Kwa nini Vita zidi ya Ugaidi/Terrorism visiitwe kuwa ni Vita kuu ya tatu ya Dunia? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini Vita zidi ya Ugaidi/Terrorism visiitwe kuwa ni Vita kuu ya tatu ya Dunia?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kevin.A, Aug 9, 2012.

 1. K

  Kevin.A Member

  #1
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Heshima kwenu wana-JF,

  Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara ni vigezo gani vinatumika ili vita yeyote kuwa mentioned kama ni Vita kuu ya Dunia?Na ni nani anajukumu la kusema kuwa hii ni Vita kuu ya Dunia (is it UN)?.Mpaka sasa kuna Vita kuu ya Dunia I & II.
  Nilikuwa nafikiri kuwa moja ya kigezo ni idadi ya nchi zinazoshiriki kupigana ktk hiyo vita.Nikajiuliza kama hiki ni kigezo kimojawapo basi ni kwa nini vita zidi ya Ugaidi/terrorism visiitwe ni Vita kuu ya tatu ya Dunia?Maana karibu nchi zote duniani zinapambana ktk hii vita na magaidi/terrorist wamezagaa karibu dunia kote.

  Naomba mawazo yenu ktk hili.
   
 2. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  hujafafanua vizuri hapo, karibu nchi zote unamaanisha nini?? hebu zitaje hizo nchi japo 10 tu. nijuavyo mimi, kwanza neno GAIDI kila anayelitamka ana maana yake, MIMI NIKIKUITA WEWE GAIDI, NA WEWE UTANIITA GAIDI. kwa sisi tunaoamini katika kila linalosemwa na matajiri wa dunia yaani marekani, israel, uingereza na marafiki zao, tunafuata tafsiri yao ambapo kwao yeyote ambaye anapingana na matakwa yao, huwa wanambatiza GAIDI ili wahalalishe kumtandika wanavyotaka (rejea Iraq, Libya, Palestina n.k). hizi nchi, hata wanafiki UN hawakuridhia zichapwe, lakini zilitandikwa.
  Kwa upande mwingine, ukifuatilia nchi kama Venezuela, Irani, Korea Kaskazini, Libya, Iraq, Palestina, Zimbabwe nao wanadai haya mataifa ya kimagharibi (marekani, israel, uingereza) ndo magaidi, sasa hapo inategemea wewe mwenyewe akili yako inayapima vipi mambo. Na msingi wa hayo yote nionavyo mie ni nchi zingine kutumia mabavu kutaka waitawale dunia wanavyotaka wao, wakiwaambia sasa muanze KUOANA WANAUME KWA WANAUME au WANAWAKE KWA WANAWAKE mseme, ndio mkuu, mkigoma HAKUNA MISAADA.
   
Loading...