Kwa nini tusitumie mawe kujenga barabara za miji?

mtafungwa

Member
Feb 27, 2012
74
16
SERIKALI mkoani Mwanza imeanza kujikita katika ujenzi wa barabara kwa kutumia rasilima zilizopo mkoani humo zitakazosaidia kutoa ajira pia kwa wananchi wake.

Akitoa maelekezo kwa uongozi wa Wilaya ya Ilemela jana Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikilo alisema kuwa wilaya hiyo ndo itakuwa wilaya ya kwanza kwa kutengeneza miundombinu ya barabara kutumia mawe yanayopatikana mkoani humo.

Alisema kuwa katika bajeti ya mwaka 2012/13 wilaya hiyo ihakikishe inatenga fedha kwa ajili ya ujenzi huo, akifafanua kuwa matumizi ya mawe katika barabara ni nafuu kuliko lami.

“Kila kilomita moja ya barabara ya mawe inagharimu Sh600 milioni, kati ya hizo milioni 250 zinabakia kwa wananchi kwa kuwa wao ndiyo watakuwa vibarua wa kuchonga mawe,”alisema Ndikilo.

Alisema kuwa ujenzi wa barabara kwa mawe ni nafuu ikilinganishwa na lami ambayo hugharimu zaidi ya Sh1 bilioni kwa kilomita.

Alisema kuwa ujenzi huo wa barabara ya mawe hauhitaji wataalamu kutoka nje ya nchi kwa sababu mkoa huo unao makandarasi wa kutosha walio na ujuzi wa kutengeneza barabara hizo.Alisema kuwa faida nyingine ya barabara za mawe ni uwezo wa kudumu kwa miaka 100 tofauti na barabara nyingine hivyo kuitaka wilaya ya Ilemela kutumia fursa hiyo ili kuimarisha miundombinu yake ya barabara. Source: Mwananchi 29.2.2012
 
Barabara za mawe zinatumika duniani kwa zaidi ya miaka 4000 kwa sasa.

Kwani hizi lami unazoona zinatumia nini kama si mawe?
 
Back
Top Bottom