kwa nini ufisadi unaonekana kwenye halmashauri zetu nchini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kwa nini ufisadi unaonekana kwenye halmashauri zetu nchini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by onania mzule, Jun 24, 2012.

 1. o

  onania mzule New Member

  #1
  Jun 24, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wakati umefika serikali iweze kubadili mfumo wa ajira hasa kwa management za halmashauri zetu.kuna baadhi ya halmashauri zinafanya vizuri sana lakini nyingine huwezi kuamini.watu wenye uwezo wa kufanya kazi wanakuwa frustrated ili wakimbie na kuacha nafasi kwa wasionauwezo na ambao wanamtandao strong wa kuiba pesa za serikali watawale.wengine wanaajili watu lakini hawawapi mamlaka ya kutenda,anakuwepo tu ili ikitokea ufuatiliaji jina linaoneshwa kuwa tuna mtu mwenye sifa hizi kumbe kiuhalisia hatumiki.kunatabia pia ya management kupeleka watu wasionasifa kwenye shughuli zinazoonekana zina pesa nyingi kwa makubaliano ya kutoa % fulani kwa mgt.kama wewe hutoi basi hutapelekwa semina yoyote!watu wanapewa madaraka kwa undugu au ukabila au hongo ya ngono,kama huna vyote hivyo hakuna atakayekuona hata kama ni mtu unayefaa kwenye kazi.mbaya zaidi ukionekana ni mzuri kwenye kazi ndo wanajitahidi kukufanya usionekane kwani wanahofia kunyanganywa nafasi walizopeana bila kukudhi vigezo.lakini pia madiwani wapo huko na wanaona ila hakuna anayethubutu kukemea mambo hayo kwa sababu kila mtu ameenda kuganga njaa yake.sehemu nyingine diwani akiongea watendaji wanaunda mbinu za kumwangusha,huwezi kuamini halmashauri nyingine zina watu kwenye mgt wenye diploma wengi lakini wenye degree wamewekwa vijijini ,basi ingekuwa ni kwa makubaliano lakini kunaudanganyifu unafanyika wakati wa ajira,mtu akienda kuripoti anaambiwa anapelekwa kijini.akifuatilia anazushiwa uongo mwingi na kuna watu special kwa kufanya mambo hayo kwenye halmashauri zetu.kwa kweli halmashauri ambazo hazifuati utawala bora watumishi wenye degree na masters ni wachache sana wanaweza kubaki huko na kunyanyasika wakati wanajua wanauwanja mpana wa kuajiriwa secta binafsi.matokeo yake ni kwamba wasomi wenye uwezo wanaondoka na kuacha mitandao ya wasio na ujuzi ila wanaoamini kuwa wanaweza kufanya kazi kimazoea,hayo ndo tunayoyaona sasa yanajitokeza.ukiuliza wasomi wengi wanaofanyakazi halmashauri hawapendi kuendelea na kazi pale ila kwa kuwa wengine majukumu yanawabana ya kifamilia wanavumila,wengine ndo wanaamua kuacha na kufanya shughuli ambazo hata hawakusomea ilimradi kuepuke manyanyaso ya halmashauri zetu.nimekutana na wengi waliopata mikasa ya halmashauri na hawataki kusikia kabisa.serikali inabidi kuwa makini sana na viongozi wanaopewa kuongoza halmashauri,idara na vitengo juu ya uwezo wao kielimu, utendaji na uongozi.la sivyo ni vigumu sana kuendelea nchi yetu kwa kuwa huko chini kwenye halmashauri zetu watu wanafanya wanavyoona!kiongozi anafanya taasisi ya serikali kama kwake kwa kweli tubadilike,viongozi wa juu tusipewe taarifa za kupikwa na viongozi tukasahau kuongea na watekelezaji wa chini wanasemaje!hilo ni kosa kubwa serikali yetu inafanya ya kutokuwa na mahusiano na wafanyakazi wa chini ya moja kwa moja.najua kuna wengi wanauzoefu na halmashauri zetu na yanayowapata wenzetu wasio na mtandao huko.naomba tushirikishane uzoefu ili tuweze kuwasaidia viongozi wa wajuu sehemu za kuanzia.
   
Loading...