mnyikungu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2009
- 1,960
- 2,464
wandugu, MKWAWA ni mtu mhimu sana kama alama ya ushujaa wakweli na utetezi wa mwafrika dhidi ya ukoloni, mtu huyu enzi zake aliogopwa mno. utawala wake ni moja kati ya tawala pekee zilizopigana na mjerumani na kumshinda.aliwafanya wahehe wajurikane kama the most powerful military people in German East Africa.ni mtu huyu pekee africa aliyekataa kulipa kodi kwa mkoloni na badala yake ni yeye ndiye aliyetaka alipwe kodi na wajerumani.najua hstoria yetu imeandikwa na wazungu na ndiyo maana vitabu vyetu vya historia havimuelezei kiundani mtu huyu kwani ni aibu kwao, ni huyu ambaye kifo chake kimejaa utata, wajerumani wanaamini alijiua na wao walimkata kichwa japo wengi hatuamini hivyo, fikra kubwa aliyokuwa nayo ni kwamba hata baada ya kifo chake hakupenda maiti yake iguswe na wazungu hivyo alikoka moto na kujipiga risasi mwili wake ukaangukia kwenye moto na kuteketea kabisa, hivyo hata kama walipata kichwa basi hakikuwa chake ila cha moja kati ya wafuasi wake. hiyo ni moja kati ya dhana zinazobishaniwa uheheni kwani wengine wanaamini alijidumbukiza mto kikombo na kupotea na wengine wanaamin aliendakujificha mapangoni na kufia huko. huyu mtu ni shujaa kweli! lakini kinachonishangaza mtu huyu kamwe haenziwi ipasavyo, wahehe wa leo utadhani hakuwa chifu wao na tanzania pia nayo imemsahau mtu huyu, mi nafikiri vya kale ni dhahabu apewe heshima yake kama inavyostahili maana huyu ndiyo kioo cha ushujaa wetu. hebu ona alivyopambana nao
(Lt. Tettenborn believed that if it had not been for the death of a large number of Wahehe chiefs, Mkwawa incorrectly included, no one would have survived. Saving the main 'part of the baggage' is also incorrect, it was not saved. Zelewski had started with 13 Europeans, some 320 Askaris, 170 porters, machine guns, and field artillery. Of these ten Europeans, 256 Askaris, and 96 porters had been lost. The German defeat made a truly enormous impression and the Hehe had now gained reputation as the most powerful military people in German East Africa and the Schutztruppe was no longer in a position to continue attacking the Wahehe.) kwa jeshi lenye vifaa kama hili alilopigana nalo mkwawa na akalishinda je ni kweli hastahili heshima?