Kwa Nini Udini Safari Hii Haukuwasaidia CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa Nini Udini Safari Hii Haukuwasaidia CCM?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Buchanan, Dec 28, 2011.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Dec 28, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  WanaJF,
  CCM imekuwa ikieneza propaganda kwamba CUF ni chama cha Waislamu na walifanikiwa sana kuwaaminisha wananchi kwamba CUF na Uislamu ni kama uji na mgonjwa! Baada ya kuisambaratisha CUF, CDM kiliibukia BUNGENI na hoja ya UFISADI ambayo iliwapa umaarufu hadi leo. CCM ikaibuka tena na hoja kongwe ya Udini, Ukabila na Ukanda! Kwamba eti CDM ni Chama cha Wakristo, Wachagga na Watu wa Kaskazini!
  This time naona mambo hayawaendei vizuri CCM inaonekana kuwa nguvu ya CDM haipungui hata kidogo kwa kueneza propaganda za Udini! Je, ni kwa nini CCM imeshindwa kushawishi umma juu ya "Udini" wa CDM kama ilivyokuwa kwa CUF?
   
 2. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kwa sababu matendo huongea zaidi kuliko maneno.
   
 3. Mtanzania haswa

  Mtanzania haswa JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 665
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  kwa sababu sio kweli
   
 4. P

  Paul S.S Verified User

  #4
  Feb 24, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu propaganda hiyo inafanya kazi sana sema tu namna ya kujua ufanisi wake inatofautiana na enzi
  Enzi kwa maana sasa hivi watu angalau wameamka kidogo lakini hata hivyo kwa hizi chaguzi ndogo sio rahisi sana kuona impact yake

  Kama hali itaachwa iendelee hivi na chuki hizi ni ukweli usiopingika itakuja kui cost CDM kwenye uchaguzi mkuu ujao, maana CDM watakwenda kwenye uchaguzi bila kuwa na hakika ya kura za jamii fulani inayoamini CDM ni kwa dini fulani
  Amini usiamini wananchi wameichoka CCM lakini hii ni moja ya nyezzo zao muhimu kuitumia kuakikisha jamii yote ya Kiislam haipigii kura CDM

  Kitakachotokea ni kuwa ingawa CDM itafanya vizuri lakini watakuwa na kikwazo cha wingi wa kura toka kwenye jamii ya waislam, na this time utaona mikoa ya pwani na yenye waislam wengi itakavyo hamasishwa na kuwa na wapiga kura wengi kupita kiasi ili hali ile yenye kutegemewa kuwa na CDM wengi hakutakuwa na uhamasishaji wa vitambulisho vya kura hivyo idadi ya wapiga kura itakuwa ndogo
   
Loading...