Kwa nini waliotangaza mgao wa umeme hawajiuzulu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini waliotangaza mgao wa umeme hawajiuzulu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmaroroi, Mar 27, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wizara ya Nishati na Madini pamoja na TANESCO wameshindwa kuzuia mgao wa umeme kama Rais alivyoahidi kuwa mgao wa umeme utakuwa historia.Ni hivi karibuni tu imetolewa tishio la mgao wa umeme baada ya kupingwa kwa ununuzi wa mitambo ya kufua umeme ya Dowans.Sasa kama wahusika hawataki kujiuzulu kwa kushindwa kazi na hawawajibishwi na mamalaka hususika je kuna anayewalinda? na kama yupo ni kwa manufaa ya nani?
   
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Na kwa nini wajiuzulu? kwani wamedanganya waliposema kuna upungufu wa umeme? kabla hamja wakurupukia kujiuzulu, mjiulize, Jee, mmewawezesha kununuwa mitambo mingine?

  Tunasikia kuwa Tanesco kwa miaka kadhaa ni shirika linalopata hasara, na hivi majuzi tu, toka ashike Dr. Rashid, tumesikia kuwa wanategemea kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu kuonyesha faida kwenye shughuli zao.

  Sasa, shirika linalopata hasara, na umemweka mtu aliweke sawa, halina fedha, yule Dr. Rashid kaonyesha kuwa anaweza kwa kuwa ameanza kulitowa kwenye hasara na kulielekeza kwenye faida, unasema ajiuzulu, sasa akisha jiuzulu, huyo anaekuja si itabidi umuwezeshe?

  Dr. Rashid alisha jiuzulu zamani (mwaka jana) au mmesahau? akaombwa arudi kuliokowa shirika, sasa hata siwaelewi wa Tanzania. Mbona mnaburuzwa-buruzwa bila kufikiri?

  Kasema, inunuweni hii mitambo ya Dowans, mkamuona mjinga! sasa nani ni mjinga? ni wale ambao wana mitambo ipo kwao, imeshajaribiwa na inafanya kazi lakini kwa siasa za kijinga waamuwa izimwe au wale wanaotaka inunuliwe watu waondoke kwenye adha ya umeme?

  Hebu pigeni hesabu, ni hasara ngapi tunayoipata kwa kutokuwa na umeme kwa masaa 8 kila siku?

  Mitambo ya Dowans waliofanya madudu ni wala rushwa na si Dowans. Waliokula rushwa wanajulikana na waliotowa rushwa wanajulikana! Jee, Dowans wamefanya makosa kuununuwa ule mkataba na kuanza kuzalisha umeme? ni kosa gani hapo?

  Dowans wameona madudu waliyofanya Richmond, wakaona hii ni business opportunity waka negotiate deal nzuri wakanunuwa ule mkataba na mitambo, wanataka kuzalisha wafanye biashara zao, mnawaletea za kuleta, wanataka kuwauzia kama kukodisha hamtaki, bado mnawaletea za kuleta.

  Hivi tuna nini? hatuwezi hata kufikiri mambo madogo kama haya, hesabu ndogo tu zinatushinda?


  Iwe isiwe, mitambo itanunuliwa, kwa nini isinunuliwe ambayo tayari ipo hapa na imeshafungwa na ingojwe mingine ambayo hatujuwi lini itanunuliwa, lini itafika, looh!

  Ama kweli yule aliesema tuliwahi kutaka kujitawala hajakosea, ndio maana leo karibu miaka hamsini, maji safi hatuna mabombani, umeme hatuna, taka kila upande, vyoo vinafurika mabarabarani na kunuka hovyo na hakuna anaeweza kutatuwa.

  Kwa ufupi kila kitu hakituendei sawa, jee tumeshajiuliza kwa nini? jibu dogo tu! hatuna akili! ujanja ni wa maneno tu si wa vitendo. Na tutasema, mpaka tutadata, kama hatutotumia akili za kujuwa lipi lina faida na lipi halina, tutabaki hivi hivi mpaka vitukuu vyetu, labda.
   
 3. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hatutaridhika na kujiuzulu tu inabibi tufike mahali na kuwashitaki watu kama hawa kwa kuhujumu uchumi na mauaji mahospitalini kwa uzembe wao.Ikiwezekana tuwapeleke The hague.
   
 4. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  DAR ES SALAAM umeeleza vizuri sana japo utaonekana unamtetea Dr. Rashid. Kila mtu ana akili yake na upeo wa kufahamu na kufafanuwa jambo aonavyo sawa kwake. Lakini hali halisi ni kama ulivyoeleza.
   
 5. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ...Wizi mtupu.
  Tangu mwaka 2007 hao tanesco waliipigia hesabu mitambo ya dowans tu?? hawakuweza kutafuta altenative nyingine for time being kwa kujua kwamba wanajukumu la kutupatia huduma ya umeme ya uhakika?

  Toka lini ukafanyia procurement ya mitambo ya kijambazi kama ya RICHMOND? unajua endapo dowans wangekuja na kuwekeza kwa mitambo yao mipya kwa utaratibu unaoeleweka baada ya kung'olewa ya richimonduli hapo tusingewanyooshea vidole (NINYI), Wamenunua mitambo iliyoletwa mahsusi kiujanjaujanja kutuibia halafu leo tuamini kwamba hawa jamaa ambao hata hawajulikani ni nani eti tununue mitambo?? labda tuwe wehu kweli ndipo tutakubaliana na upuuzi wa kuinunua.

  Kwani kwa kunua hiyo midowans ndiyo itakuwa suluhu ya matatizo ya umeme? maana hata ilipokuwepo bado huduma ya tanesco ni mbofu mbofu mbofu, tunataka solution ya uhakika na si wapiga filimbi wa hamelin hapa. Pia mheshimiwa Daslam sisi hatuburuzwi na siasa la hasha tunaburzwa na kiu ya maendeleo hasa kuboresha hali halisi ya sasa kwa ajili ya vizazi vijavyo.

  Kwa heshima tu nilidhani Ngeleja angekuwa honestly kuachia ngazi na pia MAMLAKA ya juu ingemuwajibisha Dr. Idrisa. hataka kama alikataliwa kujiuzulu lakini ameprove failure kwa hili. Haiwezekani haikubaliki na HAKUNA KULALA.

  Wizi mtupu hakuna jipya.

  Wezi wa mali ya umma msio na huruma jaribuni utu basi hata kidogo....
   
 6. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Sasa huyo Rashid kama hana maslahi anasubiri nini kama hawezeshwi,hakuwepo TANESCO tangu 2007,halafu suluhisho la mgao wa umeme ni mitambo mitumba ya Dowans pekee?
   
 7. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #7
  Mar 31, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kweli haya ni maswali magumu sana.Wapo viongozi wengi wa aina hiyo .Wapo akina Masha,Mkulo nk.Wapo tu, wanafurunda na wanaendelea.Sielewi hatma ya mambo haya ni nini.


  MUNGU AIREHEMU TANZANIA NA WATU WAKE LAKINI MAFISADI AWAFUTILIE MBALI
   
 8. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #8
  Mar 31, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wanahusika na mgao wa umeme wajiuzulu kama hawana njia nyingine ya kunusuru mgao huo isipokuwa kwa kununua mitambo mtumba ya Dowans.
   
 9. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #9
  Mar 31, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wahusika wa TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini wangekuwa wanafanya mchakato wa kutafishwa kwa mitambo ya Dowans na Serikali kwa kuwa ilidanganywa na Richmond katika mkataba na si kuyapigia debe yanunuliwe.
   
 10. M

  Mkereme JF-Expert Member

  #10
  Mar 31, 2009
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 251
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wanakijiji Jambo usilolijua ni usiku wa kiza. Hii forum isitumike kueleza ujinga! Ni busara ya kawaida kama kitu hukijui usikiongelee unaonyesha jinzi ulivyo mpumbavu. Dar es salaam anasema Dr.Idris kaleta nafuu Tanesco asijikrupukie kama mlevi. Onyo kwake na wenzake mafisadi. TANESCO imekuwa ikitengeneza hasara kubwa walipoanza kulipa Capacity CHARGE ya IPTL mwaka 2000 ilikuwa ni Dola milioni moja na nusu kwa mwezi na iliyobakia alikuwa akilipa Mramba kama ruzuku mpaka alipoondoka Mkapa 2005. Hasara iliongezewa na ujio wa SONGAS waanze kuzalisha umeme TAKWIMU ZIPO. Hata JaKaya Kikwete au OBAMA akiwa MkURUGENZI wa TANESCO hasara itakuwepo mpaka MIKATABA hiyo mibovu imevunjwa. Kwa faida yenu narudia Dr. Idris amekuwa akiendesha shirika kwa ule mkopo wa Shilingi Bilioni mia tatu (300Bn/=)alizokopa kutoka mabenki ya hapa TANZANIA hakuna cha faida Deni la IPTL halipi hata hivyo pesa alizookoa Iptl ZINAKOMBWA NA akina Dowans;NA songas!!!! ni mwendo mdundo wa hasara. Mdundiko wa Kikwere utapamba moto kwenye kuzilpa hilo deni na riba nasikia karibuni wanaanza kuzilipa haki ya Mungu hilo ni deni la TAIFA . UKITAKA HADIDU ZA REJEA GO BACK TO MY PREVIOUS THREADS ON THE SUBJECT MATTER @ REJEENI POSTS ZANGU ZA HUKO NYUMA. aCHENI HIZO ni wizi mtupu. NARUDIA MGAO HAUNA UHUSIANO NA DOWANS NI MATATIZO YA KIMIUNDOMBINU YA KURIDHI wengi wa wanAforum sio watambuzi HATA ukiwaeleza hawawezi kuelewa ubishi mtupu!! TATIZO la wa-TZ hawataki kusoma lazima wachotewe kwa kijiko ndio maana hata mgao hawahoji kwani si walizoea tangu enzi za ugawaji!!!!
   
 11. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #11
  Mar 31, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wengine wana maslahi binafsi,mimi nashauri hatakama unafaidi matunda ya ufisadi ionee huruma nchi yako na watu wake ambao wengi ni wa kipato cha chini.
   
 12. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #12
  Mar 31, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Rashid yuko pale aiwezeshe Tanesco ilyokuwa hoi bin taabani, sasa kama unataka Rashid aliwezeshe shirika lisilo jiweza, yeye katoa rai yake, mitambo iliyokuwepo uani kwao, imeshafungwa, imekaa bure inunuliwe! hilo ndilo wazo lake. Jee kakosea hapo?

  Hiyo mitambo inajulikana wazi kabisa ni nani na nani waliofanya madudu katika mkataba wao na Richmond, Jee Rashid alikuwepo wakati huo? au aliletwa yeye baada ya huo upuuzi kutokea? nadhani jibu unalo.

  Ukija upande wa Dowans, ni simpo, Dowans ni wafanya biashara, wameona kuna tatizo la mikataba kati ya Richmond na Serikali au Tanesco? utajaza mwenyewe! Dowans akapiga hesabu akauliza kwa wanaohusika, jee nikinunuwa hizi machine ntapewa mkataba mpya? wanaohusika wakamwambia ahlan wasahlan, nunuwa na tutakupa mkataba mpya, kafanya hivyo, wamemgeukia! alaa! Dowans kaenda kushitaki kwenye mataifa yenye uzoefu wa biashara zaidi yetu, kafunguwa kesi, mitambo imesimamishwa bure, si Dowans si wananchi wa Tanzania wanaofaidika. Hasara zaidi anapata nani? piga hesabu ndogo tuu. jumlisha masaa 8 ya kutozalisha kwa siku kwa sasa mpaka utakapo solve hii problem, jawabu utayopata tazama bei ya hiyo mitambo chakavu, ukiona wapi unapata faida au wapi unapata hasara basi huko ndio uelekee.

  Zaidi ya hapo hakuna, kama mitambo ya umeme ya zamani tushanunulishwa kwa nguvu na mahakama, IPTL, au mmesahau? na hii sasa itajirudia! mitambo imekaa bure, tutakuja kuilipia Dowans akishinda kesi (tuombe Mungu Dowans asishinde kesi, Mungu sijui atasikia dua yetu? maana serikali yetu haina dini!) na kuitumia hatujaitumia, mwisho wake ni nini? hasara juu ya hasara.

  Rashid ni msomi, kabla hajatowa hayo maamuzi kisha ziita kampuni za kimataifa kutathmini hiyo mitambo (technically na financially) na ushauri waliotowa inafaa.

  Hivi sisi tuna matatizo gani jamani? jibu, hatuna akili! tunachojuwa ni kulalama tu, na ndio maana mpaka leo, tu masikini wa kutupwa na utajiri usio na kifani tunao hapa hapa!
   
Loading...