Kwa nini tunaagiza magari kwa zaidi ya M300 na kisha kuyauza kwa M5 tena ndani ya mwaka?

Paulsylvester

JF-Expert Member
Oct 15, 2021
1,467
3,381
Tusiwe wanafiki, Elimu zetu mmiliki wake huwenda ni shetani!

Na Kwa bahati mbaya shetani hana mazoea na watu eti waishi vizuri na Kwa raha!

Serikali zetu endapo watu wake wangelikuwa na nia ya kuzitoa nchi zetu kwenye Lindi la umasikini wa watu wao! Basi kusingelikuwepo na matumizi makubwa mabaya na ya anasa Kwa vitu vya anasa

Nazungumizia magari yanayokuwa yakiagizwa na Serikali, nilisikiliza mchango wa mbunge mmoja akichangia hoja ya serikali kuhusu kampuni zinazopewa tenda za ununuzi wa magari ya serikali, alisema, Wizara moja tu ya Afya mwaka Jana ilikuwa imeagiza magari zaidi ya 600.

Na magari Yale humunuliwa na serikali Kwa million 300 Kwa kila moja,

Hicho hakinishangazi sana, kinachonipa taabu sana akilini ni hichi!

Unanunua gati Kwa kodi za wananchi Kwa bei kubwa kama hizi, siku umetangaza mnada wa kuyauza baada tu ya serikali kuona yanawadhalilisha Kwa sabb tu rangi zake ama toleo hilo halifai tena, yanauzwa Kwa bei sawa na bule!

Na tena wanaouziwa, ni walewale watumishi wa serikali Kwa bei ya million 5 tena ndani ya mwaka mmoja imeenda sana mmoja na nusu ama miwili!

Huku ni kuendelea kutufilisi walipa kodi!

Haiwezekani gari uagize Kwa mamilioni ya fedha na ndani ya mwaka unauza Kwa mugawa kama njugu!

Siku tukipiga hatua, shetani atatushangaa imekuwaje maana kakamata akili za wachumi wa nchi hii!
 
Acha uongo hamna gari inayonuniliwa na kumaliza miaka 1 au 2 kisha inauzwa.Magari mengi chakavu wanayouziwa Watumishi ni shakavu tena chakavu kweli na mengi unakuta yamisha tumika zaidi ya 20 years.Sasa gari iliyotumika takribani miaka 20-25 unataka liuzwe kwa shs ngapi,vilevile lazima utambue magari mengi ya Serikali yanatumika kila Sikh tofauti na magari ya Kampuni au watu binafsi.

Aidha,kuhusu kila gari kununuliwa kwa 300M napo ni uongo ,magari mengi yanayonunuliwa na Serikali na Hard Top ambazo bei zake zana range kati ya 120-150M.Hizo 300M ni kwa akili ya ununuzi wa Ma V8 -kwa ajili ya viongozi.
 
Back
Top Bottom