Kwa nini viongozi hawataki kukutana na wanafunzi wa elimu ya juu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini viongozi hawataki kukutana na wanafunzi wa elimu ya juu?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Matemu, Nov 8, 2008.

 1. Matemu

  Matemu Member

  #1
  Nov 8, 2008
  Joined: Nov 29, 2007
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nasikitishwa na kufadhahishwa sana na hali tete inayoendelea hivi sasa katika taasisi zetu za elimu ya juu nchini.Hali ya migomo na kutishia kutoingia madarasani kunapofanywa na wasomi wetu limekuwa jambo la kawaida hivi sasa kiasi kwamba inapopita miezi sita bila kusikia taarifa hizi inakuwa ajabu sana.
  Kinachonisikitisha zaidi madai ya Wasomi wetu yamekuwa yaleyale kila siku ama yanayofanana kiasi cha kufikia hatua ya kujiuliza hivi njia za usluhishi zimeshindikana kufanyika.Wataalamu wa organizations and management mara nyingi husema kwamba mahali pasipo a mawasiliano mara nyingi migogoro hutawala kwa sababu watu wa chini hukosa mahala muafaka (forum) ya kuwasilisha matatizo yao.
  Jana wakati akifunga kikao cha bunge waziri mkuu alisema kwama "Serikali haitavumilia migomo isiyokuwa na kichwa wala mkia na viongozi wote watakaongoza migomo hiyo watachukliwa hatua kali za kisheria" Hebu tichambue kauli hii kwa migomo inayoendelea hivi sasa kwavyuo mbalmbali nchini.Hapa naona kama kuna njia ya ubabe inatumika katika kuzima migomo hii.
  Suala la kuwachukulia hatua viongozi sioni kama litasadia isipokuwa litaongeza tatizo zaidi kwa sababu ukifukuza viongozi wa leo kesho wataibuka wengine.Hivi kama Pinda ana hoja za kutosha kwanini asiitishe mkutano pale NKURUMAH kama alivyokuwa Akifanya Mw Nyerere na kwa hoja zenye nguvu akawashawishi wasomi wetu kukubaliana na sera ya uchangiaji wanayoipinga?
  Nahisi viongozi hawana ujasiri wa kutosha wa kuongea mbele ya wanafunzi (hsusani wa UDSM) Wanajua hoja zao zitapwelea mbele ya maswali makali yenye data kutoka kwa wanafunzi hao.Wanajua sera yao wameitunga kutokana na kushinikizwa na mataifa ya nje,Mwishowe wanaishia kuharibu vyama va wanafunzi kwa kubandika vibaraka vyao ili vikose nguvu ya kuwawakilisha wanafunzi ipasavyo (rejea kuvunjika kwa kwa TAHLISO)
   
 2. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #2
  Nov 8, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Serikali yetu imeshindwa ku provide equitable and affordable education to the majority of the Tanzanians.
  Wameshindwa kuprovide opportunities for every young man to live a better life including the old ones!
  Sasa wameamua kuhamia kwenye vitisho.Sijui kama tutafika hivi ila serikali inapaswa kuwasikiliza hawa wanafunzi.
  Wanafunzi wa vyuo private kama wao wanaona wana uwezo sana then hiyo mikopo yao ihamishwe public universities ili ambao hawana uwezo waweze kuboresha maisha yao maana wanafunzi wengi wa hivi public universities wanatumia pesa zao za matumizi ya kila siku chuoni kutuma majumbani kwao ambazo zinatumika kama ada ya ndugu zao!
   
Loading...