Sinkala
JF-Expert Member
- Dec 22, 2008
- 1,773
- 683
Nimekuwa nikipata mkanganyiko kuhusu matukio ambayo yanastahili kuimbiwa ubeti mmoja na yale yanayostahili beti zote mbili za wimbo wa Taifa wa Tanzania. Utakuta wakati wa tukio fulani linaimbwa beti moja (Mungu ibariki Tanzania) na wakati mwingine zinaimbwa zote (Mungu ibariki Afrika kwanza halafu Mungu ibariki Tanzania mwisho).
Afadhali hata ukiimbwa kwa instrumental, si rahisi kujua unaoimbwa ni upi. Hali inakuwa mbaya iwapo wimbo utaimbwa kwa vocal, kwani hapa kila mtu ataanza kivyake, mwingine Afrika na mwingine Tanzania, huyu atasema Wabariki viongozi wake, na yule atasema Dumisha Uhuru na Umoja.
Sasa waungwana, naombeni mnifafanulie matukio yapi yanastahili beti ngapi, maana ni aibu kuimba mbele ya wageni kutoka nje, huku wakishuhudia jinsi ambavyo hatujui wimbo wetu !!