Kwanini Wanajeshi wa Tanzania wanashambuliwa DRC?

hao walikuwa walinzi wa amani ambao mpaka uwachokoze ndo wanajihami,wapo kule kwa ajili ya kuhakikisha maridhiano yanapatikana na kulinda raia.Nakuomba usipotoshe umma na itikadi zako za kisiasa;jeshi halipo kisiasa,wala urafiki wa mtu na mtu;kwani awamu ya JK;Hakuna walinzi wetu wa amani walio kufa huko kongo,sudani;lebanoni n.k.
 
Kwa kweli naongea kwa masikitiko makubwa sana, hivi kweli Wacongo wanaweza kuwauwa Watanzania kama hivi?, jibu ni BIG NO, Watamzania tunaheshima kubwa sana Congo, sisi ndio ndugu wa damu pekee kwa waCongoMan, nimezunguka Congo, hasa niseme East Congo, Nord Congo na Katanga province, kote huko (naomba niongee kicongo) Batanzanie ni batu ba kuheshimika sana,
Sio rahisi kwa mcongoman kumuua Mtanzania, Nasema hivyo kwa ushahidi wa 100% haiwezekani, hata hao watu wa Maimai chini ya Jean Kutumba aliyepo Ubembe kamwe hawezi kumuua Mtanzania, au kwa Raia Mtomboki aliyepo Urega, Shabunda, Mtanzania ni mtu wa thamani sana DRC

KITENDO CHA WATANZANIA KUWA KARIBU NA RWANDA (TUTSI) NDIO TUMEJICHIMBIA KABURI KUBWA SANA. KAMWE HATUWEZI KUWA SALAMA DRC,
Mision yetu ya kwanza tuliyokuwa nayo Congo sio tuliyonayo yo sasa (back door)"
Kamwe hatuwezi kuwa salama

Uncle kwa Siasa zako za East Africa unazoziendesha ni Bora kuwarudisha vijana wetu Nyumbani, nje ya hapo kwa kweli tutalia sana, Uncle unamapungufu makubwa sana kwenye Uelewa wako wa siasa za East and Central Africa, hasa Tutsi wakiwa main subject

Sina mengi, mods mkiamua kuufuata huu uzi sawa, lakini ntakuja na detailz za siasa za Tanzania, Rwanda, DRC na wapi tunakosea

CC: Nguruvi3 , JokaKuu , Mag3 , Pascal Mayalla
Nadhani ww ndio uelewi, je unajua kwamba vikundi vingi vya waasi Congo asili yao ni kutoka nje ya Congo?
 
Tunalala kwenye vumbi na matope ili wewe ulale kitandani,

Tunala na bunduki ili wewe ulale na mwenzi wako,
Tunalala porini ili wewe ulale kwenye nyumba,

Unavaa kofia maridadi ya kupendeza, sisi tunavaa kofia ngumu na nzito za chuma,
Unavaa "vest" nzuri ya pamba, sisi tunavaa "vest" za shaba,
Unavaa mkanda wa ngozi kiunoni, sisi tunavaa mikanda ya risasi,

Asubuhi unaamshwa na "alarm" nzuri ya simu yako, sisi tunaamshwa na milio ya mabomu na risasi,
Unatembelea gari zuri la thamani, sisi tunatembelea vifaru na malori,

Unakula chakula kizuri ukipendacho, tunakula wadudu na matunda porini,

Tunakesha ili wewe upate usingizi,

Tunauawa ili wewe uishi,
Tunaumia ili wewe upone,

Tunaitoa sadaka "leo yetu" kwa manufaa ya "kesho yako",
Tunatoa sadaka maisha yetu ili kutetea maisha yako,

Tunakupigania usiku na mchana kwa sababu tunakupenda,
Tunaipenda nchi yetu,

Sisi ni wanajeshi,
Sisi ni wazalendo,
Sisi ni mashujaa,

Ombea wote waliofia vitani,
Wamekufa wakitetea nchi yetu,
Wamekufa wakitetea uhai wako,
Ni mashujaa wetu,

Nchi yetu,
Amani yetu,
Jeshi letu.
MUNGU LIBARIKI Jeshi La Wananchi wa Tanzania (JWTZ)!
 
Kagame hawezi kuwa mshauri wako wa karibu then ukabaki salama haiwezekani.
Watusi wanaitawala Kongo kwa msaada wa kagame na mseven ambao wote ni wakaribu sana kwa Dereva wa pulling.
Ikiwa watz twaweza kuvumilia nchi yetu kuongozwa na raia wa kigeni basi tuwasihi wakongo Wa vumilie ikiwa hatuwezi basi tuwasaidie kuondoa utawala huo. Tutaona mengi.

Hyo rwanda kila siku mwasema n kama mkoa wa mtwara leo hii inatawala Tz kwel ahahaaaaaaaa
 
Hyo rwanda kila siku mwasema n kama mkoa wa mtwara leo hii inatawala Tz kwel ahahaaaaaaaa
Kinachotawala ni akili ya kiongozi siyo ukubwa wa nchi. Nyerere alikuwa mmoja lakn alidrive akili za viongozi wote Africa na wakamwelewa.
Sasa usiombee kupata kiongozi mbovu popote lazima mjute.
 
Niko na mashaka sana baada ya bombadia kushikiliwa kama haitoshi ni kuhujumu heshima na sifa ya JWTZ. Hawa watu walio zuiliwa makanikia yao wako very strategic. Moja ya pride yetu kama nchi ni utendaji wa jeshi letu na TISS.

Hawa wameabika baada ya kushikwa redhanded na nakanikia yenye udanganyif,u, so wako katika kutuhujumu hasa kuichafua serikali na kiongozi wetu mkuu. Maneno kama, "tumewapa wa shamba kuongoza nchi" si fikiri kama yana kuja tu hivihivi, ndio sifikiri.
 
Kwa vyovyote vile tunaponzwa na sizonje kuwa karibu na Paul Kagame,, kagame Ana akili ya kung'ata na kupuliza.
Lakin huyu wetu anadhani ndio sifa kuwa karibu na kagame na mbaya anaingia kichwa kichwa atakumaliza we gosha kwan jakaya hakuwa mjinga eti.
Kagame ni nyoka hatari Sana Katika jumuiya ya AFRICA MASHARIKI
Hapa tu bongo kamwaga majasusi kila kona na usishangae anajua hadi kitanda cha Ngosha kipo kona gani ya nyumba.
M23 walikuwa vijana wa kagame, na ana kinyongo Kapigwa na JWTZ.
Kwa mtazamo wangu tumepigwa na huyu mbwa wa Rwanda. Ngosha tafadhali Sana sikiliza Ushauri watu lasivyo utatuponza Sana.
 
hao wanajeshi wa UN wakifika Congo hawajishughulishi na kulinda amani.....wanatafuta madini na wao wanakuwa hawana tofauti na waasi, huo ndio ukweli mchungu hao wameingiliana kwenye magendo yao ya kutafuta madini na hao waasi.....
Unamaanisha na wajeda wa jwtz pia au?
 
Mi naona JWTZ wote tungewapeleka congo tuoneshe thamani ya askari wetu 14 tukateketeze mpaka vijusi wa waasi na kuku waoo
 
Hapa natrgemea kuona jeshi letu likiwaadhibu hao maharamia wauaji na tuwaoneshe namna gani tupo imara na michezo yao ya kuvamia kwa kidali poo
 
Kwa vyovyote vile tunaponzwa na sizonje kuwa karibu na Paul Kagame,, kagame Ana akili ya kung'ata na kupuliza.
Lakin huyu wetu anadhani ndio sifa kuwa karibu na kagame na mbaya anaingia kichwa kichwa atakumaliza we gosha kwan jakaya hakuwa mjinga eti.
Kagame ni nyoka hatari Sana Katika jumuiya ya AFRICA MASHARIKI
Hapa tu bongo kamwaga majasusi kila kona na usishangae anajua hadi kitanda cha Ngosha kipo kona gani ya nyumba.
M23 walikuwa vijana wa kagame, na ana kinyongo Kapigwa na JWTZ.
Kwa mtazamo wangu tumepigwa na huyu mbwa wa Rwanda. Ngosha tafadhali Sana sikiliza Ushauri watu lasivyo utatuponza Sana.

Sizonje ndio nini hapo naona hilo neno linajurudia rudia, Sizonje sindimanye mwee ndi kiki? ngusa kono kutitu tulongane unofu nofu
 
Tatizo Sizonje anadhani anamkomoa mbowe na cdm kwa kuwa karibu na kupata "semina elekezi" ya jinsi ya "kuongoza nchi" kutoka kwa kagame.

Kikwete hakuwa mjinga.

Sasa yeye hadi "jumba jeupe" kaweka askari wa rwanda wamlinde badala ya askari wa kitanzania.

Na kagame alivyo shetani anajifanya kujenga urafiki na sizonje huku anammaliza taratibu.

Sizonje atakuja shtuka ashawekwa kando, atabakia kuwa "rubber stamp" ya kagame.
 
Back
Top Bottom