pambe samanini
JF-Expert Member
- Oct 27, 2015
- 368
- 169
Tokea enzi za ukabaila historia inaeleza ndiko wakati watu walianza kulipa kodi. Tokea enzi hizo hadi ukoloni na baada ya ukoloni watu walilipa kodi kodi zilikuwa nyingi mfano, kodi ya kichwa, mifugo, vitu, mazao, nk ni baadhi ya kodi ambazo waafrika wengi walilipa.
Hata hivyo baada ya Uhuru hasa 1990s baadhi ya nchi za Africa zilikuwa baadhi ya kodi kwa kigezo cha kero kwa wananchi, kodi hizo zilizoitwa kero ni kodi ya kichwa, mifugo, baiskeli, nk kwa lengo la kuondosha kero kwa wananchi. Pamoja na kodi hizo kuwa kero kwa wananchi inasemekana ulikuwa mtaji wa kisiasa hasa kwa vyama tawala na watu wake wakihofia vyama vya upizani kunyakua dola kwa mwanya huo. Miswada mbalimbali ya kuondosha kodi kero ilipelekwa bungeni na kila kila mbunge alijaribu kuonesha umaarufu na weledi wake juu ya hili.
Kwa ufinyu wa fikra za waafrika walidhani wametua mizigo yao bila kujua kuwa mizigo yao imehamishiwa sehemu nyingine tena ndiyo kuzito kushinda kwa awali. Bidhaa zikapanda bei mfano sukari, nguo, dawa za watu na mifugo, hata jembe la mkono likawa juu nk . Weledi wa waafrika hawakujua kuwa kuna direct tax and indirect tax hapo ndiyo wakapagawa na kutoa kura nyingi za ndiyo kwa vyama tawala.
Baada ya mataifa yaliyoendelea kuanza kupunguza misaada kwenye bajeti ya nchi za kiafrika kutokana na bajeti kuwa tegemezi na madeni kuongezeka hali ambayo ilipelekea mataifa ya afrika kushindwa kulipa mataifa yaliyoendelea yakapunguza misaada kwa mataifa haya hapo ndipo waafrika tulipozinduka na kuanza kuhamasisha kulipa kodi.
Watawala wengi wa kiafrika wameshindwa kuleta maendeleo nchini mwao kutokana na wananchi wao kuwapumbaza wasilipe kodi, wananchi wamezoea kutolipa kodi halafu wanaleta sheria asiyedai risiti adhabu ya kifungo au pesa. Hivi hawa hawakumbuki ujinga walitupa wao wenyewe kwa kusaka kura zetu? Kama walipiga kampeni ya kafuta kodi na wakaweza kwa mbwembwe zote bila kutuuliza wananchi kama kodi hizo zilikuwa kero, pia wameona nini tena kurudisha kodi walioziita kero na kuwaaminisha hivyo wananchi wao?
Bahati mbaya kabisa wakaao bungeni ndiyo wakaidi wa Kwanza kulipa kodi kwenye mishahala yao na ndiyo wanataka wananchi wafuate nyayo zao, huu nao ni ulevi na majipu dume. Kama marais wa wa afrika walisema kodi ndogo ndogo ni kero kwa wananchi kwa nini tena wanahimiza kulipa kodi. Hapa watuambie kodi ipi na kwa mtaji upi ilipwe nk?
Kwa nini walifuta kodi, na sasa wanaleta kodi walizoziita kero?