Kwa nini viongozi wa tanzania si waoga ?? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini viongozi wa tanzania si waoga ??

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kwame Nkrumah, Jul 16, 2011.

 1. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Nilikua nasoma mada hapo chini ya jinsi spika aliyepita anavyoendelea kukaa kwenye nyumba ya serikali kwa kisingizio cha ustaafu.
  Kila kukicha viongozi wetu wanashindana kufanya ufisadi bila uoga na maamuzi yenye kuogofya.
  Licha ya mabadiliko yote yanayotokea ulimwengu wa sasa viongozi wetu wanakua kama wanaishi ulimwengu mwingine ambao wao hawataguswa na chochote.
  Tunashuhudia nchi zilizokua zinatawaliwa kipolisi ambapo ukienda kinyume na matakwa ya watawala unapotea , lakini leo wananchi wamechukua maamuzi ya kudai haki zao.
  Vyombo vyote vya ugandamizaji , na viongozi wake ni wa kwanza kusulubiwa wananchi wanapotwaa haki zao.
  Sasa viongozi wetu wanajiweka kwenye kundi gani? kwa nini hawaogopi umma wa Watanzania utakapoamka?
  Ni kwa nini hawana chembe ya uoga katika nafsi zao?
   
 2. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  nami inanishangaza: Spika Sita, ilitakiwa baada ya kustaafu arudishe nyumba ya serikali itumiwe na mtumishi mwingine anayefuata na yeye aende kwao Tabora kwani kazi iliyokuwa inamfanya aendelee kuishi mjini imeisha: sasa kama ndo hivyo wataanza kupeana Uspika na baada ya miaka 5 anastafu anabaki na nyumba ya serikali hivyohivyo na anayefuata, hizo nyumba mwishoe zitaisha waamie kwenye mahoteli ya kitalii. Nilisikia Makinda anadai kwaVile Sita ni spika mstaafu anastaili kuendelea kuudumiwa kwa heshima yake na ikiwemo na kuendelea kuishi kwenye Nyumba ya serikali iliyoko Masaki, hivi kwani akiwa kwao Tabora hizo huduma muhimu anazosema Makinda haziwezi kumfikia???Hatuwezi kuvumilia kuendekeza heshima kwa mtu mmoja eti lazima apewe huduma muhimu wakati watanzania zaidi ya milioni 40 wanalala njaa: ndo UFISADI unaofanywa na Serikali.,
   
 3. M

  Mapujds JF-Expert Member

  #3
  Jul 16, 2011
  Joined: May 12, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kama wanataka kila mstaafu ahudumiwe kwa kupewa nyumba na mahitaji mengine basi watenge eneo rasmi ambalo nyumba zitajengwa na kupewa wastaafu ili hizi zilizopo watumie viongozi walengwa.kwa bibi makinda anakaa wapi kama nyumba yake sita anayo?ufisadi huu kwani miaka yote ya kuwa madarakani sita hakuwahi kujenga nyumba yake?poor vision in this country.
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Jul 16, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  nafikiri wametawala muda mrefu halafu wanawadharau sana watanzania kwa kuwa hawawezi,mtazamo wao
  wana tabia moja mbaya ya kulindana kwa gharama yoyote ile
  watanzania tutalipa gharama kubwwa sana kuweka mambo sawa!
   
 5. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #5
  Jul 16, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Katika watu ambao sina imani nao ni wana siasa wa Tanzania
   
 6. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #6
  Jul 16, 2011
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Viongozi wetu si waoga kwa sababu hawawajibiki kwa wananchi. Mfumo ungekuwa mzuri enough ya wao kuwajibika kwa wananchi tusinge shuhudia madudu tanayoyaona siku hizi mfano;
  WM na Mawaziri kujibu hoja zinazowagusa wananchi anyhow,
  Matumizi mabaya ya pesa ya walipa kodi na mali mfano hilo la spika Sita,
  Huduma duni za kijamii...mfano afya
  Etc
   
 7. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #7
  Jul 16, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Wote tunakubaliana kwamba Sitta hatakiwi kuishi kwenye nyumba ile kwa misingi yoyote ile. Si peke yake, wapo wengi.
  Waziri wa elimu anayelipa mishahara hewa kwa maelfu ya walimu, Waziri aliyepokea barabara ya kwenda Mtwara iliyoanza kubomoka kabla haijaisha, Spika anayeziba mtaa mzima kwa ajili ya ujenzi wa nyumba yake binafsi, Waziri anayekaa hotelini kwa miezi na miezi bila hata chembe ya huruma kwa Watanzania wenzake, tena kwa hela zao. Madudu ya TANESCO hayaelezeki, Meremeta, EPA na mikataba ambayo hata mtoto hawezi kutia sahihi yake.
  Kwa nini watu hawa hawaogopi? Mabadiliko yanayotekea nchi zingine hawayaoni?
  Nakumbuka wahariri wa gazeti ka serikali la Tunisia walivyopigwa na waandishi wenzao baada ya utawala kuanguka, nakumbuka jinsi wakurugenzi wa radio ya Egypt walivyookolewa na wanajeshi baada ya Mubarak kuanguka. Hivi hata waandishi hawa wa Habari leo na TBC hawajui haya?Kwanini wanakubali kutumiwa kama vipofu? Majenerali zaidi ya 500 wa Egypt juzi wametiwa ndani kwa madhambi waliyofanya wakati wa utawala wa Mubarak. Ni nini kinawafanya akina Mwema wajisahau na kujiona ni tofauti?
  Ni kwasababu watanzania tuna "amani"? Ni kwasababu viongozi wetu ni wajasiri? Ni kwa sababu wizi na udhalimu upo toka katika familia zetu?Lakini kwa nini viongozi wetu hawaogopi??
   
Loading...