Elections 2010 Kwa nini tunauita Uchakachuaji?

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,874
310
Ivi kwa nini tunaita huu WIZI wa kura UCHAKACHUAJI? Ni kwa ajili ya kupunguza makali ya ukweli wa jambo au vipi? Kwa nini tusiuite kwa jina lake sahihi - yaani WIZI? Tunataka kugeuza huu wizi kama tulivyogeuza rushwa mwaka 2005 na kuiita takrima?
Tuache kubadilisha maneno kwa kusudi la kupunguza makali. Kitu NEC walichoafanya katika huu uchaguzi ni WIZI na hatuhitaji kulipa jina/neno lingine!!
 
Chakachua ni dansi moja murua sana la siku nyingi kidogo, eighties babies wanaweza wasilifahamu.

Nasikitika limebambikwa maana mbaya hii.
 
utashangaa kuona wapinzani ndio hodari wa kutumia hilo neno ambalo kimaana liko dhaifu kuliko kusema kura zimeibiwa.

kama hatutaki kusema zimeibiwa kwa kuona ni kali sana, basi yatumike maneno kama "kumekuwa na vitendo vya udanganyifu"
 
hakuna cha kusema ni kali sana...tunaongea UKWELI!
 
Back
Top Bottom