Elections 2010 Kwa nini wanarekodi namba ya mpiga kura kwenye karatasi ya kupigia kura

Msongoru

JF-Expert Member
Apr 16, 2008
306
24
moyo umeshtushwa, swali hili ni kubwa na la kweli. kama kura ni siri, vp waandike tena namba? kwa mantiki hyo kila kura inajulikana nani kampigia nani?
Hata hvyo kwa nini? je kuna uhusiano wowote na uchakachuaji?
 
For audit purpose kama kuna discrepancies kucross check ni rahisi
 
Mimi hata wakinijua hawatanifanya kitu

Uzuri ni kwamba hizo namba hazibaki kwenye karatasi unayokwenda kutia tiki. Hakuna mtu anaweza kujua kura fulani ilipigwa na fulani.

Hofu yangu mimi ni yale majina yanayobaki kutokana na wahusika kutokufika kupiga kura. Yanapelekwa wapi? Hayapigishwi?
 
Man, liberation struggle has its own price. Do not fear anybody fear only God the Almighty. Go and vote for CHANGE even if they know you what are they gonna do?
!!!!! GO DR SLAA GO!!!!!!!!!
 
Uzuri ni kwamba hizo namba hazibaki kwenye karatasi unayokwenda kutia tiki. Hakuna mtu anaweza kujua kura fulani ilipigwa na fulani.

Hofu yangu mimi ni yale majina yanayobaki kutokana na wahusika kutokufika kupiga kura. Yanapelekwa wapi? Hayapigishwi?

Nadhani hakuna hofu hapo. Kwani karatasi za kupigia kura hazina namba.
 
Nadhani hakuna hofu hapo. Kwani karatasi za kupigia kura hazina namba.

Lakini picha na majina vina namba.

(si unakumbuka ukiingia kwenye chumba kwanza unakutana na mtu anayekuomba kitambulisho na kuhakiki kama ni wewe kweli kwa ku-compare na karatasi zake za picha na ID?).

Naomba tuwekane sawa hapo.
 
Hilo ni sawa. Kumbuka ile namba wanayorekodi inabaki kwenye kishina tu na sio kwenye zile karatasi unazopewa kwenda kuweka tick! Wanaweza kujua nani kapiga kura na nani hajapiga, lakini hakuna anayeweza kujua wewe umempigia nani kura yako.
 
Nadhani hapo imeeleweka.
 
msiwe na wasiwasi..............pigeni kura....hakuna atakayejua nani kampigia nani...................
 
Hilo ni sawa. Kumbuka ile namba wanayorekodi inabaki kwenye kishina tu na sio kwenye zile karatasi unazopewa kwenda kuweka tick! Wanaweza kujua nani kapiga kura na nani hajapiga, lakini hakuna anayeweza kujua wewe umempigia nani kura yako.

Suala la kujua nani kampigia nani nimeshakubali kuwa si rahisi kujua.

Swali langu ni kuhusu uwezekano wa watu wasiojitokeza kupiga kura 'kupigiwa' na NEC ya CCM.

Why?

Yule mtu mwenye 'daftari' ana vitu vitatu: picha, jina na ID.

Kama muda wa kupiga kura uliowekwa kisheria ukipita ba bado mtu wa NEC akabaki na watu wasiopiga kura kwenye daftari lake, je hamuoni kuwa watu hao wanaweza kupigishwa kura?

Mbona tunasikia kuna watu walishakufa na wanapigishwa kura.

Itakuwaje kwa wale wasiohudhuria (wako hai) vituoni kupiga kura?
 
Uzuri ni kwamba hizo namba hazibaki kwenye karatasi unayokwenda kutia tiki. Hakuna mtu anaweza kujua kura fulani ilipigwa na fulani.

Hofu yangu mimi ni yale majina yanayobaki kutokana na wahusika kutokufika kupiga kura. Yanapelekwa wapi? Hayapigishwi?
Hakuna muda wa kufanya kazi hiyo...Kama vituo vinafungwa saa 12, ni saa ngapi watafanya kazi hiyo, pia hata kama wakijaribisha, watafanikiwa kuongeza kura ngapi?
 
Nadhani hapo imeeleweka.

Labda niliona kimakengeza? kwani niliona namba aliiandika kwenye karatasi yangu ya kupiga kura, pia kaikopi kwenye kile kishina! Na hata nilipo ng'aka, msimamizi na mawakala walikubaliana namimi, ila kwa upole wakadai ndo maelekezo walo pewa na NEC, na kunitaka niandike malalmiko yangu kwa NEC ambayo kwa vyvovyte vile najua nizuga tu..

Kwa maana hiyo wanaweza jua kabisa nani kampigia nani, sema kwamba kwa vile karatasi ni nyingi inahitaji muda mrefu kufatilia na kuchambua ili ajue nani kampa nani, lakini akipenda anaweza kwa kadri nilivo ona na kulalamika!
 
Zile fomu za kupigia kura hazina serial number ambayo inaendana na kishungi kinachosalia kwa msimamizi. Hakuna ambaye anaweza kujua ni nani kampigia nani kura. This is purely for AUDIT TRAILS should there be any discrepancies.

Pia itasaidia kuthibiti uchakachuaji, endapo mtu atarejea mara ya pili nao wakamtilia wasiwasi kwamba kadi yake imekwishatumika.
 
Mimi nimekagua na kuhakikisha kuwa hizo namba hazibaki kwenye karatasi unayokwenda kutia tiki. Hii ina maana kuwa hakuna mtu anaweza kujua kura fulani ilipigwa na fulani, unless kama namba zimewekwa kwa water mark ambayo kuijua ni mpaka uiangalie hiyo karatasi kupitia kwenye mwanga!!.
 
Wasiwasi wangu ni kwamba wameamua kuandaa karatasi hizi zenye utata za kupiga kura ili kuwadhibiti watanzan ia wazalendo wanaofanya kazi kwenye taasisi nyeti za serikali ili wajue nani kampigia nani.
Huu ni ubakaji wa demokrasia. (kuna mtu alituambia hapa kwamba TISS ilirekodi namba za wafanyakazi wake woote ili kuwawajibisha endapo watapigia upinzani)

Natamani wangeziacha idara za serikali hasa vyombo vya usalama viwe huru kwa manufaa ya watanzania jamani.
I will advocate that
 
Mimi nimekagua na kuhakikisha kuwa hizo namba hazibaki kwenye karatasi unayokwenda kutia tiki. Hii ina maana kuwa hakuna mtu anaweza kujua kura fulani ilipigwa na fulani, unless kama namba zimewekwa kwa water mark ambayo kuijua ni mbaka uiangalie hiyo karatasi kupitia kwenye mwanga!!.
Imekula kwako mama yangu mzazi.
Ile namba inayobakia kwenye register ina reg. namba ya voting paper hivyo ni rahisi kuverify nani kampigia nani kwa kuoanisha namba ya kura na ya kitini.
umecheki eeeh!!??? niliwaambia Lewis na Kiravu ni WANGA wetu mkakataa
 
Msanii, karatasi tumezihakiki, number inabaki kwenye shina. Karatasi za kura hazina number KABISA.
 
kile kishina kinachobaki lazima kitakuwa na unseen bonding identity ambayo wakiangalia kupitia ultaviolet light watajua namna ya kuunganisha kishina na hizo karatasi ulizopewa. ni sawa na zile karatasi za kutengenezea pesa. kuna maandishi huwezi kuona kwa macho ya kawaida. hichi kitu nilishindwa kuwa mkali kwasababu kitambulisho changu kilikuwa kimechoka sana na nafkiri nilipata tu favor. maana walishaanza kunichenchia. sasa na mimi ningeanza kuhoji kuhusu utaalam wanaoutumia kubaki na ID number yangu. du! ingekuwa sooo. Lakini nawaomba wale kina slaa, mnyika, lipumba ambao mpo humu mtusaidie.
 
Back
Top Bottom