Kwa nini wachache wajifungie Ikulu kujadili maslahi yetu hiyo ndio Demokrasia yetu Tanzania?

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
46,892
32,308
wanabodi,
imekuwa kama fasheni sasa kwa viongozi wa vyama vya upinzani chini kukutana na Rais Jakaya Kikwete Ikulu ya Dar es Salaam.

Wanaomba appointment Ikulu, wakisharuhusiwa wanakwenda kuzumgumza na Rais kisha wanapiga picha za pamoja na kuondoka, hapo tunaambiwa wanajadili sheria ya mabadiliko ya katiba.

Haya yalianzishwa na Chadema ambao walipinga muswada wa katiba mara mbili mwishoni mwa mwaka jana, chama hicho kilisusia mjadala wa katiba bungeni huku wabunge wake na wakiwemo baadhi ya wabunge wa NCCR Mageuzi, wakitoka nje ya ukumbi wa wabunge kuashria msimamo wao.

Baada ya bunge kumaliza mjadala wao, Chadema wakaomba kukutana na Rais Kikwete Ikulu, kujadili kile walichokuwa wakikipinga mkutano ukafanyika kwa muda wa siku mbili, walipomaliza Rais akausaini muswada waliokuwa wakiupinga Chadema ukawa sheria.

CUF nacho kikaomba appointment ya kumuona Rais, pamaja na kwamba chama hicho hakikususia mjadala wa shera ya mabadiliko ya katiba bado kikaenda kumuona Rais, sijui walimtaka Rais afanyaje wakati walishakubalina kila kitu bungeni.

NCCR Mageuzi nacho kikaomba appointment kwa Rais ili kutimiza wajibu wake, wamejadiliana walichojadili wakamaliza na kupiga picha na Rais Ikulu.

Mazungumzo ya Chadema yakajirudia safari hii na Slaa, nae alikuwepo, kitu cha kujiuliza hivi haya mazungumzo wananchi wameshilikishwa au na ni mawazo ya viongozi wa nyama vya siasa, tukumbuke kuwa kuna wananchi wasiokuwa na uanachama wa chama chochote, hao nao wanawakilishwa na nani Ikulu?

Kwa nini hivyo vikao vya katiba kama vinawakilisha mawazo ya wananchi visitangazwe moja kwa moja na televisheni ili angalau wananchi wasikie kilichojadiliwa? katiba hii sio ya Rais au vyama vya siasa, ni yetu sote.

Kwa nini wachache wajifungie Ikulu kujadili mustakabali wa maisha yetu???
 
Baba wanafukuzia kushikana mkono na JK na kupiga picha ya pamoja waipeleke kwa Cameroon aidi kuwamwagia mshiko
 
Mkuu ni kweli umenikumbusha. Nasikia CCM ina wanachama kama millioni 4 na vyama vingine kwa ujumla wao vina wanachama kama millioni 3 n. a watanzania yupo zaidi ya millioni 47. Kwa hiyo hao jamaa wanawakilisha watu kama millioni 7 na wengine millioni 40 hawana uwakilishi wa kwenda Ikulu! Mimi ni mmoja wao. Nami nitaomba appointment
 
Mkuu, kweli bana na haya makundi mengine kama Walemavu,Waandishi wa habari, Wakulima, Wafanya biashara, Wazee, siju hawa nao watawakilishwa na nani IKULU:A S-coffee:
 
Napata hisia mtoa mada unataka kupotosha ukweli. hadi tunaambiwa Marekebisho ya sheria husika yatapelekwa katika bunge lijalo na kwamba mabadiliko hayo yatakuwa makubwa.
ingekuwa vema kama ungemlaumu spika wa bunge kwa kutosikiliza mawazo ya kambi rasmi ya upinzani!! matokeo yake Wabunge wanafanya kazi moja mara mbili.... hii yote ni matumizi mabaya ya fedha ya umma na kithibitisho kwamba spika hana uwezo wa kuongoza Bunge kwani kaliingiza taifa kwenye hasara isiyokuwa ya lazima!!
 
Najua Ritz ni mrengo wa CCM, ila leo ameongea hoja muhimu sana.
Swala la kujifungia ikulu na kuona picha bila matukio hasa ya sababu na kilichojadiliwa inatia shaka. katiba ni kwa ajili ya watanzania wote. Wanasiasa wanamaslahi yao na sisi wafanyabiashara, wafanyakazi, dini, wafugaji, wakulima wasomi na wasiosoma, wazima na walemavu tunayetu. Je Makundi yanayokutana na Raisi yameunganisha haya makundi yote na mawazo yote ya wananchi?

Tusipokuwa makini tutapata katiba ya kisiasa zaidi badala ya kitaifa.
Nataka wachumi, wafanyabiashara, wafanyakazi, nk nao watoae maoni yao.
 
Mimi nilishalisema hapa jambo hili nikambiwa mimi gamba!

Sasa subirini kuchuuzwa! Kisa kahawa ya ikulu
 
Eti great thinker katoa maoni yake.......Napita hapa sio pangu. People might not see the difference
 
Back
Top Bottom