Nimeona nilete hii habari tuijadili wote wanajamii.Nilifurahi sana kwa kitendo cha kizalendo cha waziri wetu alipohutubia na kukerwa na kitendo cha Wahandisi wetu kuangusha Majengo.Mimi kutokana uewelewa wangu mdogo nilikuwa na machache ya kuongea.Fani ya uhandisi hapa nchini naona hatuko makini,naona siasa inaanza kuingizwa kwenye hii fani.Kwanza kuna Vyuo vingi vimeanzishwa hapa nchini kwa sasa vinavyotoa taaluma hii ya Uhandisi-shahada ya kwanza,hili ni jambo zuri kuongeza wahandisi nchini.Je bodi ya Wahandisi wameliona hilo?Kuna hizi shahada za Uhandisi shahada ya kwanza wanaziita Everning program nadhani na baadaye tutaanzisha shahada ya kwanza pale Muhimbili ya medicine everning program. Bodi ya uhandisi hapa nchini ina wasomi waliobobea kwenye hii fani.Wasipokuwa makini lawama za wahandisi kuangusha majengo zitawaelekea wao.Bodii waweke standard kupata wahandisi mahiri na si kwa sababu kaleta shahada yake sijui kutoka chuo gani halafu wewe unampa usajili hapohapo.Mimi naishia hapo,nakaribisha wachangia hoja karibuni.