Kwa nini tutumie $ badala ya tsh. Ktk tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini tutumie $ badala ya tsh. Ktk tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by hsigira, Feb 4, 2011.

 1. h

  hsigira Member

  #1
  Feb 4, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu naomba mnisaidie hili, inakuwaje wafanyabiashara wanatutoza $ hapa kwetu kwa huduma za usafi, maji ya kisima(ya "chumvi") na ulinzi (walinzi wa kisasa a.k.a security) na serikali haikemei? au ni halali kuitumia $ kwa huduma hizi?
   
 2. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Pole, wanaangalia maslahi.
  Si unajua thamani ya lipesa letu linavyoflactuate.
   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Mamii.......tatizo ni ufisadi tu! Husninyo i tell u me, hii nchi ni uozo.
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  ngoja nitafute nchi nyingine tukajifiche huko. Sawa bosi wangu?
   
 5. regam

  regam JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2011
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 268
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nilibahatika kwenda India na kustaajabu kuhusu dolari.
  Financial policy yao hairuhusu transaction yoyote kufanyika kwa dolari. Nakumbuka siku moja nilitaka kunununua kamera nikiwa na dolari zangu. Ilishindikana. Yaani hata bureau de change zao wako very strict. Hii inafanya rupia yao kuwa na nguvu saana. Kwa sasa iko dolari moja kwa rupia arobaini. Hata hapa kwetu inawezekana kabisa kuzuia transactions zote za kidolari.
   
 6. d

  danilo silva Member

  #6
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hasa hawa DSTV mbona tunalipa kwa dola?
   
 7. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Kumbuka kuwa hakuna serikali inayosimamia mambo hayo hapa, inauma sana kuona tunaiachia pesa yetu na kuanza kutumia $ tunaelekea Zimbabwe maana hawa hata pesa yao wenyewe jinsi Mugabe alivyouwa uchumi wao na kukosa hata kutumia pesa zao sasa wanatumia US$ na sisi tunaelekea hukuhuko kama hatutakemea hiki kitu. Nchi imewekwa kwenye Auto pilot na mkwere
   
 8. h

  hsigira Member

  #8
  Feb 5, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Swala la $ ni hatari kuliachia hivi hivi. Hapa nilipo wenzetu wenye asili ya asia wameligeuza kawaida. Hata kuchangia huduma za usafi na ulinzi tunalazimishwa ziwe ktk dolari! Je, wanasheria wanatuambia nini juu ya matumizi ya dolari? Tusaidiane tusikae kimya.
   
 9. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2011
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 60
  Mi pia nawashangaa baadhi ya wamiliki wa hoteli. Hoteli iko uswazi mnajidai eti 'room $20' wakati wageni mnapata mara moja kwa mwaka.. Acheni hizo
   
 10. m

  mzambia JF-Expert Member

  #10
  Feb 6, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Dolali ndiyo nzuri ili tukome kiuchumi
   
 11. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #11
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Haya malalamiko yanatakiwa yawasilishwe kwa gavana wa BOT ambaye pia nina hofu kama anaweza kufuatilia kwa ukaribu. Ni hatari kwa uchumi wa nchi kuendeshwa kwa kutumia fedha(internal transaction) ya watu wengine. Ndiyo maana pesa yetu inashuka thamani kila mara. Uki control dollar circulation inasaidia kuimarisha internal currency. Tatizo wataalamu wetu wa uchumi na mambo ya fweza wamelidhika na uchakachuliwaji unaondelea.
   
 12. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #12
  Feb 6, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  ahsante san kwa mtoa mada, sio siri hili ni janga lingine la Taifa, nenda nchi zozote zile zinazoendelea kwa kasi kama utaona upuuzi kama huu wa kwetu, yaani eti niko nchini kwangu leo nakwenda Bagamoyo nikiwa hotelini naambiwa kulipa dola, nawapa TZSH wahudumu wanazikataa na kunilazimisha lazima nizibadirishe , duh jamani hivi sisi tuko huru katika hii nchi ? kuna umhimu gani ya kutufanya watumwa wa nchi yetu?
  Trust me, waliikata pesa na ikanilazimu kuenda Bureau de change na huko nikakupa exchange rate yaani ni ya kwao tu maana haiendani kabisa rate ya kawaida.
  Hii nchi inakufa taratibu kwa uoozo wa viongozi wetu, hatuna viongozi na hili ndio tatizo kubwa.
   
Loading...