Kwa nini wabunge wa CCM na Nape wanawakana wanafunzi wa vyuo vikuu

Tuko

JF-Expert Member
Jul 29, 2010
11,178
7,319
Mara kadhaa tumesikia kauli za wabunge wa CCM 'wakiwaasa' wanafunzi wa vyuo vikuu wasijihusishe na siasa mavyuoni. Kauli kama hizi pia zimekuwa zikitolewa na viongozi mbalimbali akiwepo Nape, na Spika Makinda.

Kuna swali najiuliza; Why now?

Hivi sio CCM iliyowatumia vijana wa vyuo vikuu kuzungusha form ya urais ya Kikwete mikoani kutafuta wadhamini?
Hivi sio CCM imekuwa ikiwakusanya kwa mamia kwenye mabasi kuwapeleka kwenye kumbi mbalimbali kuwapa kadi?

Ni nini kimebadilika kwenye hiyo "memorandum of understanding" yao, na sasa CCM hawataki kusikia Vijana wa vyuo vikuu wanajihusissha na vyoma vya siasa?
Au CCM wameshindwa kwenda sambamba na Lema, wanaanza kuomba mbio ziishe kabla ya kumaliza round?

Je, kwa msimamo wao wa kuwataka wanavyuo wasijihusishe na siasa, CCM wanataka kusema hawataki tena support yao kama ilivyokuwa kwa wafanyakazi?

Je, kwa msimamo wao CCM wanataka kusema uongozi wa wanafunzi wa CCM na wanachama wao (kama wale waliocheza football match na kina Nape), kwa sasa they are useless?

Najiuliza tu...
 
Huwezi kukataza siasa vyuoni manake hapo ndipo fikra mbadala zinatengenezwa kwa ajili ya ustawi wa jamii.,ni wenye akili mgando tu na wasiotaka changamoto zozote ndio wanaona taabu kwa wanavyuo hasa wasiposapoti vyama vyao..,CCM walitaka kuifanya UDOM ngome yao tatizo vijana wakashtuka japo it was a bit late...
 
Hii nchi bila unafiki wa viongozi wa ccm waliotufikisha hapa tulipo itaendelea lkn tukiwaacha watumie raslimalii za taifa kwa manufaa yao sio ya watz basi imekula kwetu.................saaizi hatuna kiongozi tena nchi ipoipo tu
 
Ni haki ya msingi kwa kila binadamu kuchagua anavyotaka kuishi

lakini hata hivyo chuo kikuu sio level ya elimu ya mtu kuambia anachanga mambo (siasa) na shule na wale wa political science intakuwaje?
 
CCM ni sikio la kufa..... ni hao hao CCM waliokuwa wanapita na kugawa kadi kwa wanafunzi wa vyuo, yaani wanajikanganya hadi basi.......
 
Back
Top Bottom