Kwa nini upinzani huchelewa kuteua mgombea uraisi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini upinzani huchelewa kuteua mgombea uraisi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaFalsafa1, Feb 2, 2011.

 1. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #1
  Feb 2, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Chama cha Mapinduzi huwa kina mteuwa mgombea wao wa uraisi mnamo mwezi wa tano wa mwaka wa uchaguzi. Vyama vingine havi teuwi mgombea na mgombea mwenza wao mpaka kwenye mwezi wa nane au wa tisa. Je hamuoni ratiba hii ya kuteua mgombea ina ifavor CCM zaidi?

  Kwa CCM kuteua mgombea mapema ina wapa muda zaidi ya kumnadi mgombea. Hata kama kampeni hazija anza rasmi kitendo cha kumteua tu mtu tayari ni kampeni kwa maana wananchi wata kua wamesha jua mgombea wenu ni nani na wataanza kumchuja.

  Hivi unaweza kufikiria ingekuaje kama Dr. Slaa ange teuliwa kugombea kupitia Chadema tokea mwezi wa tano? Kati muda mfupi tu aliokua nao kati ya kuchaguliwa na kugombea aliweza kuzoea zaidi ya asilimia 23. Je angekua na muda zaidi wa kujinadi ingekuaje?

  Huu ni wito kwa vyama vingine. Teueni wagombea wenu wa uraisi mapema zaidi. Hii ya kuteua wagombea wenu miezi baada ya CCM inaipa CCM advantage kubwa sana. Inaweza ikaonekana ni jambo dogo ila tactically speaking kwenye uchaguzi miezi ni muda mrefu sana.

  Nawakilisha
   
Loading...