Kwa nini viongozi wa serikali uingia mitini wakitakiwa kutoa tarifa ya mambo mazito? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini viongozi wa serikali uingia mitini wakitakiwa kutoa tarifa ya mambo mazito?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Japhari Shabani (RIP), Jan 21, 2010.

 1. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #1
  Jan 21, 2010
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwanini imekua kawaida kwa viongozi wa seriksli kuingis mitini wakati wanapotakiwa kutoa au kuwasilisha ripoti ktk kamati kuhusu maswali mazito?Naamini hizo kamati zinztumia pesa na muda kusubiri au kuzifanyia kazi ripoti hizo,pia wizara au taasisi zinatumia fedha nyingi ili kuaandaa ripoti hizi.Iwejea wakati wa kuwasilisha ripoti hizi mawaziri au wahusika wanaingia mitini Hi ni nini DHARAU AU HAWANA CHA KUJIBU?AU NDIO UTENDAJI WA SERIKALI NA JK KWA UJUMLA?Ripoti ya richmound Ngeleja aliingia mitini sasa Kawambwa.Kama mambo yenyewe ni hivi kunamaana gani kuuda kamati.INATIA KICHEFUCHEFU. Waziri Kawambwa awatibua wabunge
  KUHUSU UNUNUZI WA MITAMBO YA IPTL
  Sadick Mtulya na Ramadhan Semtawa
  WAZIRI wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa jana aliwachefua wabunge wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kutokana na kushindwa kutokea kuwasilisha ripoti ya utendaji ya wizara yake.
  Anne Kilango, ambaye alikuwa akikaimu uenyekiti wa kamati hiyo, alilazimika kumtimua kikaoni mkurugenzi wa usafiri , Mussa Iyombe, ambaye alitumwa kuiwakilisha Wizara ya Miundombinu kwenye kamati hiyo.
  Wizara ya Kawambwa sasa imetakiwa iwasilishe ripoti yake katika wiki ya kwanza ya mkutano ujao wa Bunge uliopangwa kuanza Januari 27, 2010 mjini Dodoma.
  "Tumewarudisha tukiwa serious (makini) hawa watu wa wizara ya miundombinu kwa kuwa wizara imekichukulia hiki kikao kwa urahisi na wepesi wakati sisi tumekichukulia kwa uzito na nafasi ya kipekee," alisema Kilango jana kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es salaam.
  "Sasa tumewaamuru waje wiki ya kwanza ya kikao cha Bunge."
  Kilango alisema katika kikao hicho kamati yake ilitaka kukutana ana kwa ana na waziri, naibu wake, katibu mkuu na naibu wake pamoja na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi na makamu wake.
  "Sisi tulikuwa tunawataka hawa ili waweze kutueleza hali halisi na kutupa picha kamili ya hali ya barabara ilivyo nchini. Sasa wememuagiza mkurugenzi, unafikiri angetujibu ipasavyo yale ambayo tulitaka kujua," alisema Kilango.
  "Unyeti wa kikao hiki ni kutokana na ukweli kuwa barabara ndio roho ya maendeleo ya Watanzania na pia tulitaka kujua ahadi za ujenzi wa barabara zilizotolewa na Rais Kikwete wakati wa kampeni zimetekelezwa kwa kiwango gani."
  Kilango alisema pamoja na mambo mengine, kamati hiyo ilitaka kujua mtandao kamili wa barabara ulivyo pamoja na matatizo.
  Hata hivyo, kamati hiyo ilipokea ripoti ya Wakala wa Barabara (Tanroads) iliyowasilishwa na mkurugenzi wake, Felix Mrema, kwa mujibu wa Kilango.
  Jana ilikuwa ni siku ya mjadala mkali kwani wakati Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ikihoji uamuzi wa serikali kutaka kununua mitambo mitumba ya kampui ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL), Kamati ya Fedha na Uchumi ilihoji kuchelewa kwa mchakato wa ununuzi wa mitambo hiyo.
  Mzimu wa IPTL umechukua nafasi kubwa katika siku za karibuni baada ya ule wa Dowans Tanzania Limites kutulia kutokana na kesi iliyopo mahakama ya kimataifa ya biashara jijini Paris, Ufaransa na pingamizi la Tanesco nchini.
  Wiki iliyopita, vigogo wa Wizara ya Nishati na Madini walikuwa katika wakati mgumu baada ya wabunge wa PAC kuhoji mantiki ya serikali kutaka kununua mitambo hiyo kinyume na Sheria ya Manunuzi ya Umma inayozuia taasisi za umma kununua vitu vilivyotumika.
  Jana mbunge wa Tabora Mjini, Siraju Juma Kaboyanga alihoji sababu za mchakato huo kusuasua wakati tayari IPTL ilikwishalipwa kiasi kikubwa cha fedha.
  Takwimu za mwaka juzi za serikali zinaonyesha hadi mwezi Mei IPTL ilikuwa imelipwa zaidi ya sh 200 bilioni, huku kubadili mitambo yake kutoka dizeli kwenda katika matumizi ya gesi ikiwa ni Sh75 bilioni wakati iliwekeza mtaji wa Sh50,000 tu.
  "Ni mtazamo wa kamati nzima (Fedha na Uchumi), kwamba ni lini ununuzi wa mitambo ya IPTL utakamilika kwani mchakato wake umekuwa mrefu," alifafanua Kaboyonga ambaye kitaaluma ni mchumi.
  "Huu si msimamo wa mbunge mmoja, kamati nzima inataka kujua lini mchakato utakamilika ili kuondoa mlolongo mrefu wa ununuzi huo wa mitambo."
  Katibu mkuu wa wizara hiyo, David Jairo alisema mchakato huo umekuwa ukisuasua kutokana na kesi iliyo mahakamani.
  Kwa mujibu wa Jairo, baada ya kukamilika kwa taratibu hizo za kimahakama ununuzi wa mitambo hiyo utafanyika mara moja ili kuondoa uwezekano wa kulipa fedha zaidi kwa kampuni hiyo.
  IPTL imekuwa ikikoroga wabunge. Wakati kamati hiyo ikitia mkazo kutaka mitambo hiyo inunuliwe haraka na ikiwezekana kesi imalizwe nje ya mahakama, suala hilo limekuwa likionekana kwenda kwa kusuasua.
  Kamati hiyo ya Nishati na Madini, ilijikuta ikiingia katika mgongano wa hoja baada ya mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Masharika ya Umma, Zitto Kabwe, kutaka mitambo ya Dowans inunuliwe.
   
 2. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #2
  Jan 21, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Labda kwa kuwa wakikwepa kujibu hawa sumbuliwi afterwards na mambo huishia kiolela olela. wameshajifunza wadanganyika wanakelele za siku chache na kutoa labels hiyo ndio limit yao. Kufukuzwa kazi kwao kwa uzembe amna waziri mkuu anatishia Nyau watoto tu na hiyo vita yake anayoijua yeye mwenyewe so far.
   
Loading...