Kwa nini wakimbizi wanaishi kwa mateso hivi?

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,504
2,000
Juzi nimetembelea Kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu iliyoko mkoani Kigoma na nilipata Fursa ya kuzungumza na wakimbizi hao juu ya hali halisi ya maisha yao kwa ujmla. kiukweli hali inasikitisha na nayashangaa mashirika ya kitaifa na kimataifa yalijazana humo ndani huku faida yao kuwepo humo ikiwa ni ndogo kabisa.

Kuhusu chakula

kila mkimbizi hupewa Kilo nane za unga kila baaada ya mwezi. Fikiria unapewa kilo nane za unga unatakiwa uzitumie ndani ya mwezi mzima.

Kila mkimbizi hupewa sabuni Moja kila baada ya mwezi.

Hiyo ni mifano tu. na ikumbukwe kuwa wakiwa kambini hawaruhusiwi kujishughulisha na shughuli za kilimo kambini.

je kwa hali hiyo ya maisha jamani serikali iingilie kati iyabane mashirika na. nchi wahisani kuongeza misaada zaidi kwa wakimbizi hawa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom