kwa nini wanasiasa wa TZ husaka kwa udi na uvumba PHDs feki za heshima............... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwa nini wanasiasa wa TZ husaka kwa udi na uvumba PHDs feki za heshima...............

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 4, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  unapoona wanasiasa wengi wanafukuzia PHDs za heshima (Honoury Doctorates) ndani na nje ya nchi ni wakati mwafaka tukaanza kujiuliza ni msukumo upi unaowatuma wajidhalilishe heshima zao (kama zipo) mbele ya jamii kwa kujivika vilemba vya ukoka...............................................??????????????????????

  baadhi ya misukumo walionayo ni pamoja na:-

  a) kukidhi mahitaji yao binafsi ya elimu bandia baada ya kubaini ya kuwa hawana uwezo wa kukaa darasani na kuipata kihalali.............hivyo kuinunua inakuwa ni jibu la kutimiza ndoto zao ghiliba............hawa ni wa kuwaogopa kwa kuwa maisha yao yote hutegemea kudhulumu kwa kuchakachua haki za wenzao..........

  b) kiu yao ya elimu tajwa ni kuiitishia jamii kuwa wamesoma na hivyo wana kiona mbali na kutarajia jamii itawaogopa na kukaa kimya kuvumilia faulo nyingi wanazozicheza dhidi yetu...................wakisahau kuwa jamii itawapima siyo kwa makabrasha wanayotudobosha nayo bali kwa huduma wanazozitoa kwa jamii wanayoishi..............na faulo za hapa na pale siyo huduma stahiki ambayo jamii inatarajia kwa viongozi wao wawe na PHD feki au la..........................


  c) viongozi wengi wa nchi masikini kama hii yetu huabudu makaratasi lakini wenzetu wa nchi zilizoendelea huona hata aibu kuzungumzia elimu yao kwenye nafasi za umma kwa sababu hujua kazi ya siasa ni kutimiza wajibu uliopo mbele yao tu na wala siyo kujivunia sifa zilizopo kwenye makaratasi..............uhalali wao wanasiasa tajwa ni kuhudumia jamii tu na wala siyo uhalali huo kupatikana katika sifa ziliopo kwenye makaratasi tajwa............mfano Condoleesa Rice alikuwa ni profesa wa Russian studies na profesa kabla ya kuwa kwenye serikali ya Bush lakini kamwe akiwa waziri wa marekani hakuwahi kuitwa kwa uprofesa wake au udaktari wake................lakini kwetu huku kwa wanasiasa uchwara na wababaishaji uprofesa na udaktari hutukuzwa sana kama sifa za uongozi bora!!!!!!!!!!!!!


  d) wengi wa wanasiasa wenye PHD tata utawakuta ni waathirika wa kisaikolojia kwa sababu wanajuafika utendaji wao ni goigoi lakini hupata msukumo wa kutafuta sifa bandia ili kutuhadaa kuwa wako imara wakati ni la hasha.............................angallia PHD tata na utaona utendaji wake ni bomu tupu....................

  e) upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya uteuzi wa senati na mabaraza ya vyuo vikuu vyetu haswa vinavyomilikiwa na serikali pamoja na upeanaji wa PHDs bandia............................wengi ya wajumbe wa senati za vyuo vikuu tajwa hawana sifa za kuwa wajumbe wa taasisi tajwa na namna ya kushukuru nao kuvikwa vilemba vya ukoka huamua kwa makusudi mazima kuwavika wababe wao serikalini vilemba tajwa..............................na ndiyo maana siyo rahisi kuona chuo kikuu cha serikali kumpa PHD ya heshima raia yeyote yule ambaye si waziri au raisi...ambaye anastahili kupewa heshima tajwa kwenye mchango wake kwenye jamii.........na wastaafu wa uwaziri na uraisi katika nyadhifa tajwa.............................kamchezo haka kanashusha hadhi za vyuo vikuu vya serikali kwa kuonyesha kumbe taasisi tajwa ndiyo chimbuko la kuanguka kwa maadili ya jamii.......

  f) kwa kuelewa wanasiasa tajwa hawana sifa vyuo vikuu aidha hushindwa kutoa maelezo ya kuhalalisha vigezo walivyovitumia kumbeba mwanasiasa tajwa na alilinganishwa na akina nani katika tanuru la kutenda haki...........................na hivyo senate tajwa huishia kutoa maelezo ya kiujumla tu................................nchi ya namna hii kama yetu ambayo wasomi wake kwenye vyuo vikuu wanawaabudu wanasiasa haiwezi kuwa na nuru ya maendeleo na itaishia kujitetea kuwa "kwas sabau zisizoweza kuzuilika wameshindwa kuleta maendeleo.............................."

  g) wengi ya wanasiasa uchwara tajwa utakuta hii laana ya kujitafutia vitu kwa wizi na udanganyifu tayari wamewaambukiza hata watoto wao.......................matokeo yake watoto wao hujikuta wakiletewa mitihani ya wizi na wazazi wao ili waonekane na jamii kuwa wanauwezo mkubwa wa darasani jambo ambalo siyo kweli....................................uwezo bandia wa darasani unakuwa ni kigezo cha kupata nafasi za elimu ya juu na nyadhifa serikalini na makampuni binafsi.........................................huku watoto wa hoehae wakibidiishwa kujiajiri tu..........


  baadhi ya hawa wanasiasa babaishi ni pamoja na...............................................ninawaachia mjazilize wenyewe...............
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Jana kwa mfano waziri mmoja kapata digrii ya udaktari ya Mzumbe...........na huyu waziri ni mhitimu wa mzumbe kwenye stashahada ya miaka miwili na alikuwa akijiita daktari sasa huu udaktari wa pili wa nini kama kweli yeye alikuwa ni daktari?

  kwa maelezo yake mweyewe ameasa raia wawe na moyo wa kujisomea kama yeye!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  hivi kusoma kweli mnaanza mkiwa mawaziri.........................na kabla ya hapo ugumu huwa uko wapi?????

  ukichunguza sana utakuta ya kuwa ni mashinikizo aliyokuwa nayo kutoka kwenye jamii kuwa udaktari wake ulikuwa ni bandia...............kwa hiyo anatafuta namna ya kuhalalisha udaktari wake ili aendelee kutesa kwenye hii serikali isiyo na khofu mbele ya Mwenyezi Mungu........
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  huyu asema ni ya halali...................lakini kama ile ya magufuli ina utata mkubwa......................profesa nao wamo katika kuwasaidia wanasiasa kupata shahada za udaktari......profesa anayekusimamia aweza kukupatia shahada tajwa na hakuna wakubisha................sisi tusubiri michango ya wahusika katika maendeleo ya jamii......................na hii ni udaktari wa pili...........

  Habari za Kitaifa

  Dk. Nchimbi ataka vijana kuzama katika masomo
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu,Morogoro; Tarehe: 3rd December 2011 @ 13:10 Imesomwa na watu: 109; Jumla ya maoni: 0

  [​IMG]
  [TABLE="align: right"]
  [TR]
  [TD="align: right"]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="align: right"]
  [TR]
  [TD="class: kaziBody, align: left"]Habari Zaidi:[/TD]
  [/TR]
  [TR]

  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  [TABLE="align: right"]
  [TR]
  [/TR]
  [TR]

  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi amewataka vijana nchini kujenga tabia ya kujiwekea malengo na kujiendeleza kimasomo ili waweze kujiletea maendeleo yao na taifa kwa ujumla kama njia ya kupiga vita umasikini.

  Dk. Nchimbi alitoa ushauri huo muda mfupi mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Uzamivu (PhD) na Chuo Kikuu Mzumbe katika Mahafali ya kumi ya Chuo hicho mkoani Morogoro kuwa elimu nguzo muhimu inayoweza kuwakomboa vijana nchini.

  "Ninawaasa vijana kuwa na malengo na kupanga muda wao ili kutimiza ndoto zao za maisha, kielimu na kazi mbalimbali, kwani mimi niliweza kufanya hivyo na nimetunukiwa na wenzangu Shahada ya juu za Uzamivu (PhD)," alisema Dk. Nchimbi ambaye alikuwa miongoni mwa wahitimu saba waliotunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Samatta.

  Alisema shahada hiyo aliipata baada ya kufanya utafiti kwa kuangalia ni jinsi gani mikopo midogo inavyoweza kuondoa umasikini miongoni mwa jamii na anajisikia fahari ameweza kufanya jambo hilo na kulifanikisha.

  "Tatizo linalonisumbua siku zote ni umasikini miongoni wa jamii na kwa upande wake Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za makusudi katika kuondoa umasikini," aliongeza.

  Alisema mwito wake kwa vijana ni kujenga tabia ya kujipangilia muda na kuwa malengo katika maisha kwani muda haumsubiri mtu.
   
 4. Cha Moto

  Cha Moto JF-Expert Member

  #4
  Dec 4, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 945
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  PhD. zenyewe hata sijaona msaada wake zaidi tu ya maisha magumu kwa kila mTZ yanaongezeka
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  baadhi ya maswali ambayo nchimbi atapata muda mgumu kyajibu ni hivi alihitaji kweli phd ya pili kama kweli alikuwa na ya kwanza...................au hii ya pili ni kufukia mashimo ya ile ya kwanza iliyoyachimba.............

  hata huyu jaji mstaafu samatta sijui alifikaje kwenye kitebe cha kuwa mkuu wa chuo.................hana historia yoyote na usimamizi wa vyuo vikuu..........................
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  zingelikuwa na tija nchii hii ingelikuwa ni tajiri sana..............
   
Loading...