Elections 2010 Kwa nini upinzani utashindwa kwa kishindo?

Hofstede

JF-Expert Member
Jul 15, 2007
3,577
1,107
Ni jambo la kushangaza sana Tume ya uchaguzi inabadili sheria za mchezo katikati ya mechi. Hivi sasa matokeo ya ubunge na urais hayatangazwi tena katika kata .. Wapinzani wapo kimya!!

Kura zimemaliza kupigwa masaa 24 yaliyopita lakini wasimamizi wamegoma kuyatangaza mpaka wapewe maelekezo ya go ahead na CCM .. Wapinzani wamekaa kimya

My take:

Huu ndiyo wakati wa Dr. Slaa, Prof Lipumba kuitisha mkutano na waandishi wa habari na kutoa ultimatum kuwa matokeo yatangazwe yote, vinginevyo kinachoendelea Zanzibar kumhujumu Maalim Seif kikiisha kinahamia Bara. CCM wanachofanya ni ku-buy time ili kutuliza munkari za wapiga kura na kuwa fanya wachoke na suala hili ili wasione haja ya kudai haki yao kwa vyovyote.

Kinachoshangaza ni kwamba maeneo yote CCM iliposhinda yanatangazwa harakaharaka mpaka ya urais Singida mjini. Kila msimamizi amepewa talking point kuwa ni jiografia ngumu, ila wakati wa kusambaza vifaa in late hours jiografia ilikuwa rahisi. Huu ni upuuzi kama wa 1995, kura zikipigwa mawakala waka sign forms na mabox kufungwa nini cha ziada?. Huu upuuzi unatakiwa kukemewa kwa nguvu zote. WAPINZANI AMKENI MNAWAKATISHA TAMAA WATANZANIA WANAO WAANGALIA NINYI C'MON!
 
We subiri wagombea hao ni watu makini na wanafahamu vyema michezo yote michafu ya KIJANI hapatakalika hapo...
 
hakuna vyombo vya habari vilivyo na ushujaa huo, hata kama Slaa na Lipumba watataka, hakuna chombo kitakachokubari
 
Mimi kinachonishangaza ni kitu kimoja, ninavyofahamu mimi nadhani lazima kila chama kiwe na wawakilishi wao ambao kazi zao ni kuhakiki zoezi zima la kuhesabu kura, kwa hivyo lazima wawe na takwimu ya kura walizopata wagombea wao, Jamani tupeni hizo data tutoe rambirambi mapema huko CCM makao makuu (CHIMWAGA).
 
Hebi wasinitie hasira mie,,,,, upuuuzi gani sasa huu, kwanini jana watangaze na leo waaache, sijui niwatu.... ila ni vibaya basi nawalaani
 
Hapo mdau umenena ukweli,ingawa inaeleweka wawakilishi wa vyama wanajua lakini si sahihi kutoyaweka haradhani haraka iwezekanavyo.Ni lazima itakuwa ni ktk lengo la kuchakachua hivyo ni vizuri wahusika wakachukua hatua mapema,kwani jukumu la kulinda kura walizopigiwa na wananchi ni la kwao.
 
Mimi nashangaa sana. Hivi matokeo yanawai kutoka singida ila kutoka kawe na Ubungo jiografia ni ngumu. Hivi imekaa sawa kweli hii?
 
Back
Top Bottom