Kwa nini vijana tusiungani na kuanzisha a Publication? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini vijana tusiungani na kuanzisha a Publication?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Jul 8, 2011.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Sasa hivi tunaona vijana wengi wakiungana kufanya vitu kwa pamoja kwa nia ya kujiendeleza na kuendeleza taifa kiujumla? Tumeona Maxcence Mello na mwenzie wakianzisha JamiiForums, tunaona jinsi baadhi ya vijana wanavyo peana nguvu kwenye siasa, nk.

  Mimi siku zote nimekua na wazo la kuanzisha a publication inayo jikita zaidi kwenye siasa na maswali ya uchumi na kijamii. Ndiyo najua hata sasa hivi kuna magazeti kibao lakini mengi yana upendeleo wa kisiasa ambao haulengi kutoa ukweli bali kusafisha au kuchafua upande fulani. Kikubwa zaidi ni kwamba hamna magazeti yanayo milikuwa na vijana.

  Kwa nini nimetoa wazo la magazeti na si redio au tv? Kwa sababu kupitia JF nime kutana na vijana wengi wenye uwezo mkubwa wa kutumia nguvu ya kalamu. Kwa nini sasa tusiungane na kutumia nguvu hiyo ya kalamu nje ya JF?

  Najua ni kazi nzito lakini hakuna kinacho shindikana. Naamini ili kuleta mabadiliko lazima vijana tuingie kwenye nyanja mbali mbali na si siasa tu. Tutumie vipaji vyetu kwa manufaa ya nchi na si kujiangalia sisi binafsi tu. Naamini kwanzia sasa mpaka 2015 na hata mbele zaidi vijana tunaweza tukawa na impact kubwa kwa hili taifa.
   
Loading...