweli kuhusu maisha yao ya nyuma, hasa yanayohusiana na uhusiano na wanawake na hata watoto (kama wapo).

  Mara nyingi huamua kusema kuhusu watoto wao wa nje baada ya ndoa, wakiamini kwamba katika kipindi hicho wake zao watakuwa hawana njia isipokuwa kuwakubali watoto hao.

  Lakini ni afadhali wangekuwa wanasema ukweli wote ili kuepuka dhahama na wenzi wao...........!
   
 2. Asabaya

  Asabaya JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 1,317
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Nakubalina na wewe 100% ni bora ujue ukweli mapema kuliko unaletewa mtoto keshafika miaka 10 unauliza hiki kituko kinatoka wapi unapewa hadith kibao mpaka kichwa kina uma.
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  May 10, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kwasababu wanajua wanawake wengi 'wanafungwa' na ndoa. Kuwaambia kabla wakati bado wanaweza kukimbia wanaogopa (wanaona ni risk ambayo sio ya lazima) hivyo wanasubiria wawaweke vifungoni kwanza ili waishie kulalamika/kununa na kuitisha vikao tu na sio kuondoka. Kwa kifupi HAWAJIAMINI kwa hao wenzi wao.
   
 4. fazaa

  fazaa JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2012
  Joined: May 20, 2009
  Messages: 2,986
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Wanawake wanapenda story, yani kama huwaelezi story zako basi wanakuwa kama wamekosa raha...cha kushangaza pale wewe ukitaka story zao utajuta kuliza.
   
 5. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #5
  May 10, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  sasa kwa wale ambao hawajui kua wana watoto nje ya ndoa mpaka baada ya kuoa inakuaje?? kuna mi wanawake mingine inapata mimba za wanaume hawasemi huko mbeleni akiona mwanaume mambo yamekaa fresh kifedha na katulia ndani ya ndoa ndio yale siku unasikia hodi mlangoni kaja na kimwana sa hapo sijui inakuaje
   
 6. wahida

  wahida JF-Expert Member

  #6
  May 10, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ya iyo n kweli kuna watu mpaka apo unaongea basi wanaficha wake zao ktk hilo au wachumba zao
   
 7. Brine

  Brine JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2012
  Joined: Oct 28, 2011
  Messages: 376
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ni kuto jiamini ila kwa anaye jiamini anasema kabla maana hiyo imetokea kabla hamjajuana na huyo mwanamke unayetaka kumuowa sasa tatizo liko wapi au ugumu wa kumwambia ukweli?
   
 8. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Nani kakudanganya kwamba wanawake wanapenda kuambiwa ukweli?, shauri yako. Tena kwa taarifa yako wanawake ni waongo kuliko hata wanaume! Kama una mke, kila siku lazima udanganywe kitu angalau kimoja!

  Mungu alisema ishi nao kwa akili, unajua ni kwa nini? HAWAELEWEKI, ni WAONGO, kila mwanaume analalamika kama sio hadharani basi kimoyo moyo. ila nawapenda sana!

  take it as a joke!
   
 9. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mwanamke ukimwambia ukweli humpati?
  Mnaanza kwa kudanganyana, mambo yakikaa sawa ndio unamweleza timu ya mpira uliyonayo
  .
   
 10. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  watoto wana shida gani
  leta hata mia......
   
 11. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  hata unapomtongoza ukileta story za ukweli unakataliwa,kakija kajamaa kampige sound za uongo anakubali. Sijui tuwaelewe kwa lipi?
   
 12. charminglady

  charminglady JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2012
  Joined: Apr 16, 2012
  Messages: 17,858
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  Kama alizaa kabla ya ndoa sawa ila kama ataleta mtoto baada ya ndoa hapo patachimbika mbona! Ukweli humweka mtu free!
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  true true, ni vyema kumueleza mwenzako mapema ili akubali kusuka au kunyoa
   
 14. J

  JOJEETA Senior Member

  #14
  May 10, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huwa najiuliza y huwa hawasemi na wakati imetokea b4 marriage,mfano alizaa mwaka 1985 alipokua 4m5,akaja kuoa 98,mke anakuja kujua kua mumewe ana mtoto na anamuhudumia mwaka 2008....cio fair ni bora kumtel mapema ili kieleweke
   
 15. papag

  papag JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 688
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  mimi nilipa ukweli..na hakusepa yupo na maisha yanaendelea
   
 16. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2012
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kinachouma ni kuwa analeta mtoto ambaye amepata wakat amenioa hapo ndo kinaponuka kizaazaa ila kama akiniambia ana mtoto kabla ya ndoa yangu na yeye mi sitakuwa na shida.
   
 17. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ai na wewe umeng'ang'ania "kifungo" lol.........

  Sio sheria ya uanaume hiyo ni uoga tu, mi suala la Malaika wangu namwambia mtu siku ya kwanza tu wakati namtongoza akiwa ananikataa anikatae vizuri!!
   
 18. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Heri wewe unakuwa umeepusha mengi!!
   
 19. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Pole sana Michael! Wewe unaangalia tu kumpata mwanamke, wakati huo huangalii wanao watajalelewaje!
   
 20. S

  STEGRA Member

  #20
  Feb 5, 2013
  Joined: Aug 20, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaelekea wewe ni mmojawapo kati ya wale walioleta mtoto wa kuokota huko nje akiwa katika ndoa ya ndoa yake maana jinsi ulivyotetea. pia uongo wao wa vitu vidogovidogo sio sababu ya wewe kutafuta vifurushi vya wototo na pengine hata uwezo wa kuwatunza huna matokeo yake unmrundikia mkeo mizigo. Wanaume acheni hizo tabia
   
Loading...