Kwa nini waalimu wanadharaulika? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini waalimu wanadharaulika?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Msongoru, May 15, 2009.

 1. Msongoru

  Msongoru JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  wajameni, nimejaribu kufikia kwa muda mrefu kidogo sababu inayopelekea waalimu wetu (hasa wa shule za msingi) kudharaulika. Nimeshindwa kujua ni kwa nini waalimu wanaonekana kama watu wasio na hadhi kubwa kwa jamii yetu? Wamepewa majina tofauti na hata wakati mwingine utasikia "una nguo moja kama mwalimu!" au "uso umekupauka kama mwalimu"

  Serikali nayo kwa upande wake, inawaona sijui kama nini! Mishahara yao na wajibu wao kwa jamii haulingani. Hivi tatizo ni nini hasa?
   
 2. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kweli kabisa wanadharaulika sana tena mno utakuta mzazi anamwambia mwanae umekosa vyuo vyote umeshindwa hata kwenda ualimu? Inaonyesha ni kazi ya watu wa hali ya chini na ndo maana mishahala yao ipo chini hata ukiwa na degree utaambulia mshahala kiduchu sana.Ni taaluma inayo dharauliwa sana kuanzia serikalini mpaka kwenye jamii.
  Kitu kingine walimu wenyewe wamekuwa wapole mno kudai haki zao za msingi wao wapo wengi sana wanaweza goma au kushinikiza serikali kuwalipa vizuri.
   
 3. Komamanga

  Komamanga JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2009
  Joined: May 2, 2009
  Messages: 221
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  heheheh....kweli hizi ni dharau sanaaa wakati bila ya walimu sasa hivi kusingekuwa na viongozi
   
 4. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #4
  May 16, 2009
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0

  Nimesoma post ingine hapo kuwa walimu wa Temeke na Rombo hawajalipwa mishahara kwa mwaka mmoja !!!!! Hivi kweli ni haki !!! unategemea huyu mtu anaishi vipi!!, Kweli wacha waandamane wakalale Ikulu ili Kikwete naye awaone.

  Mod ikiwezekana mkaziunga na ile post ya walimu kutolipwa kwa mwaka mmoja italeta maana kidogo.
   
 5. I

  Ikena JF-Expert Member

  #5
  May 28, 2009
  Joined: Oct 24, 2007
  Messages: 482
  Likes Received: 247
  Trophy Points: 60
  I'm happy that I'm a teacher.I would rather be a teacher than a salesman.Although a salesman makes a lot, more than I do, I would not change places within him, for he sells machines, fountain pens and other materials but I sell IDEAS. I would rather be a teacher than a Stenographer. For she helps write letters but I help to write CAREERS. She touches keys but I touch LIVES. I would rather be a teacher than Architect. For an architect helps to buld edifieces but I help to build CHARACTERS. Edifices endure for a time but character endures throughtout ETERNITY. I would rather be a teacher than an Artist. For an artist paint good pictures on walls and canvas but I paint pictures on the MEMORIES OF THE YOUTH. An artist makes impressions on tablets of clay but i make impression on the tablets of the SOUL. I would rather be a teacher than a book-keeper. For a book-keeper balances accounts but I balance LIVES. I would rather be a teacher than a great business,executive. For he works with facts and figures and lifeless coins, but I work with MINDS that open, FUTURES that unfold and PRINCIPLES that grow. I would rather be a teacher than a musician. For he plays on strings of violin and piano, but I play on HEART STRINGS. I would rather be a teacher than an orator. For he stirs adults to applause and admiration but I stir the YOUTH to RIGHT choosing and NOBLE THINKING. I would rather be a teacher than a potter. For he shapes vessels of clay but I shape DESTINIES. I would rather be a teacher than an archaelogist. For he unearths buried treasure, but I unearth TALENT. I would rather be a teacher than a scientist, for though he studies the wonders of rocks and beauty stars, and the miracle of plants and glory of the skies; I deal with that which is still more miraculous in throbbing human HEARTS unfolding human LIVES and the formation of life time CHARACTER which makes a man to be a MASTER OF HIS DISTINIES.
   
 6. c

  chatts New Member

  #6
  May 28, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kudharauliwa kwa waalimu ni kutokana na kurithi mfumo wa enzi za mwalimu, maana enzi hizo mtu aliyekuwa amefeli kidato cha nne alipelekwa chuo cha ualimu. Sasa jiulize kama ualimu ilikuwa ni kazi ya waliofeli ni nani ataiheshimu? Ndio maana hata serikali haina muda hata wa kufikiria juu ya mishahara yao kwani ilijengeka hivyo tangu enzi za mwalimu
   
 7. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #7
  May 28, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  waalimu wa shule za umma/serikali ndiyo wanadharaulika... kutokana na kushindwa kwa serikali kuwekeza kwenye miundombinu ya Elimu hasa ya msingii.Ukiangalia shule za binafsi waalimu wanawajali na kuwapa stahiki/stahili zao na ndiyo maana shule hizo hata ziwe za msingi zinaweza kuvuta hata wahitimu wa chuo kikuu.
   
 8. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #8
  May 28, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Mwalimu ni kibao kielekezacho.
  Faida ya kibao kielekezacho mtaa,njia ua uelekeo wowote ni wakati ule ti kihitajikapo kuelekeza. Ukijua kule uendako huhitaji kuelekezwa. Faida ya kibao kile ni nini?

  Nilirudi kule niliko soma shule ya msingi miaka 30 iliyo pita nikakuta kibao au ukuta tulio jenga miaka ile bado upo unasomeka vile vile.

  Nilisimama kuungalia ukuta ule na maandishi yale tu kwa kukumbuka miaka iliyopita lakini si kwa kukipa heshima kibao kile.
  Nilijua wapi niendako, sikuhitaji kuelekezwa,kibao cha kuelekeza ulekeo wa shule au jina la shule cha nini kwangu?
  Nikisha jua kusoma na kuandika sihitaji tena kujifunza kusoma na kuandika mwalimu wa masomo hayo ana faida gani kwangu?
  Nikipata elimu ya Chuo kikuu nini faida ya mwalimu wangu wa UPE aliyenifundisha kwa bidii zake zote??
  Mwalimu habadiliki kwa mfano wa kibao kilekezacho kisivyobadilika.
  MWalimu ni mwanafunzi wa kudumu.
  MWalimu huendelea kujifunza na kufundisha kwa uvumilivu wote.
  Malipo halisi ya mwalimu si mshahara wa shilingi bali ni furaha ya mafanikio ya wanafunzi wake.
  Mwalimu halisi hufundisha kwa wito na mvuto na si kwa faida ipimwayo na uwingi wa fedha.

  Sisi tuliofundishwa na walimu walio sawa na vibao vielekezavyo ndiyo tubadilikao kutoka katika hali tete na ya ujinga hadi na kufikia kupata maarifa mengi ya hali ya juu na kukosa nidhamu hata kudiriki kusahau njia tuliyopitia.

  Walimu wamesahaulika na sisi wote kabisa siyo serikali tu.
  Wanafunzi tukiwakumbuka na kuwaenzi walimu katika maisha yao ya kila siku watasahaulikaje.
  Nani mwenye cheo kikbwa sana hapa Tanzania liyefika hapo alipo hakukunjwa akingali mbichi na walimu na kupewa ujanja wote alionao??
  Sisi wanafunzi tumejaa dharau kubwa na kiburi hii ndiyo asili ya walimu kudharauliwa.

  Watu wengi tunachukia kwenda tuliko soma, wale wa umri wangu na zaidi wanadai maeneo ya shule yanawakumbusha mboko walizo rambwa enzi zile hadi kutoa mchozi mbele ya ndito zao( washikaji).
  wengine waliichukia shule kwa ujumla.
  Wengine walikuwa nachuki biafasi na walimu wao.

  Tumesahau walimu kwa sababu tulichotaka walisha tupa siku nyingi.
  Ganda la muwa likisha fyonzwa usukari wake wote linafaa nini? Linafaa kuliwa tena?
   
 9. M

  Mama KK New Member

  #9
  Mar 1, 2010
  Joined: Jul 17, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku hizi kila mtu anatafuta njia ya kuchuma hela haraka, na kazi ya mwalimu ni ya kujivuniya lakini hailipi vizuri. Kwa hiyo kuwa mwalimu ni kazi ya mwisho mtu atataka kuchagua kwa sababu ya malipo. Lakini hawajui kwamba kila mmoja anahitaji mwalimu kumsaidia kupanda ngazi ya maendeleo yake. Bila mwalimu mwanafunzi ataweza wapi kumaliza shule? Wazungu walisema ' I am a Teacher I Touch the Future'. Kwahiyo ndugu usisononeke na hilo kwani kuna binadamu ambaye alimaliza elimu yake bila ya msaada wa mwalimu?????
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Msongoru
  Nafikiri umeuliza swali la msingi sana kuhusu hali ya walimu nchini Tanzania. Kuna vitu kadhaa hapa vya kujiuliza, wakati wa Nyerere aliweka wazi kabisa kwamba ualimu ni wito, lakini sote tuliona ni kwa kiasi gani Mwalimu alikuwa anaonekana ana thamani kumshinda mtumishi mwingine yeyote wa serikali. Pale vichaa walipochukua nchi na kuanza kumwona mwalimu ndo wa kumpunja mafao, mwalimu ndo wa kumcheleweshea mishahara, mwalimu ni profession unayoweza kusoma kwa miezi mitatu, ualimu ni profession unayoweza kusomea hata kama utakuwa na zero kama ambavyo ilifanyika wakati wa kuanza ule mpango wa MMES and the like ndipo hapo watu wanapojifunza kwamba kumbe hata fulani, kilaza kabisa na yeye amekuwa mwalimu, basi ualimu ni profession ya kila mtu hata mbumbu tu. Hapo ndipo tulipoanzia.

  Na pengine kitu ambacho kinawafanya walimu waendelee kuonekana wapuuzi na waliokosa mwelekeo ni ulimbukeni mkubwa walionao, wa kutokuwa tayari kushirikiana kudai kilicho chao. Wanakubaliana wote tugome, lakini utasikia Mtwara walimu waliendelea kufundisha kama kawaida. Sasa hicho ni nini? Yaani walimu watadharaulika hata zaidi ya hivi wanavyodharaulika sasa. Kwa kuwa hawana umoja na wala hawana mpango wa kufuatilia na kujua haki zao kama raia wa tanzania na kama wafanyakazi. Hivi unamlipa mwalimu shilingi l50,000 hapo anaishi Dar, amepanga nyumba, ana watoto wanasoma na anahitaji chakula. Unategemea nini? Na bado wakati wa kampeni watageuzwa mabango ya CCM au ndiyo waandikishaji wa wapiga kura au wahesabiaji wa kura za CCM na watakuwa mstari wa mbele kupiga makofi kuwashangilia haohao wanaowafanya waishi maisha hayo wanayoishi.

  Sisi walimu ni Wehu
  . Nikiwemo na mimi mwenyewe ambaye pia ni Mwalimu. Somewhere I read an article somebody wrote: "Ualimu Tanzania, ni headache??" Huwa napenda sometime kuexplore mambo ya elimu na huwa navutiwa kusoma issue zinazohusu elimu kutoka kwenye blog hii inayoitwa Elimu ya Tanzania na Mustakabli wa Taifa. Mnaweza kutembelea hapa: http://vangidunda.blogspot.com/2010/02/ualimu-tanzania-ni-headache.html muone jamaa anavyokomend kuhusu ualimu Tanzania, na Elimu ya Tanzania kwa ujumla.
  Regards
   
 11. h

  hilbajojo2009 Member

  #11
  Mar 2, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pamoja na mambo yote yaliyosemwa na wadau wengine hapo juu, walimu hawatekelezi wajibu wao ipasavyo. Walimu wengi hawafundishi ipasavyo, wanashiriki kufanya maovu(Si mfano wa kuigwa na jamii), hawatekelezi kazi zingine za kiualimu. Kwa hali hiyo walimu wataendelea kudharauliwa tu.

  Walimu wakitaka kuheshimiwa wajiheshimu wao kwanza kwa kufuata maadili ya ualimu kisha washikamane kudai maslahi zaidi katika kazi.
   
 12. I

  Irizar JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2010
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 217
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ikena, umegusa moyo wangu and I do agree with you.

  Inasikitisha sana jinsi Tanzania wanavyodharau walimu, bila walimu tutafikaje hapa tulipofika??!! na kweli walimu hawatakiwi kuwa WAJINGA, ni vema kuwaheshimu sana walimu.
   
 13. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  very sad... lakini haya mambo should be taken seriously by the respective Ministry...
   
 14. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #14
  Mar 7, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu unamaana wanalipwa kidogo kwa sababu hawatekelezi majukumu yao vilivyo?unataka kusema wabunge au watumishi wengine wanalipwa vizuri kwa sababu wana tekeleza wajibu wao vizuri na wanajieshimu? Na hapa kujieshimu mkuu una maana gani? sidhani kama hizo ndo sababu za walimu kutolipwa vizuri. ofisi za umma nyingi tumetembelea pengine unaweza kukuta walimu wanajitahidi kutoa huduma kwenye mazingira magumu kuliko mtu yeyote.May be kwa sababu watu waliofeli ni wengi kama watu wanadhani kupewa ajira ni kama kupendelewa tu na si haki yao.yaani hawajiamini vile. Kumbuka waziri mwantumu maiza aliwambia kama malipo ni kidogo si waache kusomea ualimu! wao kimya. Ukiwambia walimu wa kenya hivyo moto utawaka na lazima utajiuzulu tu.Wakati mwingine naunga EAC waje wawazindue hawa watumishi wetu. Na serikali yetu lazima ijiandae kwa hilo. Ni kama wananchi wa vijijini vile ambao hawajui wajibu wa serikali kwao. Hata kuji-organize kudai haki au kukataa kudharauliwa na waziri wao wanaona ni poa tu.Mishahara ya walimu na watumishi wengine ni sawa tu tena ya ualimu inazidi kidogo.TGSD ya ualimu aliye maliza chuo kikuu ni kubwa kidogo na GSD ya idara nyingine kwa Takriba Tsh1000. Lakini Per Day, Semina, Workshop, posho za kazini, gharama kodi za nyumba, matibabu usafiri nk hawa wenzetu hawana. Ukirejea pesa za budget zinazopitishwa bungeni haya mafungu yana-count kuliko mishahara.watumishi wengine wanamafungu haya. Walimu wanaambiwa zimeunganishwa humo humo wakati si kweli kwa sababu TGSD anayopewa na wa idara nyingie ni sawa wakati yule wa idara nyingie yuko legible kwa posho kibao.wenyewe kazini hakuna hata hizi chai za asubuhi. Nyumba miaka ya nyuma enzi za nyerere zilikwepo kwa sasa serikali inafahamu kabisa walimu wanapanga uraiani kama walivyo askari, manesi na watumishi wengine. wengine hao wanalipwa kodi za nyumba hata ma-lecture wametoa muda pesa za kodi za nyumba zilipwe haraka na juzi tu tanesco mumeona wanatoa units 750 kwa wafanyakazi wake. Hapo ndo umaskini wao unapoanzia. Walimu wanafahamu na hawadai vitu hivyo. Kenya wanapata kodi ya nyumba, afya, na zimeanishwa. Makato mengine ya PAYE, bima ya Afya, Ada ya ualimu, nazo ni kubwa mno.
   
 15. F

  FOE Member

  #15
  Mar 7, 2010
  Joined: Sep 21, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi wenzetu waalimu pia wanatakiwa kulipa ada? ndio ipi hiyo mkuu? I'm ignorant of that.
   
 16. T

  Tall JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 1,431
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Walimu wa UPE na sasa hawa wa Vodafasta ndio wamechangia kudharaulika walimu. LAKINI ni hapa mjini tu nenda vijijini we mwalimu anaheshima yake ati.
   
 17. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #17
  Mar 7, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kuwadharau walimu ni kujidharau sisi wenyewe kama taifa.
  Natuma ujumbe huu nikiwa mbele ya PC haya ni matunda ya walimu. Kinacho tusumbua mara nyingi ni kutojua vipaumbele vyetu kama nchi. Na mkorogo huu wote unatokana na watu kutojali haki za wananchi wengine ila wao kama viongozi kujilimbikizia mali.

  Hali hii ndio imepelekea ma Dk, Prof wote kukimbia vyuoni ili kwenda majukwaani ambako wanaona patawatoa, kwa nchi ambazo ziko makini hii ingechukuliwa kama ni alarm ambayo inatakiwa ifuatiliwe kwa makini kwa hofu ya kuangamia kwa taifa ki taaluma. Lakini kwa kuwa bongo tambalale who cares bwana let it be.
   
 18. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #18
  Mar 7, 2010
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Walimu walianza kudharaulika tangu pale serikali ya ccm ilipoona kuwa elimu sio kipaombele cha taifa hili.
  Pale walipoona kuwa awaye yote anaweza kuwa mwalimu ili mradi amemaliza darasa la saba (msingi) na kidato cha nne (form 4). Walipoona kuwa mwalimu anaweza kuandaliwa kwa miezi mitatu (upe na voda faster sasa). Lakini kubwa zaidi tumejengewa ndani ya taifa hili na tumeendelea kukubaliana na mfumo huu chakavu na matokeo yake fani pekee yenye thamani Tanzania ni Siasa kwani utakufikisha kwenye ufisadi mapema.
   
 19. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #19
  Mar 8, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,813
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Very serious comment Nono
   
 20. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #20
  Mar 8, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nilikuwa na maana ya mchango wa chama cha walimu mkuu.
   
Loading...