Kwa nini tunaendelea kuwapigia kura viongozi ambao hawaperform ktk kipindi chao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini tunaendelea kuwapigia kura viongozi ambao hawaperform ktk kipindi chao

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FirstLady1, Sep 29, 2009.

?

kwanini tunaendelea kuwapigia kura

 1. kwanini

  1 vote(s)
  100.0%
 2. tunawapigia

  0 vote(s)
  0.0%
 3. kura

  0 vote(s)
  0.0%
 4. viongozi

  0 vote(s)
  0.0%
 1. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Nashangaa nasikitika na sipati majibu kabisa
  Hivi huwa ni akili zetu watanzania au ??
  Tunaelewa kabisa huyu ni mbunge wetu whatever lakini katika kipindi chake cha miaka 5/10 or more hajafanya lolote zaidi ya kulala na kutowakilisha hoja zetu |Bungeni kijijini au maeneo yetu hayatamaniki ,hatuna maji ,umeme,barabara mbovu magari hayapiti ,hatuna mahospital ,kina mama wajawazito na watoto wanateseka ..ni matatizo yanayoonekana bila kificho
  Inakuwaje bado tunaendelea kuwapigia kura na kuwaweka madarakani?:confused::mad:
  Inakuwaje lakini??
   
 2. E

  Exaud Minja Member

  #2
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Kwasababu ya laana tuliyonayo ya kutokujua tunachokifanya.
  Kinachotakiwa ni maombi kwa ajili ya kuondoa laana kwanza baada ya hapo tuombe kwa Mungu atupe uwezo wa kujua kuchagua Viongozi watakao weza kutufanyia kazi na sio Viongozi tunaowafanyia kazi sisi kwa ajili ya kujaza matumbo yao.

  Na waliochagua kwa ajili ya ushabiki wa chama inawabidi watubu kwa sababu ni dhambi kubwa sana waliotufanyia watanzania.
   
 3. M

  Mzee Mwafrika Senior Member

  #3
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 168
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  mbona hiyo poll haijakaa vizuri!ebu irekebishe maana sioni options!mi nadhani ni kwa sababu hatuoni mbadala ya hao wanaotutawala.yani nisipompigia nitampigia nani tena?wote walewale!nadhani tunahitaji mbadala wa hawa tulionao leo na sio upinzani njaa!
   
 4. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #4
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,054
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280

  My darling first lady, Hivi Nilivokwambia sitapiga tena kura kumbe hukunielewa? Hata usipowapigia kura hao wadudu, lazima watashinda tu. Maboksi ya kura wametengeneza wao, wanayasafirisha wao, kura wanazihesabu wao, mawakala wanawalipa wao (kifisadi), mtangaza matokeo ni mtu wao, ukienda mahakamani utakuta watu wao, wanaapishwa na watu wao,........ Kila kitu chao. Unategemea nini?

  Siku ya kupiga kura ungana nami kuchapa mtindi tuongeze damu mwilini kuliko kusimama juani kukausha damu mwilini buuuuuure wakati tutakaowapigia kura hata tufanye nini hawatatangazwa washindi.
   
 5. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #5
  Sep 29, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Kwasababu wanakuja na takrima na somo la uraia hatulijui
   
 6. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #6
  Sep 29, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Khanga, Vitenge, Tshirts, Pilau.......Wananchi either tumelogwa au we are simply not serious kuhusu maisha yetu.
  Tunahitaji maombi ya kuvunja hii laana kwa kweli inauma sana!
   
 7. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #7
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,054
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Mkuu, hilo la takrima nakuunga mkono lakini hilo la somo la uraia......... hapana. Hapa hata ulijuaje somo hilo, bila kubadili system nzima kuanzia ya tume ya uchaguzi. Vimejaa wizi mtupu!
   
 8. K

  K4jolly JF-Expert Member

  #8
  Sep 29, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 366
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wengine wanachaguliwa wakiwa wazuri tuu na wananchi wanawaamini, lakini akishaingia kwenye hiyo system anabadilika kama kinyonga.

  Ila siasa ni mbaya ukiwa msema ukweli unachakazwa kama Mrema au unafatiliwa hadi uvunguni kama Mh. Slaa.
   
 9. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #9
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,421
  Likes Received: 3,770
  Trophy Points: 280
  Sababu ni hizi.........

  1. Kipindi cha uchaguzi ndiyo utaona TV zote zinaonyesha vita, huku zikitangaza kuwa kumchagua yeyote nje ya CCM ni kutaka vita. Kwa vile hatujazowea vita, lazima tuogope. We angalia mabomu ya mbagala yalivyotuhangaisha..............

  2. Takrima au rushwa

  3. Elimu ya uraia hatuna kabisa

  4. Watanzania wanaojuwa haki zao kwa mujibu wa katiba ni wachache sana.

  5. Mazoea.

  6. We are actually fearing risks za kuiondoa CCM.

  7. Wagombea wa upinzani huwa wanasimamishwa bila kuangalia kama wanakubalika eneo husika.

  8. Kwa vile hatujui haki zetu, tunadhani tunavyopata vinatokana na uwepo wa CCM, hivyo kuwaondoa kunamaanisha kuvikosa. Usishangae kumsikia mtu akisema "CCM imekusomesha, imekuletea amani n.k.........."
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  mie hata sijui imekaaje maana imetokea tu wakati na post ikanipa option habu nifundishe kidogo Mtu wangu
   
 11. E

  Exaud Minja Member

  #11
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 84
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Hii kitu mpya ya kuandaa documents zote za kupigia kura ndugu zangu kama kweli wizi wa kura upo masanduku ya kura zilizopigwa yapo tayari.

  Labda wasimamizi na wahesabu kura wasiwe watanzania masikini wanaorubuniwa kwa baiskeli.

  Naogopa kusema sana napoteza muda wangu. Nashawishika kutokukaa foleni kwa ajili ya kupiga kura.

  Tangu nianze kupiga kura kura yangu haijawahi kushinda.
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  kama ni laana kwa nini wote tusifunge katika dini zetu tukemee hii laanna ambayo imekithiri ??
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,054
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280

  Grrrrrr!!!!! Mkuu unataka kutuambia hao wanaosimamishwa na CCM wanakubalika? Mgombea wa upinzani hata akubalike vipi, siku ya siku atapigwa mweleka!

  Rejea uchaguzi wa 1995 NCCR Mageuzi ya kina Lamwai, Marando na Mrema walivyoliteka jiji la Dar badala yake uchaguzi wa Dar ukafutwa. Au angalia wa 2000 John Mnyika alivyomchachafya Keenja kule Ubungo na mizengwe ilivyoibuka. Ukitaka kushangaa zaidi rejea uchaguzi na matokeo ya Busanda na Biharamulo.

  Mi nakwambieni niacheni nigome kupiga kura niiridhishe nafsi yangu! aggrrrrrr!!!
   
 14. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #14
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  ila am so confused inakuwaje katika akili ya kufikirika tunaendelea kufanya hivi .wakati mabadiliko matunda na mafanikio hayaonekani

  kuna Mbunge mmoja kaja hapa wa CCM kanunua masanga kwa vijana vijana baada ya kulewa wakaanza kumzomea :)lakini kuzomea tu haisaidii ni vitendo zaidi ndo vinatakiwa ili kuleta mabadiliko ktk nchi hii
   
 15. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #15
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280
  Tunadanganyika ??
   
 16. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #16
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,054
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Umevaa viatu vyangu mkuu!
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Sep 29, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,054
  Likes Received: 24,060
  Trophy Points: 280
  Join me kugoma kupiga kura. Labda ndio solution pekee iliyobakia. Ikitokea mbunge kachaguliwa na watu mia kwenye jimbo lenye watu laki saba labda ulimwengu utashtuka halafu kitaeleweka.
   
 18. Kobe

  Kobe JF-Expert Member

  #18
  Sep 29, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 1,756
  Likes Received: 361
  Trophy Points: 180
  Tunakosa fikra sahihi japo tunajua jukumu la kumchagua kiongozi aliyebora lipo kwetu.
  Pili tunaweza kuw sie tunafanya kilicho sahihi lakini kuna dhulma inafanyika kati ya viongozi wanaogombea madaraka kwa kuiba ama kura au kubadilisha matokeo wakishirikiana na Chombo husika katika kusimamia chaguzi zetu.
  kingine inaweza kuwa tunadanganyika na vitu vidogo (wengi wetu) kama Khanga,fulana,vyakula na hata pesa pindi chaguzi zinapowadia nalabda kuna ile kitu mapenzi kupindukia kwa wagombea dhidi ya wapiga kura pasi na kuangalia nini cha kufanya(ujamaa,undugu,urafiki) ilhali baadae utalalamika juu ya uongozi wa huyo uliyemchagua.
  Kumbe na la msingi tunabidi Tubadili FIKRA zetu sasa.
   
 19. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #19
  Sep 29, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,421
  Likes Received: 3,770
  Trophy Points: 280
  Uliyoyasema ni kweli lakini, tuna vingi sana vinavyosababisha na unaweza ukaona kila mahali pana at least sababu moja kati ya hizo nilizozitaja. Kukaribia kura za mpinzani wako si kushinda. Kinachotakiwa ni kupata kura zaidi yake...... na si chenga twalawa ...........lakini kufungwa .......... twafungwa
   
 20. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #20
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 543
  Trophy Points: 280

  hawakubariki hata kidogo mie mbunge wetu lol kimeo lakini ndo mauzauza yayotokea everyday
   
Loading...