MwanaFalsafa1
JF-Expert Member
- Feb 26, 2008
- 5,565
- 836
Kwanza napenda nianze kwa kusema sina neno na kuwa na wanasiasa ambao wamebobea kwenye taaluma zao. Natambua kwamba mtu hasomei siasa kwa hiyo mwanasiasa yoyote kazima atakuwa na taaluma fulani nje ya siasa. Pia natambua madhara ya kuwa na viongozi wengi ambao hawana kisomo kikubwa. Mwisho niseme pia kwamba natambua kwamba siyo wanasiasa wote "wasomi" wana visome halali au vya kueleweka.
Tatizo langu ni kwamba inaelekea Tanzania kuna wimbi la wanataaluma ambao wanaona ni heri kuwa wanasiasa kuliko kufanya kazi walizo somea. Ingekuwa wachache ningeelewa ila sasa inabidi nijiulize kwa nini wengi hukimbilia siasa? Kwenye Bunge letu na hata serikalini kumejaa "madokta" tena wengine wenye specializations lakini bado ukiangalia hospitali zetu tunaambiwa kuna upungufu wa wataalamu.
Kuna watu kama Prof. Lipumba. Mseme utakavyo huyu bwana lakini ni jambo lililo wazi kwamba ni mchumi aliebobea hata kipindi fulani kuwa mshauri wa raisi. Prof. Lipumba kila leo ana gombea uraisi lakini huishia kapa. Kwa nini asifanye kazi inayo husisha taaluma yake baada ya kung'ang'ania siasa?
Mtu kama Prof. Kapuya ina tambulika kabisa kuwa ni mtaalamu wa mifupa. Kwenye nchi iliyo na upungufu wa madaktari bingwa kwa nini huyu bwana hashughuliki na taaluma yake?
Nime taja hawa baadhi siyo kwa ajili ya kuwa single out ila kama kutolea mfano watu ambao nina uhakika na elimu zao. Kwenye siasa leo upo kesho haupo. Kwenye siasa ina tegemea sana na mazingira. Kwa nini wanataaluma hawa washughulike na siasa ambayo ni bahati nasibu kuliko kutumikia taaluma zao?
Mimi naheshimu sana watu kama wakina Prof. Othman Haroun (R.I.P.) na Prof. Shivji. Hawa ni wanataaluma ambao hawaja kimbia taaluma yao. Inapo bidi wanaikosoa serikali ila hawaingii kwenye siasa. Kwa nini na wengine wasifanye hivyo?
Katika nchi yoyote dunia kazi mbali mbali zina hitajika kuendeleza taifa. Siasa siyo mahali pekee kwa kuleta mabadiliko na mageuzi. Tuki kazania siasa na kupuuzia taaluma zetu tuta jikuta tuna geuka nchi ya wanasiasa tupu isiyo na mabadiliko yoyote. Je tatizo ni nini?