Kwa nini wanandoa wasiopata mtoto lawama huelekezwa kwanza kwa mwanamke??

Kingcobra

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
1,000
309
Wapenzi wanaJF,
Kuna tabia imejengeka tangu enzi na enzi ya kuelekeza lawama kwa mwanamke pindi ndoa inapokosa mtoto. Mbaya zaidi, mwanamke ndiye anayesukumwa aende hospitali kupimwa. Halafu hata akipimwa na kuonekana hana matatizo mwanaume anakuwa mgumu kupimwa ana lawama zinaendelea kuelekezwa kwa mwanamke. Kwa maeneo mengine, mwanamke ndiye anayekuwa mhanga wa hilo tatizo hata kama wakati mwingine siyo yeye aliyesababisha. Hivi ni kwa nini tabia hii imeshamiri kiasi hicho? Kwa nini wanaume wengi hawapo tayari kupimwa, kama ilivyo kwa wanawake?
 
Ukandamizaji kwa wanawake ulianza tangu enzi za zamani. Ila siku hizi no tunakwenda wote hospitali hakuna mchezo kabisa
 
Hivi wakati ukandamizaji ulipoanza wanawake walikuwa wapi mpaka wakaruhusu hii kitu?
 
Mwanamke uwa wa kwanza kushukiwa kwa sababu mazingira ya yeye kuwa mgumba ni natural na kujitakia kama kutoa mimba, kunywa madawa ya kuzuia mimba n.k. lakini mwanaume yeye ni nature tu - shaft kutokusimama, mbegu kutokukomaa, fluid ya kuondoa chumvi kwenye shaft ili mbegu zipite bila kufa hayapo lakini la kwanza linabatilisha ndoa.
 
Hivi wakati ukandamizaji ulipoanza wanawake walikuwa wapi mpaka wakaruhusu hii kitu?

Mkuu hizo enzi za mwalimu zimepita siku hizi tuko ngangari mpaka clinic tunakwenda wote usifanye mchezo kabisa na gender balance ya siku hizi wamama zetu wazamani walikuwa waoga, wapole, wanyenyekebu nk lakini siku hizi umpate wapi.

Wote tunatoka asubuhi tena unaendesha gari namimi naendesha unapata mshahara na mimi napata utanibabisha na nini thubutu
 
hapo sasa!
 
Elimu tu ndugu yangu, mwenye kuelimika vizuri sidhani kama ataleta ligi hiyo iwapo tatizo kama hilo litajitokeza
 
Nadhani kuna tatizo kwa watu/wanaume wengi kushindwa kutofautisha kati ya sperm (shahawa) na semen (manii). Sperm ndio mbegu wakati semen yenyewe ni kama chombo tu kinachobeba hizo sperm wakati wa kutoka. Hivyo semen peke yake haiwezi kamwe kusababisha mimba. Sperm zinatoka kwenye makende wakati semen kwa sehemu kubwa zinatoka kwenye matezi yaliyopo kwenye njia ambayo sperm zinapitia wakati wa kutolewa nje. Mara nyingi kinachoonekana kwa macho ni semen na hata kiujazo zenyewe ni karibu asilimia 95 ya kile tunachokiona.

Sasa mwanaume anaweza kuwa anatoa semen tu na kudhani anao uwezo wa kutia mimba. Katika mahusiano mengi yaliyokosa motto/watoto lawama inaangukia kwa mwanamke kuwa hazai kwa sababu mwanaume ‘ana uhakika' kuwa anatoa ‘sperm' kumbe ni semen tu (au pengine ni sperm lakini katika kiwango ambacho hakitoshelezi....low sperm count). Inakuwa ni kama vile mwanaume aliyefanyiwa vasectomy, kwa maana ya kuendelea kuwa na uwezo wa kutoa semen ambayo haina sperm.

Kiwango (na ubora) cha sperm kilichopo kwenye semen ni muhimu sana katika ku determine kama mwanaume anaweza 'kuzaa' (kutia mimba!) ama hapana. Sio rahisi kwa macho pekee, mwanume kujua kama manii anayoitoa ina sperm au haina. Sasa hili ndilo hasa linafanya iwe muhimu kwa wanaume pia kwenda hospitali kupima ili wajue kama uwezo wa ‘kuzaa' upo.

Wapenzi wanaJF,
Kuna tabia imejengeka tangu enzi na enzi ya kuelekeza lawama kwa mwanamke pindi ndoa inapokosa mtoto. Mbaya zaidi, mwanamke ndiye anayesukumwa aende hospitali kupimwa. Halafu hata akipimwa na kuonekana hana matatizo mwanaume anakuwa mgumu kupimwa ana lawama zinaendelea kuelekezwa kwa mwanamke. Kwa maeneo mengine, mwanamke ndiye anayekuwa mhanga wa hilo tatizo hata kama wakati mwingine siyo yeye aliyesababisha. Hivi ni kwa nini tabia hii imeshamiri kiasi hicho? Kwa nini wanaume wengi hawapo tayari kupimwa, kama ilivyo kwa wanawake?
 
Mkuu hizo enzi za mwalimu zimepita siku hizi tuko ngangari mpaka clinic tunakwenda wote usifanye mchezo kabisa na gender balance ya siku hizi wamama zetu wazamani walikuwa waoga, wapole, wanyenyekebu nk lakini siku hizi umpate wapi.

Wote tunatoka asubuhi tena unaendesha gari namimi naendesha unapata mshahara na mimi napata utanibabisha na nini thubutu

we mwanamke we ni mmachami au mnyakyusa wa kyela?............ nyie mnaotaka usawa utawacost, hata maandiko yanasema mwanaume ni kichwa cha familia
 
MBONA WANYAKYUSA NA WAMACHAME......au ndio wanao ongoza kwa utata na ukakasi.
 
Hali hii ilikuwepo zamani, siku hizi sio sana sababu uelewa wa watu unazidi kuwa mkubwa..., Alafu kuna njia nyingi wanandoa mkikosa mtoto mnaweza kuishi kwa upendo.. Adoption ikiwa ni njia moja wapo (mtoto mkimpa malezi kama wa kwenu tangia mdogo attachment itakuwepo sawa kama vile ni wa kwenu)
 
Back
Top Bottom