Kwa nini VIONGOZI WA DECI ;WASIPELEKWE KUPANDA MBEGU KEKO | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini VIONGOZI WA DECI ;WASIPELEKWE KUPANDA MBEGU KEKO

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Pdidy, Apr 23, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 23, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,613
  Likes Received: 5,782
  Trophy Points: 280
  Kwa kweli nilikuwa kama mshabiki mkubwa wa DECI lakini nakiri kukufahamu...naomba hawa watu yaani serikali kama inavyowanyanyasa wananchi kwa nini wale viongozi waliokuwtwa na million 100/300 nk wasiende kupanda mbegu nao pale KEKO....sidhani kama lyumba amesambaza ukimwi kwa karibu robo ya watanzania na yuko keko kwa nini hawa wanoua watu kama mlivyoona mama yule amekufa kwa kupeleka pesa za urithi.......sioni kama wanatofauti na wale wahindi walioko na kesi ya mauwaji kule KEKO jamani.....tunaomba kama serikali wameshindwa waachie wananchi wafanmye kazi kwani wachungajji wanajulikana mpaka wanapolala vyumba vyao......\
  wal msihangaike kuwatafuta
   
 2. S

  Shelute Mamu Member

  #2
  Apr 24, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama wewe ulipanda ilikuwa ni kwa tamaa yako ya kupata utajiri wa haraka haraka. Hakuna mtu alilazimishwa huko. Na wenye akili hawakuingia huko, ndiyo maana watu na Serikali walisema anayepanda huko anahatarisha mtaji wake mwenyewe. Aliyekutuma nani? ndio faida ya kutaka vya rahisi daima rahisi aghali rafiki!!!!!!
   
 3. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #3
  Apr 24, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,123
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Sasa kama mnakubali kuwa hela inaweza ikapandwa kama mbegu ikatoa mavuno, basi inabidi mkubali kuwa unaweza ukatokea ukame mbegu zote zikapotea.
  Au labda mchimbe visima mfanye kilimo cha kumwagilia.
   
 4. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #4
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkakati waandaliwa kuifufua Deci kwa mfano wa Yesu aliyekufa na kufufuka


  Geofrey Nyang'oro na Festo Polea
  WAKATI wanachama wa Taasisi ya Development Entrepreneurship Community Inciative (Deci) wakiendelea kujiorodhesha kwa ajili ya kung'oa mbegu zao; kuna taarifa za kuanzishwa kwa chombo kingine ndani ya taasisi hiyo chenye lengo la kurithi kazi zake.
  Chombo hicho kinadaiwa kwamba kitakuwa na nguvu kuliko Deci iliyosambaratishwa na seriakali, huku watendaji wakikielezea kwa kufananisha na Yesu Kristo aliyekufa na kufufuka siku ya tatu na kufanikisha ukombozi wa waamini wa dini ya kikristo ulimwenguni.
  Jumapili iliyopita serikali iliizika rasmi Deci kwa kutanganza kufunga akaunti zote za viongozwa taasisi hiyo na kuwataka wananchi wajiorodheshe kwa ajili ya kurudishiwa fedha zao walizopanda.
  Wananchi waliopanda mbegu zao walianza kukukusanyika katika ofisi za taasisi hiyo nchini kote kwa ajili ya kujiandikshisha, lakini kazi uandikishaji ulianza Jumanne wiki hii.
  Hata hivyo, zoezi hilo limeingia dosari kuduatia vurugu zilizotokea juzi katika ofisi za makao makuu ya Deci yaliyoko mabibo wakati watu wakigombea kuingia ndani kujiandikisha.
  Mwanancha mmoja ambaye alikuwa akiwashawishi watu kujiunga na chombo hicho kipya, alikuwa anawaambia kuwa Deci imekufa kama Yesu na kwamba itafufuka kwa nguvu mpya na kuwaletea mafanio makubwa kuliko ya kwanza.
  "Hata ukiingia ndani unaambiwa Yesu alikufa na kufufuka siku ya tatu, kisha kufanikisha ukombozi wetu. Hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa Deci ambayo sasa imekufa, lakini itafufuka ikiwa na nguvu zaidi ya ile ya kwanza," alisema Mwanachama huyo.
  Mwanachama huyo alisema taratibu zinazofanywa na uongozi hivi sasa ni kukiandaa chombo hicho kulingana na uwezo waliopewa na Mungu, ambao uliwawezesha kubuni Deci, na kwamba mipango ikiamilika wanachama wataelekezwa.
  Alisema sifa za wanachama watakaoruhusiwa kujiunga na chombo hicho ni wale walioko ndani ya Deci, wanaotarajia kuanza kung'oa mbegu kuanzia Aprili 25 mwaka huu.
  Alisema ili kuwapata wanachama watatumia utaratibu wa kuwashauri na kuwapa uhuru wa kuchagua kama watang'oa mbegu zao ama watazihamishia katika chombo hicho.
  Hata hivyo, tofauti na juzi, jana zoezi la kung'oa mbegu liliendelea kwa utulivu huku ulinzi katika ofisi hizo ukiwa umeimarishwa.
  Askari polisi likishirikiana na walinzi Kampuni ya ya Ulinzi ya Chui walifanikiwa kuwalazimisha wanachama waliokuwa wamefurika katika eneo hilo kufuata taratibu zilizotolewa na uongozi wa Deci, ikiwemo kujipanga katika mistari tofauti.
  Askari hao walitumia mbinu mbalimbali kuhakikisha kuwa vurugu hazitokei na kuhatarisha maisha ya watu kama juzi. Ili kudhibiti watu kukiuka utaratibu, walifunga kamba karibu na mlango wa kuingilia ofisini kwa ajili ya kuwaongoza kuingia ndani kwa kufuata mstari.
  Kutokana na ulinzi huo mamia ya wanachama walijipanga foleni katika mistari kuanzia kwenye makao makuu ya ofisi hizo hadi karibu na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kilichoko Mabibo jijini na kuwaamuru wafuate maelekezo yaliyotolewa na uongozi wa taasisi hiyo.
  Bila kujali mvua iliyokuwa ikiwanyesha na kukatika, wanachama hao walibaki katika foleni wakihofia nafasi zao kuchukuliwa na watu wengine.
  Mmoja wa wanachama hao ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini, aliliambia Mwanachi kuwa alifika katika ofisi hizo saa 11:00 alfajiri na kukuta watu wengi wameshafika wakisubiri kupewa maelekezao ya jinsi ya kupata huduma.
  "Niliamua nije hapa alfajiri ili nipate huduma mapema ili niende kwenye shughuli nyingine, lakini nilipofika hapa nilikuta umati mkubwa wa watu," alisema mwanachama huyo.
  Jana uongozi wa taasisi hiyo ulibadili ratiba iliyokuwa ikitumika awali na kuandaa ratiba mpya wa kutoa namba kwa wanachama badala ya kuita makundi ya watu kwa kufuata tarehe na mwezi waliopanda.
  Ratiba ya jana ilionyesha kuwa wanaotakiwa kujiorodhesha ni waliopanda mbegu zao kuanzia Machi 2 hadi 7, 2009 na leo ni waliopanda Machi 9 hadi 14.
  Mabadiliko hayo yalifanyika kwa lengo la kurekebisha kasoro zilizo tokeza juzi na kusabisha watu 10 kuzimia na saba kutumbukia kisimani baada ya vurugu kutokea wakati wanagombea kuingia ofisini kujiandikisha.
  Nje ya ofisi hiyo baadhi ya wanachama walalamikia utaratibu wa kuorodhesha majina yao upya, kwa madai kwamba wangetumia majina yaliyopo mafaili yaliyotumika wakati wa kupanda.
  "Sisi wengine ni wafanyakazi, jana tulifika hapa lakini hatukufanikiwa kuorodhesha majina yetu, leo foleni ndio hiyo.
  Wanachama hao walisema kama Deci wangetumia majina ambayo watu waliyatumia kujioorodhesha wasingepata usumbufu wa kuja mara kwa mara kujiorodhesha.
  Kwa mjibu wa ratibu mpya, wanachama hao wataanza kung'oa mbegu zao rasmi Aprili 25 mwaka huu kwa wale walioorodhesha majina yao Aprili 21 na waojiorodhesha juzi walipwa Mei 4, mwaka huu.
   
 5. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #5
  Apr 24, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Unapoenda kufungua akaunti ya Akiba, na kutarajia kupata faida ya asilimia tatu kwa mwezi, hapo hujapanda mbegu? Benki nazo ni sawa na DECI, lakini hazisemi kwamba wanafanya wanayoyafanya DECI? Tatizo ni kwamba, wanataka sisi tupate kidogo wao wachukue kikubwa. Mfano, ukichukua mkopo (kama UKIFANIKIWA.... maana kuchukua na kufanikiwa ni mambo mawili tofauti....) wa Shs. 10 milioni, utarejesha Shs. 16 milioni ndani ya miaka 5, hii ni kwa CRDB. Lakini ukiwekeza Fixed Deposit Account ya Shs. 1 milioni, utavuna Shs. 3 milioni baada ya muda huo huo wa miaka 5. Kupanda "mbegu" huko CRDB unavuna Shs. 50,000 kwa mwezi, lakini wakichukua "mbegu" yao na kukupa wewe, unawarejeshea Shs. 100,000 kwa mwezi. Sasa kwa nini wamiliki wa CRDB na wezi wengine wasiende kupanda mbegu Keko? Jibu unalo! Tatizo sisi Watanzania ni vichwa maji. Kila jambo geni tunalipiga vita, tukiambiwa hiki kibaya, hatuulizi ubaya wake ni upi, tunasema: SAWA! Tutakuwa kondoo mpaka lini? Kwa nini tunakubali kila tunachoambiwa? Haya, wanachama wa DECI wamekatazwa kukutana na kujadili hatma ya fedha zao, mahali popote pale, kwa amri ya Kamanda Kova. Sawa? Jiulize... Kova anatoa amri kwa minajili gani? Anatumia kifungu gani cha Sheria? Haki ya Kukutana (Right of Peaceful Assembly) imeainishwa wazi kwenye Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Sasa toka lini utaratibu wa watu kulazimika kuomba KIBALI kwa Polisi (mbwa wa mafisadi... samahani, mtaniwia radhi, lakini huo ndio ukweli!) ulianza, mimi sijui. Na Watanzania walivyo na nidhamu ya woga, basi, watakubali tu! Serikali imefunga akaunti za DECI, ili iweje? Hizo pesa za Watanzania watazipataje, iwapo akaunti zimefungwa? DECI watarudishaje hizo pesa kwa wanachama wao? Tutakuwa WAOGA mpaka lini? Tutakuwa WAJINGA mpaka lini? Tuamkeni, tufungue macho, TUMEINGIZWA MJINI! WIZI MTUPU! ./Mwana wa Haki! Na bado nitasema! Siogopi kufa! Siogopi kutishwa! Kufa ni WAJIBU wa kila mwanadam!
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Apr 24, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  There goes Mwanahaki
  hongera mkuu.
  ila napinga na kupiga vita upatu na hii DECI. maana haohao watanzania wakiambiwa kitu hiki ni kizuri huwa hawaulizi mara mbilimbili hata kujua huo uzuri upo wapi. mpaka wapige dafrao ndipo zainze zile nyimbo tukufu 'serikali ilikuwa wapi?'

  Mi nakwambia TZ ni nchi ya miujiza kwa kuwa hata kama hizo akaunti zao zikifungwa bado wataweza kuwalipa wanaMBEGU wao waliooteshea jangwani....
   
 7. NgomaNzito

  NgomaNzito JF-Expert Member

  #7
  Apr 24, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 561
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mama alfu wanaotakiwa kupelekwa ni Mkulo na Ndulu wakishirikiswa watu wa UWT, Viongozi wa DECI waachwe warudishe hela za watu kwanza habari yao ni baada ya zoezi hilo kuisha ndio ijulikane pumba na mchele
   
 8. Shukuru

  Shukuru JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2009
  Joined: Sep 3, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi siufagilii huu upatu wa DECi ila ninachoamini ni kuwa wajamaa(pastors) walikuwa on business with fool tanzanian.....so its time for them (tanzanian) to realise their foolishness....

  You can not put 100 and get 150 free then come back to claim your 100.
   
 9. M

  Magehema JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 448
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sio wote waliokuwa wanataka utajiri wa haraka, mfano wanafunzi wa vyuo vikuu baada ya kuchukua boom waliona bora wakahifadhi nusu ya boom deci ili baada ya semester kwisha wakachukue boom lao. Wengi walihofia kuweka bank kwasababu wangeenda kuchukua kidogo kidogo hadi zinakatika. Madenti wengi wameliwa fedha zao na deci.
   
 10. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Haya ni kama ya abunuwasi aliazima sufuria kwa jirani siku ya 3 akarudisha mawili akadai sufuria limezaa.Baada ya wiki akaazima tena jamaa baada ya kuona kimya akauliza vipi mbona hurudishi sufuria? Akajibiwa limekufa,jamaa kuja juu akaambiwa kama ulikubali lilivizaa na kufa ukubali.

  Mama mia unavosema wakapande mbegu Keko ujue kule mbegu zake za aina ingine.
   
Loading...