Kwa nini tume ya Kuchunguza matatizo ya mikopo haina mwanafunzi hata moja? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa nini tume ya Kuchunguza matatizo ya mikopo haina mwanafunzi hata moja?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by STEIN, Feb 8, 2011.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tumeona tume ya kuchunguza matatizo ya mikopo haina mwakilishi wa wanafunzi hata mmoja. Ni jambo la kushangaza kuona tume imejaa upande mmoja tu wa CCM na serikali hata wanafunzi wangeshirikishwa kwa sababu ndio wahanga wa hayo matatizo ya bodi na baadhi ya vyuo vinahusika moja kwa moja na unyanyasaji wanaofanyiwa wanafunzi.

  Hii tume haitakuwa na jipya kwani matokeo au mapendekezo yake yatachakacchuliwa tu, kwa hiyo wanafunzi wasitegemee jipya hata kidogo kwani ni ya watu wale wale.


  1. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar-es-Salaam Profesa Makenya Maboko.
  Wajumbe ni

  2.Masoud Mohamed Haji ambaye ni Ofisa Mahusiano wa Kimataifa,

  3.Dk. Eliawony Kristosia Meena, mhadhiri mwandamizi Chuo Kikuu cha Tumaini Arusha na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Zanzibar.
  4.Paul Daniel Magwiza, Naibu Katibu Tume ya vyuo vikuu,

  5.Sarah Baharamoka, Mkurugenzi Msaidizi Uandishi Sheria, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,

  6.Profesa Penina Mlama, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa tawi la Tanzania la taasisi inayopigania elimu kwa wanawake.
  7.Deo Mbasa Daud ambaye ni ofisa taaluma wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha, 8.Kassim Almasi Umba, ambaye ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kiislamu Morogoro.
  9.Anderson Mlabwa ambaye ni Mkurugenzi wa Mikopo Benki ya CRDB.
  10.Profesa Wilbert Abel Mkurugenzi wa Elimu ya Juu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi pamoja.
  11.Rosemary Rulabuka ambaye ni Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu.

  Masomo mema
   
 2. n

  nndondo JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  huyu JK anamatatizo jamani upuuzi na udini ndivyo vinavyomtawala, sasa hebu angalia hata hiyo listi iliyokosa wanafunzi huyo masourd hapo anafanya ninie eti afisa uhusiano wa kimatafa hicho ni cheo gani? unaona kabisa wakati wenzake wana address yeye hola yaani anapendelea mpaka anatia kinyaa this guy anamatatizo na kutia aibu kabisa yaana hafanyi kitu bila kuharibu kila mmoja hapo utaona kazi yake na justification huyu hata huelewi mwe, nakubaliana na lipumba kwamba huyu kavunja rekodi ya ubovu wa kuongoza kabisa.
   
 3. Unyanga

  Unyanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mkuu tunaomba source na hichho ulichokiandika hapo juu, mnapenda kulaumu kila kitu tusemeni kweli basi, hiyo tume inayo wawakilishi wanafunzi na mmoja wa wajumbe hao upande wa wanafunzi ni bwana sylvanus waziri wa mikopo ktk serikali ya wanafunzi udsm na anafanya kazi na kamati hiyo, mie pia ni kiongozi mwenzake hapa udsm ndio maana nayafahamu haya upo hapo mzee?
   
Loading...