Kwa nini Waafrika tunaitwa bilingual wakati Wazungu siyo?

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,811
Bilingual maana yake ni mtu mwenye uwezo wa kuongea Lugha zaidi ya moja, mpaka hapo sina tatizo napo ila mahali nisipoelewa pale ambapo Waafrika karibia wote tunahesabika kama ni bilingual au hata waati mwingine Multilingual lkn Wazungu wao hawajitambulishi kama Bilingual ingawaje Wazungu karibia wote wanaongea Lugha zaidi ya moja?

Kwa mfano Waswidi mbali na Kiswidi karibia wote wanafahamu Kiingereza na Kijerumani kwa kiasi, Waholanzi karibia wote wanafahamu mbali na Kiholanzi, Kiingereza, Kijerumani na wengine hata Kifaransa lkn kamwe Muholanzi, Mswidi au hata Muingereza anayejua Kifaransa hawezi kujitambulisha kama Bilingual au Multilingual sasa ni kwa nini?

Ni kwanini sisi wanatuita Bilingual au Multilingual lkn wao hawajiiti hivyo? Kwa mfano hapa TanZania kuna watoto wengi sana leo hii naweza kusema sasa hivi mpaka asilimia 30 ya wanajua Kiswahili tu lkn bado tunaitwa ni Multilingual au Bilingual wakati nchi kama Uholanzi au Denmark zaidi ya asilimia 80 (80%) ya wananchi wake wanaongeoa Kiingereza kwa ufasaha kabisa pmj na kikwao lkn hawaitwi Bilingual, sasa ni kwa nini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom