Kwa nini wanakimbia radio one/itv

Gudboy

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
867
77
Jamani ndugu wadau, naomba mnifahamishe mana sasa hivi kuna lindi kubwa la wafanyakazi wa IPP media kukimbia na kwenda kufanya kazi kwenye vituo vingine vya radio au television. Kwani kuna tatizo gani pale IPP media? Juzi tu nasikia Mirald Ayo na Regina Mwalekwa wamekimbilia clouds.

Mwenzenu nijuzeni kuhusu hili, mwenye kufahamu amabye pia ni mfanyakazi au anahusika na IPP media ruksa kumwaga siri ya hii kampuni kongwe kwenye maswala ya habari.

Naomba kuwasilisha
 
Wawili tu wanakufanya upige yowe? unajua wangapi walioondoka clouds kwa mwaka huu pekee??

tafakari
 
Huenda mnasakama vyombo vya habari kwa kuwa ndio wanaofahamika. Watu wengi huhama mahali walipo kwa ajili ya kutafuta challenges na opportunities. Sasa mtu akihama kuna tatizo? Inamaana huko mtaani watu hawaachi kazi na kukimbilia sehem nyingine? Ni sehem ya maisha kusonga mbele.
 
Ni jambo la kawaida wafanyakazi kuacha, makampuni mangapi watu wanaacha kazi? Who is Regina mpaka kuhama kwake kuwe issue? Mi kama mwajili natambua kuwa employees saa yoyote wanaweza kuacha kazi na wako huru na siwapi mikataba ya kuwafunga!

Halafu, pale Radio One/ITV kuna yule mama mkuu wa kitengo ndo huwa analalamikiwa na kila mfanyakazi anayeacha kazi, ni wa kuangaliwa sana. Nina imani na mzee Mengi na najua anaweza kuchunguza nini chanzo, cannot blame him katika masuala ya uajili
 
Hapo Clouds kwenyewe wangapi wameshahama kwa mwezi wa November pekeyake?
 
Mtoa mada,naona maslahi zaidi ndiyo yanayowafanya watu waache kazi. Lakini sidhani kwamba IPP inaongoza, unaona hivyo sababu unawajua hao watangazaji. Kuna makampuni madogo tu,watu wanaondoka zaidi ya 20 kwa mwaka.
 
sasa na wewe unamuuliza swali ili iweje? hujamjibu bado kama unajua sema tusikie NASI TUJUE BILA MASHINDANO
 
Poor internal marketing, focus ya kampuni nyingi ni kutazama wateja wa nje na kusahau wateja wa ndani ambao ndio staff. Mara nyingi kampuni hizi promotion ni kwa know who? na sio merits.

Popote pale sababu kubwa ni boss kwanza zingine zinafuata, wasimamizi ndio noma.
 
Wawili tu wanakufanya upige yowe? unajua wangapi walioondoka clouds kwa mwaka huu pekee??

tafakari
kaka sio wawili, IPP Media kwa mwaka huu imeondokewa na wafanyakazi wengi sana, noja nikutajie ninao wakumbuka. 1. Kijo, 2. Muro, 3. maimatha, 4. ze comedy group, nk. Halafu hawa wanaanza kazi wakiwa sio maarufu, lakini wakipata tu umaarufu wanachapa lapa kwingineko. Halafu sijalalamika ila nilitaka kujua ni kitu gani kinawakimbiza huko?
 
Huenda mnasakama vyombo vya habari kwa kuwa ndio wanaofahamika. Watu wengi huhama mahali walipo kwa ajili ya kutafuta challenges na opportunities. Sasa mtu akihama kuna tatizo? Inamaana huko mtaani watu hawaachi kazi na kukimbilia sehem nyingine? Ni sehem ya maisha kusonga mbele.
nakubaliana na wewe, kumbe moja ya sababu ni maslahi
 
Hapo Clouds kwenyewe wangapi wameshahama kwa mwezi wa November pekeyake?
naomba tusaidiane kuwaorodhesha wote waliokimbia clouds, mimi najua Gadner ndio ameng'atuka wengine siwajui
 
Mtoa mada,naona maslahi zaidi ndiyo yanayowafanya watu waache kazi. Lakini sidhani kwamba IPP inaongoza, unaona hivyo sababu unawajua hao watangazaji. Kuna makampuni madogo tu,watu wanaondoka zaidi ya 20 kwa mwaka.
halafu kuna mdau kanidokezakuwa pamoja na maslahi ila pale IPP hakuna ajira zaidi ya kuwa kibarua muda mrefu, je kuna ukweli wowote juu ya hili waungwana?
 
sasa na wewe unamuuliza swali ili iweje? hujamjibu bado kama unajua sema tusikie NASI TUJUE BILA MASHINDANO
si ndio hapo mkuu, mana kama unajua unaorodhesha ili nasi tujue, maana hapa tupo kwa ajili ya kujadiliana, yale majadiliano ndio huzaa muafaka. Ninacho fahamu mimi si kila mtu anajua kila kitu bana, tusaidie wajameni
 
Ni jambo la kawaida wafanyakazi kuacha, makampuni mangapi watu wanaacha kazi? Who is Regina mpaka kuhama kwake kuwe issue? Mi kama mwajili natambua kuwa employees saa yoyote wanaweza kuacha kazi na wako huru na siwapi mikataba ya kuwafunga!

Halafu, pale Radio One/ITV kuna yule mama mkuu wa kitengo ndo huwa analalamikiwa na kila mfanyakazi anayeacha kazi, ni wa kuangaliwa sana. Nina imani na mzee Mengi na najua anaweza kuchunguza nini chanzo, cannot blame him katika masuala ya uajili
sawa kabisa mkuu, yawezekana hayo yote uliyoyasema yakawa ni sababu tosha, big up kwa majibu mazuri
 
Biashara yenyewe ikiwa inalega lega mtu anabadilisha au anaacha kabisa.
Maslahi na heshma kazini. Hata kama mnanilipa vizuri lakini heshma yenu inashuka lazma nitaacha.
 
Mara nyingi kuhama mahali pa kazi ni maslahi tu, so ni mtazamo wa mtu mwenyewe!
 
kaka sio wawili, IPP Media kwa mwaka huu imeondokewa na wafanyakazi wengi sana, noja nikutajie ninao wakumbuka. 1. Kijo, 2. Muro, 3. maimatha, 4. ze comedy group, nk. Halafu hawa wanaanza kazi wakiwa sio maarufu, lakini wakipata tu umaarufu wanachapa lapa kwingineko. Halafu sijalalamika ila nilitaka kujua ni kitu gani kinawakimbiza huko?
hivi maimatha alikua itv au east african?
 
Back
Top Bottom