Kwanini ukiwa hauna pesa unadharaulika?

commm

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
1,674
1,903
Wakuu kama kichwa cha uzi kinavyosomeka hapo juu.

Hivi ni kwa nini mtu ukiwa huna pesa, yaani ninamaanisha ukiwa na maisha duni unadharaulika?

Na hili utaliona kuanzia ngazi ya familia, jamii inayokuzunguka na muda mwingine hata kwenye nyumba za ibada.

Ni kwa nini mtu kama huna kitu watu wanashindwa kuthamini hata utu wako?
 
Ndio nazitoa hapa

20200326_192038.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu Kama kichwa cha Uzi kinavyosomeka hapo juu

Hivi Ni kwa nini mtu ukiwa huna pesa ,yaani ninamaanisha ukiwa na maisha duni unadharaulika?

Na hili utaliona kuanzia ngazi ya familia,jamii inayokuzunguka na muda mwingine hata kwenye nyumba za ibada

Ni kwa nini mtu Kama huna kitu watu wanashindwa kuthamini hata utu wako?
kwa sababu pesa ni sabuni ya roho. Roho chafu huwa haithaminiki
 
Kwasababu pesa inakuwezesha kutatua matatizo na inatafutwa kwa jasho so ukiwa hauna inaonyesha wewe pia ni sehemu ya tatizo na pia Ni mzembe ila sio wote wanakudharau ila ndo vile tena mimi binafsi huwa nadharau mtu kujitakia ujinga,yani mbumbumbu yani empty mind😎
 
Kwasababu ulipopata pesa ulikua unadharau sana nakujiona unamchango mkubwa kuliko wengine, na ukasahau kua maisha ubadilika leo waweza kua chini kesho juu.
sasa hapo kwanini wasikudharau
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom